Nimepata kazi ya millioni 10, nifanyeje kuutoroka umasikini?

Hii nimeiweka kwenye droo kwanza.
Lakini pia mkuu hizi hatifungamani,hisa pia huongezeka thamani na unaweza kuombea mkopo pia.
Hazihitaji usimamizi pia.

Na uzuri wake sio kubaharisha unakuwa na uhakika wa muongezeko wa thamani kwa kiasi kadhaa.

Ni kweli ardhi inaongezeka thaman lakini kuijua ipi itaongezeka na ipi haitaongezeka ndiyo mtihani.
Kuna ndugu yangu mwaka 98 aliambiwa achague kiwanja Mbagala au Goba, yeye akachagua Mbagala rafiki yake akachukua kile cha goba kwa laki 2.
Hakupenda Goba maana ilikuwa mapori tu kidogo mbagala kumechangamka.

Yule rafiki yake alikuja kuuza pale goba kwa million 40
 
mkiandikaga upuuzi km huu mnapata malipo yoyote? Mtu mzima mwenye akili zako utaandikaje utumbo km huu, hizi ni dharau dogo uwe na adabu
 
Okay,nielezee kidogo hiyo nidhamu nitakayoipata kwenye uislam na itanisaidiaje kuutoroka umasikinì.
Keep in mind,kuna masikini wengi tu wenye nidhamu
Kwanza kabisa katika Uislam utatakiwa kuwachana na pombe, kamari, uasherati na uzinzi. Vyote hivyo ni haramu.


Hivyo ndivyo vichocheo vikubwa vya umasikini.
 
Kwanza kabisa katika Uislam utatakiwa kuwachana na pombe, kamari, uasherati na uzinzi. Vyote hivyo ni haramu.


Hivyo ndivyo vichocheo vikubwa vya umasikini.
Asante, lakini madam kuna watu hawafanyi vyote hivyo lakini bado ni masikini.
Na kuna watu wanafanya vyote hivyo na bado wanazidi kutajirika mfano Diamond.

Unaweza kunisaidia labda mbinu gani uislam unafundisha katika uwekezaji au biashara ili kumfanya mtu kuwa tajiri?

Maana naona ni kweli waarabu wako vizuri kwenye biashara
 
Ukifika Kigoma karibu niwe mwenyeji wako tupate na muda wa kushauriana kuhusu Investment.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…