Nimepata matatizo lakini hakuna Ndugu yangu aliyekuja wala kupiga Simu ya pole

Pole sana ndugu zetu ndo walivyo tunaishi nao tu,ukija fanikiwa utaskia lawama!
 
Kweli mkuu, sasa sijui wanafanya hivyo kwakuwa wanapesa? Maana hao ninao waongelea wanapesa hivyo wanajiona matawi japo mimi nilikuwa napenda kuwajulia hali. Chakushangaza sasa ninao elewana nao mimi ni wale wenye maisha ya kawaida kama mimi.
Stick to your lane.
 
Habari zenu? Kunakipindi nilileta uzi huu, Ndugu zangu nashindwa kuwaelewa
Baada ya kuvuta jiko niliishi na mke wangu, mwezi wa 11/2021 tulibahatika kupata mtoto na mke wangu, sikuwa na hiyana niliona japo ndugu zangu walinikosea kiasi fulani acha niwataarifu japo mke wangu alipata PPH (Postpartum Haemorrhage) nusura afe niliwataarifu pia kuhusu hayo matatizo lakini hawakujari na wala mke wangu hakupigiwa sim wala kuulizwa chochote.

Baadae nilisema isiwe kesi acha niendelee kutulia kimya nikaamua kutokuwatafuta tena, pia japo nilifiwa na baba niliandika kwenye uzi hiyo link juu, baada ya kutoka msibani hakukuwa na mtu aliye kuja kunipa pole hasa mama yangu mdogo wala wajomba zangu hakuna na wala eti waulizie kuhusu mtoto wangu anaendeleaje hakuna.

Baada ya kuona hivyo nilitulia tulii, juzi kati mamdogo wangu ananipigia na kunilazimisha nimpeleke mke wangu na mtoto wangu kwake, pia naambiwa mtoto wa mjomba anafunga ndoa mwaka huu hivyo nijiandae kirohoni nikanisemea hivi hawa wananichukuliaje? Nimepata msiba hawajaja na baadhi yao hajanipigia sim kunipa pole, haya mke wangu alijifungua na akapata matatizo na niliwataarifu hakuna aliye toa pole na wala kujali.

Nawasilisha wakuu, hiyo ni sahihi? Pia kunamambo mengi tu sema siwezi andika wakuu [emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]
 
Baada ya kuvuta jiko niliishi na mke wangu, mwezi wa 11/2021 tulibahatika kupata mtoto na mke wangu, sikuwa na hiyana niliona japo ndugu zangu walinikosea kiasi fulani acha niwataarifu japo mke wangu alipata PPH (Postpartum Haemorrhage) nusura afe niliwataarifu pia kuhusu hayo
Piga chini Mambo ya ndugu ukiendekeza hufanyi kitu na utakuwa na vinyongo,which means itakutafuna mwenyewe. Same damn thing nilichowahi kupitia wakati wa uzazi wa mwanangu wa kwanza mpaka ndoa them mtoto wa pili.

Kwanza ndoa hakuja mtu japo walikuwa wanataarifa (Labda kwa sababu sikufanya iwe ya mbwembwe hawajazoea,nikafanya na watu wachache hawakuzidi 15) Wife kujifungua kuna mmoja mke wa bro alikuwa na taarifa ya kukaribia kujifungua,siku namchek hayuko hewani,nikampigia mume wake(bro) akakausha.

Nikamuhudumia wife mwenyewe mpka siku 14 akasema Yuko fresh nikarudi na ratiba yangu ya awali. Ushauri wangu; wakikushirikisha,halafu moyo ukaona linakuingia wape support. Moyo ukikataa achana nao. Nilishasema najua wengi tunaogopa kutengwa na ndugu jamaa tukihisi Labda tutakosa watu wa kutustili tukifa.

Nikwambie tu acha uoga hata munispal ofisi ya jiji Ina kitengo Cha kuzika watu wasio na ndugu.
 
watu wengi tunafeli sana kwasababu tunafanya mambo kwa kutegesha, hatuwezi fanikiwa.

Tufanye bila manung'uniko jamani, hapa duniani tunapita.

Usisubiri waje au wakupigie simu ya pole, wee endelea na mabo yako na hata wakikualika wewe tenda wema, usirudishe ubaya ndugu yangu
 
Pole mkuu hayo mambo ya kawaida tu kutokea ww umefanya kwa sehemu yako kama hawaoneshi kusaidia basi waache tu endelea na wale wanaonesha kukusikiliza na kukusaidia.
 
Mkuu, pole sana kwa yaliyokukuta.

Ila ushauri wangu: Mambo kama hayo usipende kuyaweka-weka hadharani?

Wengi wamepitia huko!

Nakuambia ukweli: Baadhi watatumia kulialia kwako kama faida ya kuja kwako na kujifamya waungwanaaa! Kukusikitikia kwingiii! kumbe wanazidi kukusanifu!

Achana nao! take your time!
 
Maisha yamebadilika sana mkuu, ndugu sikuhizi siyo wale wa damu tu, ndugu ni yule aliye tayari kuwa na wewe wakati wa shida na raha bila kujali.

Ukipata watu wa aina hiyo hatakama siyo ndugu yako wa damu ishi nao vizuri.

Mindset uliyonayo ya kutaka ndugu wa damu waonyeshe ushirikiano na kukujali kwa kila jambo kwasababu tu ni ndugu /wana ukoo, hiyo mindset ondoa kabisa na kuwa flexible kuishi nao jinsi walivyo.

Siyo ndugu tu, hata marafiki pia, kuwa flexible kuishi nao jinsi walivyo, yaani usilazimishe kuwa na umuhimu katika maisha ya wengine.

Shida zipo na huwezi kosa mtu hata mmoja wa kukupa support.

Hao wachache walio tayari kuwa na wewe komaa nao, ambao wako bize na maisha yao waache waendelee na maisha yao.

Usipokuwa na umuhimu katika maisha ya mtu usitegemee ataonyesha kujali na kukupa muda wake, hivyo achana na habari ya kuamini ndugu wa damu LAZIMA wawe upande wako kila wakati.

Ulimwengu umebadilika sana, mind your own business na ishi kutafuta amani ya moyo wako na siyo kutafuta ndugu.

Huwezi pendwa na wote, hata Yesu mwana wa Mungu hakupendwa na wote, wewe ni nani kila mtu akupende na kujali matatizo yako??

ISHI MAISHA YAKO, ALIYE UPANDE WAKO NENDA NAYE, ASIYE UPANDE WAKO ACHANA NAYE.

Kikubwa USIWACHUKIE. Kubali tu uhalisia wao na uendelee na maisha yako.

Hiyo mialiko kama imetoka kwa watu ambao hawakuonyesha kukujali wakati wa matatizo na wewe USIENDE, endelea na maisha yako.

Kama ipo pesa ya ZIADA wachangie kidogo waambie ratiba zimebana ila kama pesa uliyonayo una bajeti nayo muhimu USITOE.

Ukiishi kutaka kumfurahisha kila mtu huwezi ishi kwa amani kamwe.
Mkuu uliochoandika ndio uhalisia,nashauri azingatie haya
 
ndugu yako ni yule anaekuchukulia kiubinadamu ila hawa tunaotoka nao utotoni especialy wale waliokuwaga wababe enzi hizo ghafla ukubwani ukawazidi kete hao ni mwiba km sio vidonda vy tumbo basi.
 
Tafakari njia zako labda we ni kikwazo uhakika zaidi ni kuwauliza majibu wanayo
 
Habari zenu? Kunakipindi nilileta uzi huu, Ndugu zangu nashindwa kuwaelewa
Baada ya kuvuta jiko niliishi na mke wangu, mwezi wa 11/2021 tulibahatika kupata mtoto na mke wangu, sikuwa na hiyana niliona japo ndugu zangu walinikosea kiasi fulani acha niwataarifu japo mke wangu alipata PPH (Postpartum Haemorrhage) nusura afe niliwataarifu pia kuhusu hayo matatizo lakini hawakujari na wala mke wangu hakupigiwa sim wala kuulizwa chochote.

Baadae nilisema isiwe kesi acha niendelee kutulia kimya nikaamua kutokuwatafuta tena, pia japo nilifiwa na baba niliandika kwenye uzi hiyo link juu, baada ya kutoka msibani hakukuwa na mtu aliye kuja kunipa pole hasa mama yangu mdogo wala wajomba zangu hakuna na wala eti waulizie kuhusu mtoto wangu anaendeleaje hakuna.

Baada ya kuona hivyo nilitulia tulii, juzi kati mamdogo wangu ananipigia na kunilazimisha nimpeleke mke wangu na mtoto wangu kwake, pia naambiwa mtoto wa mjomba anafunga ndoa mwaka huu hivyo nijiandae kirohoni nikanisemea hivi hawa wananichukuliaje? Nimepata msiba hawajaja na baadhi yao hajanipigia sim kunipa pole, haya mke wangu alijifungua na akapata matatizo na niliwataarifu hakuna aliye toa pole na wala kujali.

Nawasilisha wakuu, hiyo ni sahihi? Pia kunamambo mengi tu sema siwezi andika wakuu [emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]
Wewe ndio mwenye tatizo, wanaukoo wote haiwezekani wakutenge pasipo na sababu
 
Namthamini na kumuamini rafiki kuliko ndugu

Maumivu niliyopata kutoka kwa wanaoitwa ndugu ni makali mno ningekuwa wewe hata nisingejishughulisha nao kabisa
 
Habari zenu? Kunakipindi nilileta uzi huu, Ndugu zangu nashindwa kuwaelewa
Baada ya kuvuta jiko niliishi na mke wangu, mwezi wa 11/2021 tulibahatika kupata mtoto na mke wangu, sikuwa na hiyana niliona japo ndugu zangu walinikosea kiasi fulani acha niwataarifu japo mke wangu alipata PPH (Postpartum Haemorrhage) nusura afe niliwataarifu pia kuhusu hayo matatizo lakini hawakujari na wala mke wangu hakupigiwa sim wala kuulizwa chochote.

Baadae nilisema isiwe kesi acha niendelee kutulia kimya nikaamua kutokuwatafuta tena, pia japo nilifiwa na baba niliandika kwenye uzi hiyo link juu, baada ya kutoka msibani hakukuwa na mtu aliye kuja kunipa pole hasa mama yangu mdogo wala wajomba zangu hakuna na wala eti waulizie kuhusu mtoto wangu anaendeleaje hakuna.

Baada ya kuona hivyo nilitulia tulii, juzi kati mamdogo wangu ananipigia na kunilazimisha nimpeleke mke wangu na mtoto wangu kwake, pia naambiwa mtoto wa mjomba anafunga ndoa mwaka huu hivyo nijiandae kirohoni nikanisemea hivi hawa wananichukuliaje? Nimepata msiba hawajaja na baadhi yao hajanipigia sim kunipa pole, haya mke wangu alijifungua na akapata matatizo na niliwataarifu hakuna aliye toa pole na wala kujali.

Nawasilisha wakuu, hiyo ni sahihi? Pia kunamambo mengi tu sema siwezi andika wakuu [emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]
Mkuu usiwategemee ndugu ,

Mtoto wako ndy ndugu yako wa kweli,

wengine wanafata uwezo wako wa kimaisha.

Mfano pesa,kazi yako nk.
 
We nae unatuchosha sasa vitu vingine unaamua kama mwanaume sie tushakwambia atayekupenda mpende huyohuyo mtu hakujali ya nini kuhangaika naye? mbona kujiongezea majukumu yasokuhusu? ndo maana mnakufa haraka

Yaani una mke na mtoto bado unahangaika na ndugu kwani hakuna marafiki wanaoweza kukusaidia kipindi cha shida mpaka ndugu zako? kwani mkeo naye hana ndugu?
 
Back
Top Bottom