Nimepata matatizo lakini hakuna Ndugu yangu aliyekuja wala kupiga Simu ya pole

Pole sana ndugu zetu ndo walivyo tunaishi nao tu,ukija fanikiwa utaskia lawama!
 
Kweli mkuu, sasa sijui wanafanya hivyo kwakuwa wanapesa? Maana hao ninao waongelea wanapesa hivyo wanajiona matawi japo mimi nilikuwa napenda kuwajulia hali. Chakushangaza sasa ninao elewana nao mimi ni wale wenye maisha ya kawaida kama mimi.
Stick to your lane.
 
 
Piga chini Mambo ya ndugu ukiendekeza hufanyi kitu na utakuwa na vinyongo,which means itakutafuna mwenyewe. Same damn thing nilichowahi kupitia wakati wa uzazi wa mwanangu wa kwanza mpaka ndoa them mtoto wa pili.

Kwanza ndoa hakuja mtu japo walikuwa wanataarifa (Labda kwa sababu sikufanya iwe ya mbwembwe hawajazoea,nikafanya na watu wachache hawakuzidi 15) Wife kujifungua kuna mmoja mke wa bro alikuwa na taarifa ya kukaribia kujifungua,siku namchek hayuko hewani,nikampigia mume wake(bro) akakausha.

Nikamuhudumia wife mwenyewe mpka siku 14 akasema Yuko fresh nikarudi na ratiba yangu ya awali. Ushauri wangu; wakikushirikisha,halafu moyo ukaona linakuingia wape support. Moyo ukikataa achana nao. Nilishasema najua wengi tunaogopa kutengwa na ndugu jamaa tukihisi Labda tutakosa watu wa kutustili tukifa.

Nikwambie tu acha uoga hata munispal ofisi ya jiji Ina kitengo Cha kuzika watu wasio na ndugu.
 
watu wengi tunafeli sana kwasababu tunafanya mambo kwa kutegesha, hatuwezi fanikiwa.

Tufanye bila manung'uniko jamani, hapa duniani tunapita.

Usisubiri waje au wakupigie simu ya pole, wee endelea na mabo yako na hata wakikualika wewe tenda wema, usirudishe ubaya ndugu yangu
 
Pole mkuu hayo mambo ya kawaida tu kutokea ww umefanya kwa sehemu yako kama hawaoneshi kusaidia basi waache tu endelea na wale wanaonesha kukusikiliza na kukusaidia.
 
Mkuu, pole sana kwa yaliyokukuta.

Ila ushauri wangu: Mambo kama hayo usipende kuyaweka-weka hadharani?

Wengi wamepitia huko!

Nakuambia ukweli: Baadhi watatumia kulialia kwako kama faida ya kuja kwako na kujifamya waungwanaaa! Kukusikitikia kwingiii! kumbe wanazidi kukusanifu!

Achana nao! take your time!
 
Mkuu uliochoandika ndio uhalisia,nashauri azingatie haya
 
ndugu yako ni yule anaekuchukulia kiubinadamu ila hawa tunaotoka nao utotoni especialy wale waliokuwaga wababe enzi hizo ghafla ukubwani ukawazidi kete hao ni mwiba km sio vidonda vy tumbo basi.
 
Tafakari njia zako labda we ni kikwazo uhakika zaidi ni kuwauliza majibu wanayo
 
Wewe ndio mwenye tatizo, wanaukoo wote haiwezekani wakutenge pasipo na sababu
 
Namthamini na kumuamini rafiki kuliko ndugu

Maumivu niliyopata kutoka kwa wanaoitwa ndugu ni makali mno ningekuwa wewe hata nisingejishughulisha nao kabisa
 
Mkuu usiwategemee ndugu ,

Mtoto wako ndy ndugu yako wa kweli,

wengine wanafata uwezo wako wa kimaisha.

Mfano pesa,kazi yako nk.
 
We nae unatuchosha sasa vitu vingine unaamua kama mwanaume sie tushakwambia atayekupenda mpende huyohuyo mtu hakujali ya nini kuhangaika naye? mbona kujiongezea majukumu yasokuhusu? ndo maana mnakufa haraka

Yaani una mke na mtoto bado unahangaika na ndugu kwani hakuna marafiki wanaoweza kukusaidia kipindi cha shida mpaka ndugu zako? kwani mkeo naye hana ndugu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…