Nimepata matatizo lakini hakuna Ndugu yangu aliyekuja wala kupiga Simu ya pole

Kitendo cha kukupeleka shule ya vipaji bado alikuwa anakujali sema shida ni pale mtu unataka akufanye kama mtoto wake ridhika kwa hichohicho alichotoa maana angekuwa baba yako usingesema alikuwa hakujali
 
Mkuu shida sio kupelekwa shule kilicho niuma sana sana ni pale nafiwa na baba yangu mzazi ambaye ni kaka yake hakuja msibani. Na kwenye upande wa mama baba alivyo fariki hawakuja msibani pia je' kwa wewe utajisikiaje?
 
Asant kwa ushauri mkuu
 
Kama wana pesa basi wapotezee tu Mkuu.. Ukiwaendekeza hawakawii kusema unajipendekeza kwao..

Kwani maisha yako bila wao unaona hayawezekani?
Nikweli mkuu ila shida inakuja huyo mamdogo ananilazimisha nimpeleke mtoto na mke wangu, sasa na mimi nikifikiria mke wangu alipata shida na hawakumjulia hali hata kuuliza mtoto anaendeleaje? Et leo hii nimpeleke mtoto na mke wangu kwao.
 
Kweli mkuu, sasa sijui wanafanya hivyo kwakuwa wanapesa? Maana hao ninao waongelea wanapesa hivyo wanajiona matawi japo mimi nilikuwa napenda kuwajulia hali. Chakushangaza sasa ninao elewana nao mimi ni wale wenye maisha ya kawaida kama mimi.
Kumbe jibu unalo jaribu kuwa bize kujenga maisha yako na familia yako hao unaowazungumzia unaweza kukuta hawajawahi hata kidogo kukuwaza kama ni ndugu yao.
 
Kumbe jibu unalo jaribu kuwa bize kujenga maisha yako na familia yako hao unaowazungumzia unaweza kukuta hawajawahi hata kidogo kukuwaza kama ni ndugu yao.
Kweli mkuu ngoja nipambane na maisha yangu aisee
 
Mkuu shida sio kupelekwa shule kilicho niuma sana sana ni pale nafiwa na baba yangu mzazi ambaye ni kaka yake hakuja msibani. Na kwenye upande wa mama baba alivyo fariki hawakuja msibani pia je' kwa wewe utajisikiaje?
Sasa unataka ufanyeje kama wamekataa kuja? Kunywa sumu basi ufe ili wajue umechukia.
 
Mkuu shida sio kupelekwa shule kilicho niuma sana sana ni pale nafiwa na baba yangu mzazi ambaye ni kaka yake hakuja msibani. Na kwenye upande wa mama baba alivyo fariki hawakuja msibani pia je' kwa wewe utajisikiaje?
Kumbe unajua cha kufanya,simple kuwa mwanaume basi nenda na atayeenda na wewe usiishi kutaka kumfurahisha mwanadamu
 
Pole sana, nahisi nawe hauna tu hela kama mimi.....mara nyingi ndugu wapo kama panya wa SUA wananusa penye hela.

Ukiwa na hela ukikohoa tu ndugu na marafiki wanajaa kukujulia hali, ukiwa na hela daktari atakuja kukuona bar na kukupa tiba, ukiwa na hela mwanasheria atakufata hata night club kukusikiliza shida.

Ishi maisha yako anaekujali mjali, anaekutafuta mtafute, asiekujali akafie mbele usientertain mambo ya miungu watu.
 
Wakwende zao huko[emoji1787]
 
lipa mema kwa mabaya kisasi si chetu ni cha Mungu,duniani tunavimbiana kwa mali na ujuaji ila tu wapitaji tu kuna leo na kesho unaweza usiwahitaji weww ila kizazi chako kikawahitaji,pole umeandika kihisia
 
Mkuu.

Usilipe ubaya kwa ubaya.

Ubaya hulipwa kwa wema.

Yangu ni hayo tu
 
Unaweza kuta wewe ndo mwenye matatizo...jichunguze. inawezekana una mkono wa birika
 
Nenda nao sawa wale wanaoenda sawa na wewe, huwezi ukamfurahisha kila mmoja. Move on na maisha yako!

Sent using Samsung J1
 
May be wanamuona Hana hela
 
"Tusichoke kutenda mema,hata kama tuwatendeao wema uo hawathamini mema yetu,kwani mwisho wa mema yetu ni sisi na MUNGU sio sisi na wao"- By Mama Teresa.

Kawa unaweza kuwasaidia wasaidie kama sadaka sio kama mchango wa kawaida pia wasamehe kbs moyoni mwako, ukisamehe hutoangalia walifanya nn na nini,japo si kitu rahisi kwa watu waliyokuumiza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…