Nimepata milioni 30, mnanishauri nifanye biashara gani, mimi ni mwajiriwa, ili niweze kuacha kazi

Nimepata milioni 30, mnanishauri nifanye biashara gani, mimi ni mwajiriwa, ili niweze kuacha kazi

Wakuu habari.

Nimepata milioni 30, mnanishauri nifanye biashara gani, nimechoka kufanya kazi, nataka kujiajiri

Nawasilisha
Mkuu endelea na kazi tu huku iyo million 30 unafanya uwejezaji. Jaribu kuchuku hata million 15 weka bonus account NMB
 
Kwa sababu hujawahi kuipata unaweza kuiona ni nyingi sana. Subiri uipate ndipo utatuelewa tuna maana gani.
Biashara ninayomiliki mfaji wake ni 1/3 ya hiyo 30M and yet kwa mwezi nakunja zaidi ya 2M, nikiona mtu anaibeza 30M kwenye biashara moja kwa moja ni wale wazee wa biashara za kwenye makaratasi (sio wafanya biashara kwenye field).

Kuna jamaa yangu yupo Mwanza anamiliki kisehemu fulani ya kupata vyakula mbalimbali (kwa wale wenyeji wa mwanza, yupo maeneo fulani ya Sheli ya WEEKEND), anapata hela nzuri kwa mtaji ambao haukaribii hiyo 30M.

Biashara ni wateje tu, hata 5M inakuheshimisha, msilete ugumu ambao muda mwingine haupo.

NB: Biashara na kamari havikai chungu kimoja, nasema hivi kutokana uzoefu wangu wa moja kwa moja.
 
Hizo ndio zile kila service kwa Fundi au sio?,
Hizo mguu brake mguu fundi zinauzwa 10M to 15M
Mimi nazungumzia gari zilizorudisha hesabu mtu anauza anachukua mpya, na hazina mkorogo yaani sio town trip yaani zimetumia kwa tours tu.
 
Nikopeshe milion mbili nakurudishia 4.5 mil ndani ya mwezi mmoja..kwa mkataba wa kisheria kabisa..niko serious mkuu nicheki pm
 
Naendelea kupata ushauri wenu.
Nimepitia uzi wako nimeona ushauri mwingi sana ni vizuri.
Nami naandika hapa hapa ili kama nione mawazo ya wana jamvi,kuna mradi kama utaweza tuungane kuufanya maana nipo natafuta hela ila sijapata za kuufanyia,kuna kampuni moja sitaitaja na mkoa iliyopo nimeunganishwa nayo kuwapa huduma wafanya kazi wake walioko saiti,idadi yao kwa kuanzia hawapungui50, na malipo yatafanyika kwa mwezi,binafsi nimejaribu njia za kupata fedha sijapata ili niifanye hiyo kazi na ninauzoefu wa kuosha kuifanya(sijaitaja),kuna watu ambao nilitegemea wao waungane nami katika kazi hii maana waho wana nguvu za kiuchimi na ni waajiliwa wa serikali na mimi natamani hiyo kazi ili niendeshe maisha yangu,so naona kama hawajali japo wanapenda kuwa na kitega uchumi cha ziada kuwaingizia kipato,pia nilifungua nao kampuni ya kufanya huduma kama izo na kuna baadhi ya tenda nazisubilia lakini wao wanataka matokeo ya papo kwa papo,hawana subila.
Kama utaona vyema tutafutane tuone tunaifanyaje hii kazi na nakuhakikishia tutafanikiwa na wala utaweka fedha hiyo yote,.
Jambo la mwisho usiache kazi,kama utakuwa tayali kujua ni kazi gani na tutafanyeje na tukafanikiwa kufanya basi baada ya kuona matokeo ndani yamiezi miwili au mitatu unaweza sasa kuacha kazi maana utakuwa ushapata uzoefu ata baadae kila mtu kuwa na uwezo wa kufanya mwenyewe.
PIA MDA SIYO MREFU WANA JAMVI NITAKUJA KWENU KUOMBA MSAADA NA NITAKUJA NA MCHANGANUO KAMA NITAKUWA NIMEKWAMA NAOMBA MSIACHE KUNISAPOTI AU KUSHILIKIANA NAMI MAANA KAZI NANAZO ILA Mtaji imekuwa shughuli,
Ahsante [emoji122]
 
Mrejesho mkuu, ulifanya biashara gani?
 
Back
Top Bottom