Nimepata mshtuko mkubwa Ubungo Bus Terminal leo alfajiri!

Kwa size ya stendi ya ubungo, kulipaswa kuwa na vibao to guide people. Ndiyo maana watu hupotelewa na mali na wenzi wao only kwa kutojua where to stand nor where to ask.
Kuhusu vyoo ndiyo kabisa, vilipaswa kuwa strategically located, so that abiria anaposhikwa na mawili ana kuwa na the nearest point kujisevu kabla moja halijamponyoka. Pole anyway na tuendelee kuliombea Taifa
 
Ndio maana mimi hata siku moja sipandii basi Ubungo. Panda mwendokasi ukalikute mbele (Kimara au Mbezi).
 
tandale kwa mfuga mbwa sijui ni wapi stendi yake ipo wapi?
 
Ile ni aibu. Ni katika vitu vinavyotutia aibu kama taifa. Hata airport yetu ya dar pia ni aibu tu. Ngoja tujaribu viwanda huenda huko "tutaweza".🙁🙁

Tumerogwa!
 
Ipo haja ya kuugeuza uwanjwa wa mpira wa miguu kuwa stendi kuu ya mabasi ya mikoani... Itakuwa ni manufaa makubwa kuliko ulivyo kaa kaa kihasara sasa hivi.
Hauna tofauti na uwanja wa mnada wa ng'ombe, kuna haja gani ya kuchukua ushuru sehemu isipo na maboreshi hata wageni utushangaa sehemu ambayo inabeba Magari yenye thamani zaidi ya bilioni 200 kwa siku. Inakosa stand ya kisasa ambayo hata gharama yake haifiki bilioni 100.Tupambane na maendeleo tuache kupambana na watu.
 
Next time, mpandishe bibi kwenye bombardier mpaka Mbeya then aendelee kwa bus!

[emoji39] [emoji39] [emoji39]
Yaani mtu anaenda Kondoa apande Ndege ya Mbeya? Utakuwa hujui Jogorafia wewe!
 
Hii ndio sababu nalazimika kupanda ''DARLUX'' pekee kwani sina jinsi ... Kituo cha mabasi ya kwenda mikoani - Ubungo kwangu ni kama uwanja wa vita.

Sina hamu napo hata kidogo, ni kama hapana uongozi
 
Ifike pahala tuwe sehemu ya suluhusho na sio kulalama tu. Ushauri wako ni upi kwa mamlaka husika?
 
Ubungo unaweza kuachwa na Gari na wakati umewahi

Halafu bila ya aibu wanatoza ushuru ni Heri wangeacha tu.
 
Hivi Kwa nini kusiwe na terminal tatu za wilayani Temeke, Ilala na Kinondoni? Ubungo imekuwa ganzi kwenye akili za wahusika miaka nenda-rudi na watu hawana ubunifu, wanatesa abiria bure tu!

Nani kasema lazima wasafiri wa wilaya zote wakitaka kwenda bara lazima wapitie Ubungo? Au nani kasema mabasi toka nje ya Dar yasiende moja kwa moja Temeke, Mwenge au Kigamboni?

Nini maana ya "satellite cities" kama mmeng'ang'ania gari zote kwenda bara zianzie Ubungo na zitokazo baravziishie Ubungo tu?

Msongamano mnausababisha wenyewe kwa kukosa ubunifu miongini mwa vitu kama SUMATRA, TANROADS, CITY PLANNING, na Watawala kwa ujumla.Flyovers pekee sio solution ya mipango miji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…