Narudia maoni yangu kwa Jiji kuhusu UBT ingawa nakiri kwamba mimi sio mtaalamu wa mipangomiji.
1. Jengeni terminal Kinondoni, Temeke, Ilala, Kigamboni na Ubungo yenyewe; ili mtu akitoka bara akate ticket ya kule aendako, sio aishie Mbezi halafu atafute usafiri wa kumfikisha Temeke, Kigamboni nk.
2. Lengo ni kupunguza msongamano kwenye terminal na miundombinu Jijini. Mtu anaetoka Mwanza na safari yake inaishia Kigamboni, kwanini alazimike kushuka Mbezi au Ubungo? Hamuoni kwamba ni usumbufu? Vilevile mtu yuko Kigamboni au Mbagala anaetaka kwenda Mbeya, kwanini asipate usafiri hukohuko wilayani na kupitia njia za mkato (ring roads) kuunganisha Mbezi au Kilwa road bila kuingia CBD?
Si hivyo tu, kuna wasafiri wa kupita (transit passengers) kwa mfano toka Kigoma kwenda Zanzibar, huyu naye munataka ateremkie Mbezi, halafu apande commuter bus au taxi hadi bandarini! Usumbufu wote wa nini?
3. Anzeni kuplani transit connectionability kikanda na kimataifa. Ili huko mbele MTU aunganishe toka Lusaka hadi Zanzibar au Temeke au Tangibovu. Haina tija kusafiri toka Mwanza hadi Dar kwa treni ya mwendo kasi halafu utumie masaa kibao kufika Tangibovu.
4. Anzeni kubuni multilevel, multipurpose terminal structures kwa maeneo husika, kwa kuzingatia mahitaji ya sasa na miaka 50-100 ijayo. Sio kwa staili ya zimamoto kama ilivyo sasa.
5. Lazima kuwepo coordination kati ya stake holders ili kuepusha viroja kama vya DRT-UDA pale Ubungo na Msimbazi.
6. Pamoja na hayo sidharau kazi mliyonayo, ni kazi ngumu inayohitaji ueledi, elimu na upeo mkubwa. Naamini mnajituma sana.