Nimepata msiba wa mwanangu wa pili, ana miaka 2

Nimepata msiba wa mwanangu wa pili, ana miaka 2

Magical power pole sana kama hizi habari ni za kweli ila kama ni za kuzusha JF inaweza kugeuka shubiri kwako
Binafsi nimepata ukakasi na hii taarifa. Msiba umetokea saa tisa usiku na saa kumi usiku ukaingia JF kupost!
Naamini kwanza umepata taharuki kubwa na kuna mengi ya kufanya kabla ya kutangazia watu msiba utakuwa wapi
Je marehemu aliugua? Kwa muda gani?
Je kafia hospital au nyumbani?
By the way tupe taarifa sahihi tutakushika mkono katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mwanao ikithibitika ni kweli
Nimewaza pia
 
Poleni Sana na MWENYEZI MUNGU AWATIE NGUVU KATIKA KIPINDI IKI KIGUMU
 
Pole sana ni kazi ya Mungu
Kwa hiyo Mungu kamuua mtoto wa ndugu yetu Magical power ?

Kwa nini mnapenda kumfanya Mungu aonekane mkatili sana wakuu?

Kweli Mungu awanyang'anye Magical power na mke wake mtoto wa miaka 2 waliyempenda?

Kwa hiyo wazazi wanavyolia kwa uchungu Mungu anafurahi au naye anahuzunika?

Kama Mungu ndiye kamchukua mtoto kwa nini tena tunamuomba muuaji huyohuyo awafariji na kuwatia nguvu wafiwa?

Does it make sense?
 
Back
Top Bottom