Nimepata msiba wa mwanangu wa pili, ana miaka 2

Nimepata msiba wa mwanangu wa pili, ana miaka 2

Magical power pole sana kama hizi habari ni za kweli ila kama ni za kuzusha JF inaweza kugeuka shubiri kwako
Binafsi nimepata ukakasi na hii taarifa. Msiba umetokea saa tisa usiku na saa kumi usiku ukaingia JF kupost!
Naamini kwanza umepata taharuki kubwa na kuna mengi ya kufanya kabla ya kutangazia watu msiba utakuwa wapi
Je marehemu aliugua? Kwa muda gani?
Je kafia hospital au nyumbani?
By the way tupe taarifa sahihi tutakushika mkono katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mwanao ikithibitika ni kweli
Jamaa post zake nyingi kama unamfuatilia nyingi ni za kutunga,sio mkweli,ana post nyingi humu za kutunga. Ata hii naamini sio kweli.
 
Kila mmoja ana namna yake ya kuomboleza, huyu hii ndiyo namna yake.

Huyu ni ndugu yetu hapa jukwaani, ametupa taarifa na eneo uliko msiba akitegemea faraja kutoka kwetu na sio haya uliyoandika.

Kama huna neno la faraja msibani ni vyema usizungumze kabisa.
Makuzi ya Watu wengi yanawafanya waweze kuandika chochote na popote bila kujali anaathiri kiasi gani Watanzania wengi hawajakulia maisha ya kuambiwa Utotoni hiki usifanye na majibu ya humu ndio kioo cha makuzi yao..
Mtu anatupa taarifa ana msiba wa Mtoto wake anamkebehi asieee watu pana mtoto wa Kike alifiwa na Baba yake aliendesha gari ikiwa na maiti ya Baba yake toka KCMC Hospital mpaka Mbeya huyu Mzala anaona kutoa taarifa ni tatizo mbona tukifiwa tunapiga simu na kutuma meseji...
 
Nadhan age hii ya social media imechangia pakubwa watu kukosa ujasiri.
Zamani ilikuwa unafiwa, halafu unalazimika kuandika barua kadhaa za taarifa ya msiba huo na kuzituma kwa ndugu na jamaa mikoani kwa kutumia vyombbo vya usafiri
Na ilivyo kuwa ni kwamba unampatia mtu yeyote barua, akifika kijiji husika ye anatupa tu barua hapo kijijini, atakayeiokota ndio anamtafuta mlengwa
 
Back
Top Bottom