Unaniletea motivation speakers🤣 hao wanakupigia hesabu ya kilimo unajionabushakuwa tajiri hata hujaingia shamba
Kweli wewe ni form six bado upo na akili za shule siyo za maisha. Ubishi mwingi. Learn to listen.
Hujapata hoja ya msingi kwenye hiyo video au ushauri wa wadau. Unawaza watu wanaogopa uchawi.
Ngoja nikupe mfano wa usiri toka kwenye biblia.
Unakijua kisa cha Yusufu (Joseph) na nduguze?
Joseph alijikuta utumwani sababu ya kutokuwa msiri. Alipata maono au kuoteshwa ndoto ya maisha yake yajayo na Mungu kwamba yeye atakuwa tegemeo la familia yao. Wote watampigia magoti kaka zake na wazazi wake.
Akaanza kuwaambia kwa furaha familia yao kila alipopata maono hayo.
Kilichotokea nduguze wakapata wivu, wakapanga kumuangamiza wakamtumbukiza kisima kikavu cha zamani, kisha mmoja akapata huruma akashauri wamtoe wamuuze utumwani ....
Do you know what is the moral of the story?
I will tell you one of them, and that is
Keep silence kwenye baadhi ya mambo hasa yale ya kukuletea mafanikio. At least for a while. Nazungumzia yale mambo ya kutoboa maisha. Lengo hasa Avoid envy (epuka wivu au husuda) dhidi ya ndugu jamaa na marafiki, Wana JF inclusive.
Kuna wengine wakisikia wanaweza kufanya fitina ukwame, au kukupa ushauri wa kukukatisha tamaa usifanye hivyo au usiende huko Brazil, n.k.
Wengine watalaani mpango wako kwa maneno tu. Wanasema maneno huumba.
Hili somo muinjilisti maarufu Hayati Myles Munroe amefundisha sana. Ni mojawapo ya kanuni za mafanikio.
Nikupe mifano miwili ya hapa Tanzania.
1 . Mzozo wa Marehemu Ruge na Sugu kuhusu mradi wa malaria, Sugu katika stori kaongea na Ruge plan zake Ruge kaichukua kaipeleka Mawingu, Sugu kabaki kulalamika watu wakapiga pesa .
2. Kuna mtu sitamtaja alikuwa na wazo la internet ya Wi fi Zanzibar yote kila sehemu. Akaenda kwa mdau mmoja wenye mamlaka akawasilisha bila kuwasainisha NDA (Mkataba wa usiri) bila kusajiri hati miliki n.k. Watu wakaichukua plan yake wakaipigia pesa anastuka mradi unaanza hayumo. Hata hivyo mradi haujafanikiwa kihivyo sababu nini? That is another story.