Nimepata Tsh. Milioni 1.3, naomba ushauri wa aina ya biashara ninayoweza kufanya

Huo
Fata huu ushauri.
U
We jamaa yaani kama umeniandikia Uzi vile mi mwenyewe Nina kiasi icho icho 1.3M imetulia ghetto sijui nifanyie nini? Kuna mawazo yananiambia nifanyie expenses za vitu muhimu aswa mavazi na assets ambazo nitaendelea kuziona,maana kufanyia business nahisi ntapoteza maana Kwa kuanzishia business ni pesa ndogo sana
 
Sio lazima.ila kama huna wazo la utaitumia wapi hyo pesa kuna watu wana mawazo kwahyo kuliko kukaa nayo kubaliana na mawazo ya mwengine wewe ubaki kuwa mwekezaji.Wewe unafikili wana wekeza UTT hawana akili? Ni vile hawajui wawekeze wapi ambapo pesa yao itakuwa salama. Tatizo la watanzania mpaka kukosa makampuni ya kutosha ni watu kutoaminiana. Unakuta watu wana milioni 20 mpaka 50 benki tena wala hazipo fixed account lkn badala watafutane vijana wenye mitaji watengeneze makampuni waanze ata kuomba tenda mbalimbali hawawezi wanasubiri kustaafu kazi ndo waanze biashara.
 
Hata elf 10 inaweza fanya biashara ya aina yake
 
Nimeiweka nbc malengo account
 
Siogopi ajali Tatizo ni kua nina ajira fulani sekta binafsi ko nakuua free kuanzia sa 10 jion na wikiend tu.
Sawa...ila huo mtaji wako kununua pikipiki na kumpa mtu sidhan kama ni wazo sahihi hawa jamaa ni wasumbufu mno
 
Biashara unataka uangalizi na muda
Biashara haijaribiwi
laZima ujitoe Kwa hiyo biashara

Nadhani jitafute zaidi Kwa mbinu ulizitumia kupata hiyo fikisha million3 nitakushauri cha kufanya

Au acha kazi komaa na biashara nitakushauri hapa Kwa mtaji wa laki 7 laZima Kwa siku ukunje elfu 30, hiyo ni lazima
 
Hiyo ni pesa kubwa mkuu

Watu wanafanya biashara ya laki 3 na wanaendesha familia
 
Naomba uniashauri wa lako 7 nione kama itanifeva mkuu samahani Nielekeze
 
Kuwekeza na mtanzania ni suicide dive,kama watu wanaiba Hadi Kodi waliyotoa maskini unafikiri kuna zaidi wanaogopa,Hadi kura zinaibwa.Tz kila mtu ana vina saba vya wizi.
Mimi ni shahidi wa matukio ya partners kupigana na vitu vizito,mtu anaiba anakuacha kama mkiwa,nadhani taifa hili Lina vita ya mtu kwa mtu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…