Nimependwa na bibi wa kizungu anataka tuoane

Joined
Mar 22, 2022
Posts
15
Reaction score
13
Habari wakuu.

Nisiwachoshe na maneno mengi. Nimebahatika kuwa kwenye urafiki na huyu mama/bibi wa kizungu kwa miaka 10 sasa.
Amekua akinisaidia hapa na pale.

Sasa anataka tuwe wapenzi na mimi niende kwake. Anaishi na mabinti zake wawili. Mabinti wamekubali uhusiano na kuubariki.

Pia anataka anisajili kama mrithi wa nyumba yake, kingine anataka nikienda nipate kazi, hataki nikae bure na kipato changu nikitumie kumsaidia mtoto wangu na ndugu zangu. Nchi ni Finland.

Wakuu nishaurini nikubali au la? Maana hapa mjini sina ishu ya kueleweka.
 
Finland sehemu gani? Msingi kiuno Mzee, huku divorce ni kitu cha miezi sita tu uko free mtaani. Kama una ndoto ya kuja Ulaya nakushauri umchukue tu ila ufunge ndoa bomani. Chukua mashahidi wawili funga ndoa makaratasi yakamilike uje.

Ujiandae kwa baridi lakini, Finland tuna baridi kali sana. Ukifika ukihitaji ushauri usisite kunitafuta. Naishi mji wa Espoo Karibu na Helsinki.
 
Duuh, kumbee bongo walioko ughaibuni ni wengi eeh!! [emoji848]
 
Ina maana tangu uko na 18 umeanza rondea bibi ya kizungu?

Watu8 inawezekana.
Jirani yetu kulikuwa na mtoto wa darasa la saba.
Kibibi cha kizungu kikampenda kufa anatoka Ulaya anakuja kumtembelea kwao, anamsomesha mpaka sasa na amempeleka kwao Ujerumani, mie nilikuwa naona ni uhusiano wa mtu na mjukuu wake, wengine wanasema wa kimapenzi(kuna raia mpaka zilikuwa zinatamani ile nafasi na kumuonea wivu dogo)
Kijana anasoma chuo Ujerumani sasa sijajua aina ya mahusiano wanayoendelea nayo sasa.
 
Okay, dunia ina mambo...

Najaribu tafakari, mtu anawezaje kuwa na urafiki na bibi mtu mzima ambaye ni rika la bibi yake...!
 
Back
Top Bottom