Nimepigwa Tsh milioni 8 kwenye biashara ya uwakala kupitia mfanyakazi mzembe

Uyo binti inawezkana hao watu ni watu waliokuja kimazoea na kumuachia vitipu vya hapa na pale sasa akawa kawazoea ndo maana hata simu akawaachia mpaka kutokea utapeli huo ila pole sana mkuu uyu binti kama inakupendeza msamehe tu muachie Mungu atakulipa zaidi
 
Dah! Pole sana.
Hapo cha kufanya binti alipie gharama za uzembe wake, mpeleke polisi.
Kivipi madame? Unajua hata bosi anaweza kutumia mbinu hiyohiyo kumtapeli mfanyakazi wake ili azuie mishahara yake au apate fedha kwa njia isiyo halali?

Swali la muhimu inatakiwa tumsikilize binti maana huenda hajawahi kumpa mtu simu ya kazi
 
Nkamu
Hucheki na wowote
Kwenye pesa hapana tucheke na mengine..!!
Hapo apelekwe polisi wazazi wake km wana pesa wamtolee kufidia hasara..!!

Mtu kakatazwa usitoe simu yeye katoa, hapo nitaamini vipi km hawako wote wameshirikiana?

Hata akisema amkate mshahara hatofanya kazi kwa ufanisi, atafanya bora liende mwisho ataiba tena kwa kujua atakatwa kwa kufanyishwa kazi..!!
 
Umesema walikuja wiki moja kabla, ina maana hiyo wiki moja kabla mpaka jana wewe hukuwa umewasiliana na mfanyakazi wako? Hii mbona kama chai
 
Kivipi madame? Unajua hata bosi anaweza kutumia mbinu hiyohiyo kumtapeli mfanyakazi wake ili azuie mishahara yake au apate fedha kwa njia isiyo halali?

Swali la muhimu inatakiwa tumsikilize binti maana huenda hajawahi kumpa mtu simu ya kazi
Kwa kesi ya huyu hawezi kupoteza muda kuja kuongea uongo JF.

Hivi wewe ushawahi kupoteza pesa au unaona mwenzio analeta utani??
 
UKuingia kwenye anga ya utapeli hata uwe naakili timamu lazima ulie
Kanuni ya kwanza katika pesa
Mpigie kwanza tajiri kujiridhisha kwamba ni kweli anataka pesa yeye mwenyewe

Yaani mtu anakutumia meseji tu,meseji pekeyake
Na unakubali kumtumia kwa namba ngeni,pasi na kujiridhisha kwa simu..huu ni uzembe na ujinga wa wakala.
Pesa siyo rahisi kihivyo aisee.
 
Asante mkuu
Ni kweli au kama ya JF siku hizi unataka tu ku-draw attention? Huu mchezo ni wa siku nyingi na karibu watu wote walioko kwenye hii business wameshawafundisha wafanyakazi wao wasikubali kufanya ujinga kama huu. Hukumpa maelekezo? Kama ulimpa basi yeye anashirikiana na hawa wezi na anajua akikumbia hivi utamfokea siku mbili tatu na kumfukuza ila atakuwa amefaidi. Lakini bado siamini kama ni kweli kwa sababu hata ulivyo na muda wa kujibu kila comment inaonyesha kabisa unatafuta attention. Halafu ID yako, imeanzisha thread kadhaa zenye mada za kutafuta attention kama hii.
 
Inamaana huwa unatumiaga simu ya kazi kuwasiliana na Binti wa kazi??

Means huwa unampigiaga kupitia simu ya wakala au anatoa line?

Hapo itakuwa hawkuomba simu ya kazi,labda walimuomba simu yake mwenyewe binafsi,.pole..hiyo hela hesabu imeenda tu,huwezi kupata tena.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…