Nimepoteza marafiki kisa mke wangu!

Nimepoteza marafiki kisa mke wangu!

Na nitoe ushauri kwa wanawake,,ukiwa penda ndugu wa mume hata ikitokea tatizo kati yenu tambua utapata sapoti kubwa toka kwa ndugu wa mume,,yaani watasimama na wewe mwanzo mwisho,,bahati mbaya wengi wenu hamlijui hili
 
Matumaini yangu mlio wengi humu ndani mlikua na weekend njema.

Ni miaka sita sasa tangu nimeoa na nimebarikiwa kua na watoto wawili. Kabla sijaoa nilikua nna marafiki wengi na bahati nzuri rafiki hao angalau wanajiweza wao wenyewe na familia zao. Namshukuru sana Mungu kwa ajili yao kwa sababu kwa namna moja au nyingine ndio walionifanya nibadili maisha ya kisela ya kibachela na kuamua nami niwaige kua na familia. Niliona kabisa nahitaji kufanya hivyo ili niendane nao.

Huyu mke wangu anawafahamu vizuri rafiki zangu hata kabla sijamuoa, ingawa kuna tabia alikua anaionesha ya kuchukia/kukasirika hasa nnapomwambia nipo na marafiki zangu au la pale anaponiona na marafiki zangu. Wakija kunitembelea nyumbani alikua anawapokea vizuri na anawachangamkia.

Lakini mambo yalibadilika ghafla baada ya kufunga nae pingu za maisha.

Anaonesha dhahiri kwamba hawataki rafiki zangu. Hataki waje nyumbani wala hataki mimi niende kuonana nao. Anataka nikitoka kazini moja kwa moja nyumbani, weekends anataka tushinde nyumbani tu. Akisikia hodi ya rafiki yangu yoyote atanuna siku nzima. Anasema wananiharibu, amesahau hao hao ndio walionifanya nimenunua kiwanja na kujenga nyumba, nilinunua gari kwa msaada wa rafiki zangu haohao. Vingi nilivyonavyo nimevipata kwa kua inspired nao.

Hata kumchagua yeye nimuoe, ingawa hajui lakini rafiki hao ndio walinishauri kwamba anafaa zaidi yeye kuliko wengine nilio kua nao. Hataki ndugu, hataki mtu yoyote mgeni zaidi ya rafiki zake au ndugu zake tu.

Kwa sasa rafiki zangu hao pamoja na kumtetea sana mke wangu, wameshagundua kwamba wanajibembeleza sana kuja kwangu. Wote wamekata mguu, imebaki mimi kuwatafuta lakini kila mmoja sasa hivi anaonekana anahamsini zake.

Furaha ya mke wangu ni kuniona mimi tu pembeni yake muda wote. Sina mawazo mapya sababu sijumuiki na wenzangu. Nimekua kama msukule sipati marafiki wapya na niliokua nao hawapo tena.

Hivi majuzi nimepata kibarua mkoani, nimepata angalu muda wa kuwapigia, lakini muamko wao si kama wa zamani.

Naombeni ushauri wenu, nyumba yangu kubwa lakini haivutii kabisa wala siipendi kwa sababu inasisi watu wazima wawili na watoto wawili ambao nao wanashinda shule. Muda mwingi ipo kimya kama wanga vile 😭😭
Ili mwanamke akutawale lazima akutenge na rafiki/jamaa zako. Kwa hilo keshafanikiwa. Sasa ni mwendo wa wewe kutii shuruti bila sheria😂😂😂
 
Asanteni wote kwa mawazo yenu, nafuatilia comments zote ili nitoke na maazi sahihi. Siwezi kumjibu kila mmoja lakini ntakachokifanya hapa ni "Wengi wape". Kwa sababu niliyona moyoni ni mengi kuliko niliyoyaandika.
 
Shida ni kuwa mkewe hajavunja cycle za upande wake (marafiki zake na ndugu zake) mke wa namna hiyo ni mbinafsi hafai.
Kama ni cycle alipaswa avunje zote za mumewe na zake pia wabaki wawili tu na watoto wao.
Sahihi
 
Ukishaoa/Olewa kuna vitu automatic inability uachane navyo kabisa au upunguze mojawapo ni hilo last marafiki especially wa jinsia tofauti au hata wa jinsia yako tu

So ni kuchagua mke au marafiki!
The choice is yours

Cc Smart911
 
Ooh kumbe watu wakioana inabidi waje ndugu wa mwanamke tu ila ndu wa mwanaume wakija mke achukie. Safi sana
 
Amekuokoa, mkeo ana akili kashaona hamna kitu mule, yale ni magalasa.
Fukuzwa kazi leo ama pata tatizo kubwa afu uone kama kati ya hao ukipiga simu atapokea.
 
Huyo jamaa sio wewe Mkuu ? 🤣😀🤣 au wewe ni Kataa ndoa
Screenshot_20240423_124048.jpg

Sio mimi mkuu, sijaoa na sina mpango huo kwa sasa japo ntaoa.
 
mwanamke ukishaolewa kuna mambo unatakiwa usiingilie kabisa marafiki wa mume na ndugi zake hao umemkuta nao hujui wanaishije huwez jua wanasaidiana vipi pengine n msaada mkubwa kwa mumeo wewe deal na nyumba yako, ukiona ana complain juu ya rafiki fulani anamfungia vioo hata usidandie treni kwa mbele mshauri tu ndio dunia watu na viatu yeye aaangalie mechi zake kimya ni jibu sio nilikua nakuangalia mtafika wapi na huyo rafiki yako,sjui ndugu zake wamemfanya nn mshauri ki hekima lakini usisahau shika jembe ukalime hao ni ndugu zake umemkuta nao wewe zingatia anatoa excuse kabla kama atachelewa kurudi anakutreat kama malkia wake sio kumwambia marafiki zake ni wanawe na wewe hapo kabla anaanza urafiki wao had ukanoga na kufika happ ulipo ulikuwepo?
Ushauri mzuri sana huu
 
Matumaini yangu mlio wengi humu ndani mlikua na weekend njema.

Ni miaka sita sasa tangu nimeoa na nimebarikiwa kua na watoto wawili. Kabla sijaoa nilikua nna marafiki wengi na bahati nzuri rafiki hao angalau wanajiweza wao wenyewe na familia zao. Namshukuru sana Mungu kwa ajili yao kwa sababu kwa namna moja au nyingine ndio walionifanya nibadili maisha ya kisela ya kibachela na kuamua nami niwaige kua na familia. Niliona kabisa nahitaji kufanya hivyo ili niendane nao.

Huyu mke wangu anawafahamu vizuri rafiki zangu hata kabla sijamuoa, ingawa kuna tabia alikua anaionesha ya kuchukia/kukasirika hasa nnapomwambia nipo na marafiki zangu au la pale anaponiona na marafiki zangu. Wakija kunitembelea nyumbani alikua anawapokea vizuri na anawachangamkia.

Lakini mambo yalibadilika ghafla baada ya kufunga nae pingu za maisha.

Anaonesha dhahiri kwamba hawataki rafiki zangu. Hataki waje nyumbani wala hataki mimi niende kuonana nao. Anataka nikitoka kazini moja kwa moja nyumbani, weekends anataka tushinde nyumbani tu. Akisikia hodi ya rafiki yangu yoyote atanuna siku nzima. Anasema wananiharibu, amesahau hao hao ndio walionifanya nimenunua kiwanja na kujenga nyumba, nilinunua gari kwa msaada wa rafiki zangu haohao. Vingi nilivyonavyo nimevipata kwa kua inspired nao.

Hata kumchagua yeye nimuoe, ingawa hajui lakini rafiki hao ndio walinishauri kwamba anafaa zaidi yeye kuliko wengine nilio kua nao. Hataki ndugu, hataki mtu yoyote mgeni zaidi ya rafiki zake au ndugu zake tu.

Kwa sasa rafiki zangu hao pamoja na kumtetea sana mke wangu, wameshagundua kwamba wanajibembeleza sana kuja kwangu. Wote wamekata mguu, imebaki mimi kuwatafuta lakini kila mmoja sasa hivi anaonekana anahamsini zake.

Furaha ya mke wangu ni kuniona mimi tu pembeni yake muda wote. Sina mawazo mapya sababu sijumuiki na wenzangu. Nimekua kama msukule sipati marafiki wapya na niliokua nao hawapo tena.

Hivi majuzi nimepata kibarua mkoani, nimepata angalu muda wa kuwapigia, lakini muamko wao si kama wa zamani.

Naombeni ushauri wenu, nyumba yangu kubwa lakini haivutii kabisa wala siipendi kwa sababu inasisi watu wazima wawili na watoto wawili ambao nao wanashinda shule. Muda mwingi ipo kimya kama wanga vile 😭😭
Pole, ila hapa hakuna mwanaume. Umeolewa tayari.
 
Sio marafiki tu mpaka ndugu hawataki mkuu
Wee nao hapo si ndo pa kutobolea.
We kila kitu mpakazie mkeo kwamba hapendi.
Omba Mungu usipatwe na tatizo na wale washkaji waliokusaidia ukawatosa ukawafata watakubalasa ukafie kwa mkeo.
Mkeo nae atatimka ndio utajua rangi za rainbow zikoje.
Na ujifunze Namna ya kupiga makofi style tofauti itasaidia
 
Wee nao hapo si ndo pa kutobolea.
We kila kitu mpakazie mkeo kwamba hapendi.
Omba Mungu usipatwe na tatizo na wale washkaji waliokusaidia ukawatosa ukawafata watakubalasa ukafie kwa mkeo.
Mkeo nae atatimka ndio utajua rangi za rainbow zikoje
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Back
Top Bottom