Nimepoteza mimba 10 kwa tatizo hili

Nimepoteza mimba 10 kwa tatizo hili

Kafanye kipimo cha Rhesus Factor. Inawezekana damu yako haiendani na hao wa mama.
 
Ni ishu ya kiimani zaidi mkuu
Kama kiimani zaidi namba za daktari nahisi hazitakusaidia. May be upate namba za waganga wa jadi, ila ukifuatilia somo la chumvi la mshana linaweza kukusaidia
 
Wakuu nimekuja kwenu kwa mara nyingine tena naombeni msaada wenu.Mwaka 2022 nilileta uzi kuhusu watoto wangu wanaozaliwa na kufa kabla au baada ya kuzaliwa. Sasa mwaka huu tena 2024 nimepoteza watoto wengine wawili kabla ya kuzaliwa wakiwa tumboni.

Baada ya tukio hilo ikabidi kutafuta wazee kuwaomba ushauri.Kuna sehemu huku mkoani nikapelekwa kwa mama mmoja akaniangalia akasema nina likango kwa jina maarufu.

Hii ni kama bawasiri ila sio bawasiri na kazi yake ni moja tu kumaliza watoto. Huota katikati ya tundu la haja kubwa. Nikaambiwa inatakiwa nipate tiba ili niweze kuitwa baba.

Na katika mimba hizo 10 zimepatikana kwa kipindi cha miaka hii miaka4 kwa wanawake tofautitofauti. Nimekuja kwenu kuomba ushauri kwa mwenye experience na hii kitu aweze kunisaidia jinsi gani nitaiondoa katika mwili wangu.Asanteni 🙏..

Hii picha nilipiga mwaka 2021 ilivyonianza hilo tatizo la likango.
Hakuna kitu kama hichonenda hospitali achana na wachawi
 
kila mtu na fikra zake.
Kila mtu ana fikra zake lakini hilo halina maana kwamba swali hili halina mantiki kwa sababu kila mtu ana fikra zake.

Kila mtu ana fikra zake katika kila kitu, lakini bado kuna fikra fulani ni sahihi na fikra nyingine si sahihi.

Swali halijajibiwa bado, kwani kuwa na mtoto ni lazima?
 
Achana kwanza achana na huo ujingavwa likango, Kuna ishu ya rhesus factor (Rh) inakupasa kuwa na mipango juu ya mwanamke unayemtaka awe mama wa wanao, na hapo ndio linakuja suala la kwenda hospital ukiwa na mwenzi wako nakupima vipimo vya damu na hapo doctor atakuja na vimimo. Hata waambia ukweli kuhusu uwezekano wa nyinyi kuweza kupata mtoto kutokana na vipimo. Anaweza akashauri pindi anaposhika mimba tu haraka achomwe sindano ili kutoadhiri ujauzito.
 
Wewe ni ME au KE alafu unianbie na kabila lako maana ilo likango wanakuwanalo KE kama utakuwepo sehemu ambayo nimewahi kupita nitakupa mtu akusaidie utajieleza unachohitaji atakusiadia
Mimi ME mtu Ruvuma
 
Bawasiri ukipaka shubiri mwitu(aloe Vera)Huwa inaondoka)ukizingatia na ulaji wa mbogamboga nyingi pamoja na maji
Unapaka alove vera kila siku au..Na inaondoka kwa muda gani?
 
Mwanaume unapotezaje mimba au huyo mwanamke ana pid sugu!
Mzee hii ishu ni serious sio masikhara,na sio mimba tu hata watoto wakizaliwa hawafiki mwezi wanakufa kwa wanawake karibia 10 wote
 
Back
Top Bottom