Nimerudi kazini sijamkuta mke wangu, nauliza majirani naambiwa ameondoka kwenda kwao

Nimerudi kazini sijamkuta mke wangu, nauliza majirani naambiwa ameondoka kwenda kwao

Hatukua na ugomvi kwa kuwa tuliishi vizuri tuu ila huko kipindi cha nyuma tuliwahi kukwaruzana kama sehemu ya binadamu. Vipi kuhusu ndugu zake wanaomtafuta niwajibu nini?
Hongera sana.
I wish nipate nafasi kama uliyoipata
 
toa taarifa polisi mkuu, wazazi nao wapewe taarifa......mlijaliwa watoto? mna mda gani kwenye ndoano?....kwa kifupi huyo sio wako tena.........fuata taratibu futa delete....maisha lazima yaende....pole sana...
 
Saloon na magengeni ni sehemu hatari sana kwa wanawake ambao waume zao ni watu wa safari
 
Hatukua na ugomvi kwa kuwa tuliishi vizuri tuu ila huko kipindi cha nyuma tuliwahi kukwaruzana kama sehemu ya binadamu. Vipi kuhusu ndugu zake wanaomtafuta niwajibu nini?
Enda kapige ripoti ya mtu kupotea, kituo cha polisi karibu na wewe. Mashahidi ni majirani zako

Itakuepusha na mengi sana hapo mbeleni
 
Kama dalili zipi?na jee hata wakwe nisiwadokeze ujio wangu?
Usiwaambie. Na ukiweza piga kamba mitaa ya karibu na ukweni kwa siku utazokuwa huko. Utajionea dalili za kama kweli Mtoto wao hayupo Chamwino ama laaah wanakuektia!
 
Pole sana Mkuu. Umeandika kwa huzuni sana na inaonekana unampenda sana mkeo.
Toa taarifa polisi ili ujihakikishie usalama, maana dunia hii binadamu wameisha.
Angalizo: Ikitokea umempata mkeo na mkaamua kuyamaliza, hakikisha unakoishi na mkeo anakuwepo. Achana na habari kwamba unaenda mkoa mwingine kikazi na yeye unamuacha mkoa mwingine. Ambatana nae mahala pote, utachokula ndicho atachokula.
 
Nafanya kazi mbali na ninapoishi kwa hiyo huwa ninalala huko ninakofanyia kazi ambako nimepanga chumba cha dharura.

Siku ya jtano wiki hii niliagana na mke wangu kuwa naelekea kazini na nitarudi siku ya alhamisi au ijumaa akaitikia na tukaagana vizuri.

Mshtuko wa moyo nilioupata ni pale nilipojisikia kurudi siku ya pili yake yaani Alhamisi baada ya kugonga mlango kwa muda bila majibu nikaamua niulize jirani aliko mke wangu, najibiwa jana ulipoondoka mkeo nae kasafiri ila funguo hizi hapa. Nilihisi kuishiwa nguvu lakini nilijikaza nikachukua ufunguo taratibu nikaingia ndani kiukweli sijaamini macho yangu hakukua na kitu chake hata kimoja zaidi ya kuniachia picha za ndoa.

Nimeumia sana na huo ulikuwa mwisho wa kupata usingizi hadi sasa. Nimempigia simu lakini haipatkani, ndugu zake hawajui yuko wapi ila leo hii Jumamosi mpangaji mmoja kanionea huruma kaniambia aliongea na mke wangu siku ya Alhamisi jioni na alimfahamisha kuwa anakaribia kufika kwao Chamwino Dodoma akitokea kwetu Mtwara.

Lakini kwao nikiuliza naambiwa haonekani na simu hapatikani, sijui cha kufanya kwanini mke wangu wa ndoa lakini amenitoroka. Naombeni mnishauri nini nifanye kwa kuwa suala hili limevuruga kichwa changu.

Mara ya mwisho kuwasiliana nae ilikuwa jioni Alhamisi kwa kum SMS kupitia private Facebook nikamuuliza uko wapi? Akanijibu kwa kifupi "my lovely husband ".Mpaka sasa simpati kwa simu.
Mkuu nipo Dodoma naomba nipe account yake ya facebook na namba yake ya Simu nikusaidie kumtafuta huwezi kupatwa na msongo wa Mawazo wakati mimi nipo Dodoma.
 
Ushauri na majibu ya watu wengi kwenye uzi huu inaonesha ni jinsi gani watu wengi hawana utu na huruma pia inaonesha watu wengi ni wa mashala hata kwenye issue za msingi.
Sio vzr ndugu zangu, mna muumiza jamaa kwa majibu yenu ya kejeri hayo
unapoleta uzi kama huu hapa uwe umejiandaa kisaikolojia .......... kuna watu wa kila aina jf anzia waokota chupa za plastick hadi majenerali
 
Si bure wewe ndiye sababu ya yeye kutoroka huyo mwanamke kwenda kwao bila kukuaga.

- Ulikuwa unampatia hela ya chakula cha kutosha na mavazi?

- Ulikuwa unapata muda mrefu wa kukaa naye na kupanga kuhusu maisha yenu?

- Ulikuwa unamridhisha katika tendo la ndoa?

Yaani kifupi JE ULIKUWA UNAMJALI?

Isije ikawa wewe ndio mwenye makosa ila unawahi kuja kushitaki na kuomba ushauri huku.
 
Back
Top Bottom