Unaposoma kitabu tunategemea unapata maarifa na baadaye kutumia maarifa hayo ili kukurahisishia maisha yako. Hatutegemei ufuate yale tu uliyoyoyasoma bila kuwa na ongezeko lolote ulilolipata (maarifa) kutokana na kusoma kitabu hicho. Vinginevyo utakuwa hujaelewa ulichokisoma; utakuwa umekariri.
Tumwomba au kusali kwa kulitaja jina la Yesu Kristo, lakini pia tunaongezea maombi hayo kwa kumuomba Bikira Maria atuombee kwa mwanae. Ni sawa tu wewe unaweza kumuomba kitu baba yako, halafu ukamuomba mama yako amsihi baba yako akupe hicho unachohitaji!
Tusikariri mambo, tulipewa akili ili kuweza kujiongeza. Sio kwakuwa Biblia ilisema hivi, basi tuishie pale pale tu, hapana, tunyambulishe mambo!