Nimeshangaa kumuona Profesa mmoja maarufu wa pale UDSM akisali sala ya Bikira Maria

Nimeshangaa kumuona Profesa mmoja maarufu wa pale UDSM akisali sala ya Bikira Maria

Moja kati ya mambo ambayo yapo wazi kabisa katika biblia ni maelekezo ya namna maombi yanatakiwa kufanywa. Agizo la maombi lipo very open.

Yesu Kristo alisema mara nyingi sana kwenye injili ya Yohana kwamba tuombe kwa jina lake. Mtume Paulo ameandika tufanye yote katika jina la Yesu Kristo.

Sasa profesa ambaye ameandika paper kibao na amefanya literature review za kutosha ameshindwa kusoma biblia kufahamu tunapaswa kuomba kwa jina gani?

Hakuna sehemu hata moja mitume waliomba kwa jina la Maria. Yule Maria mama wa Yesu alikaa pamoja na mitume na walijazwa Roho Mtakatifu pamoja na wakanena kwa lugha.

Maria alimzaa Yesu lakini hakumzaa Mungu. Kuna tofauti kati ya Yesu na Kristo. Maria sio mama wa Mungu bali ni mama yake Yesu. Yesu ni mwanadamu na Kristo ni Mwana wa Mungu.

Hivyo Yesu Kristo ni Mungu na mwanadamu kwa wakati mmoja. Asomaye na afahamu.
Hata wewe mwenyewe nawe washangaza sana. Inawezekana vipi Yesu kristo awe Mungu halafu mwanadamu kwa wakati mmoja.
 
Unajua ni suala la ufahamu tu. Ungekuwa na ufahamu wa kutosha kuhusu concept ya 'imani', wala usingetumia nguvu kumshangaa huyo hadi kuja kuanzishia uzi eti 'Unamshangaa Profesa'. Imani ni kusadiki, yeye anasadiki hayo anayotamka na wewe unasadiki mengine ambayo ni tofauti (labda kuombewa na mchungaji). Kwa kuwa nchi yetu imeweka wazi suala la uhuru wa kuamini, hauna haja ya kushangaa kiasi hiki (labda kama kuna tatizo fulani upande wako binafsi)
Mkuu shida ni elimu elimu elimu! Ukute tunabishana na jitu la darasa la 7 B! Linajidai kuchakata hoja zinazolizidi Kimo!
 
Imani waachie wenye nayo wajua Pana watu wanaomba Mbuzi/Mawe na wanafanikiwa?!!!

Shikilia ulichonacho au unachoamini, na kama waona wengine wanakosea, ni jukumu lako kuwaombea warudi au waende kwenye njia sahihi!!

Heri ya Mwaka Mpya!!!!
 
Kwanza huwa nakushangaeni sana watu wa dizaini yako, huwa mnawashwa wapi kufatilia imani za watu?
Kwani lazima uamini anachoamini mtu mwingine?
Tuache tuendeelee kumheshimu Mama wa Mungu,na kwa taarifa yako tu, TZ iliwekwa chini ya ulinzi wa Mama Bikira Maria.
Kwani Maria ni Bikira?
 
Endelea kutabiri mechi za EPL maana kombe la dunia limeisha...hizi imani tuachie wenyewe kwa sbb hatuji mlangoni kwako kuombea hapo..
 
Moja kati ya mambo ambayo yapo wazi kabisa katika biblia ni maelekezo ya namna maombi yanatakiwa kufanywa. Agizo la maombi lipo very open.

Yesu Kristo alisema mara nyingi sana kwenye injili ya Yohana kwamba tuombe kwa jina lake. Mtume Paulo ameandika tufanye yote katika jina la Yesu Kristo.

Sasa profesa ambaye ameandika paper kibao na amefanya literature review za kutosha ameshindwa kusoma biblia kufahamu tunapaswa kuomba kwa jina gani?

Hakuna sehemu hata moja mitume waliomba kwa jina la Maria. Yule Maria mama wa Yesu alikaa pamoja na mitume na walijazwa Roho Mtakatifu pamoja na wakanena kwa lugha.

Maria alimzaa Yesu lakini hakumzaa Mungu. Kuna tofauti kati ya Yesu na Kristo. Maria sio mama wa Mungu bali ni mama yake Yesu. Yesu ni mwanadamu na Kristo ni Mwana wa Mungu.

Hivyo Yesu Kristo ni Mungu na mwanadamu kwa wakati mmoja. Asomaye na afahamu.

Niaze kwa kuomba radhi kwa waumini wa RC.Hapa ndipo huwaga nadhani waliotengeneza dhehebu la RC Kuna codes hazikusomana vizuri.
Mama Maria aliyemzaa Yesu alibaki kuwa mke wa Yusuf afterward na alifariki kama mwanadamu wa kawaida.So hapa ni kupoteza muda kumwambia marehemu akuombee.Ni kweli hatujui kuomba itupasavyo lakini,kazI ya kutuombea ni ya ROHO MTAKATIFU (Rumi 8:26).Mahusiano ya Mama maria na Yesu kristo ni mahusiano ya Mtu na Mungu wake.Unaweza usitake kuamini,ila ukweli ni kwamba Yesu kristo alishakuwako kabla sana hata ya kuzaliwa kwa Bikira Maria(Ndiyo maana ya utatu mtakatifu). Alichokizaa Maria ni mwili tu wa kibinadamu wa Yesu.

Hapa usipokuwa makini tunaweza tukamfanya mama Maria ni nafsi ya nne. Yaani kuna Mungu baba, Mungu Mwana,Mungu Roho Mtakatifu na Bikira Maria.
Luka 8.21(Mama yangu na ndugu zangu ni hao wanao lisikiliza neno la Bwana).

Sahamani lakini.kama kuna neno katika biblia linalothibitisha hili mnaweza kutusaidia.Ila kama ni logic tu za kibinadamu kwamba kwa kupitia kwa mama,mwana anaweza kukusikiliza maombi yako kirahisi ni upotoshaji.Ni bora ukaenda kwa mtumishi wa Mungu ukamuomba akuombee.
 
hebukueni namsimamo mmoja.yesu nimungu siomungu?😎😎😎
 
Shida huanzia pale watu wanapochanga maneno mawili ya "KUSUJUDU"na "KUABUDU".
 
Inabidi waikristo mchapwe VIBOKO
ndio mana siku zote manabii wanawafanya kama mosukule yao
Ona hapo alivyofundishwa yaan hapo JUU alichoandika hata yeye mwenyewe SIDHANI kama anaelewa alichoandika
hawa jielewi😎
 
Endelea kutabiri mechi za EPL maana kombe la dunia limeisha...hizi imani tuachie wenyewe kwa sbb hatuji mlangoni kwako kuombea hapo..
Madam pole naona nimekugusa pabaya. Mimi mtu akisema hiyo ni imani yake huwa namuheshimu sana maana imani ni suala binafsi na la kikatiba.

Uko tayari nikupe challenge? Mosi, mimi suala la kuomba maria awaombee watu silichukulii kama suala la imani bali ni jambo la ufahamu. Ni simple, je hilo ni agizo la biblia? Kama sio agizo wala fundisho la kibiblia basi mimi naliweka kando.

Lakini pili, kuna jambo la hatari sana mnalifanya pale mnapoomba Maria awaombee kwasababu mnamfanya yeye kuwa omnipresent. Kwamba yupo kila mahali dunia nzima akisikiliza maombi yenu na kuyapeleka kwa Yesu. Hii ni sifa ya Mungu peke yake. No wonder mnapenda kumuita mama wa Mungu wakati mnajua fika maria hakumzaa Mungu bali alitumika tu kutengeneza mwili.
 
Ngoja niweke kapicha cha kusindikizia uzi , watu wanaacha kuabudu Mungu wa kweli Kazi kuabudu viumbe wenzao #InadikitishaSanaView attachment 2465677

Nb: Huyo picha siyo mtajwa katika uzi bali ni mfano tu jinsi gani watu wanavyoabudu kivyao kama content ya uzi unavyosema.
Hii nayo kali,kwamba Mungu naye ana mama kama sisi wanadamu?
Tunakosea sana kumuomba Maria.
 
Nani amefundisha kuomba kwa Bikira Maria? Tunaomba atuombee kama ninavyoweza kuomba wewe uniombee. Nikiomba wewe uniombee maana yake umechukua nafasi ya Yesu?

Utasema Bikira Maria amekufa hajui lolote, hapo maana yake tuhame mada ili ujue watakatifu hawafi, tena wako karibu na Mungu kuliko hata sisi tulio duniani.

Sisi Kanisa la duniani na Kanisa la washindi mbinguni ni Kanisa moja, tutashirikiana daima. Hapo umeona akisali na pia kuomba msaada wa maombezi kwa mama yetu lakini mimi majuzi nilikuwa kwenye maombi na intercessor niliyesali nae ni Mt. Rita.

Kama una swali uliza, sio ubishi bali majadiliano.

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
Kuna jambo la hatari sana mnalifanya pale mnapoomba Maria awaombee kwasababu mnamfanya yeye kuwa omnipresent. Kwamba yupo kila mahali dunia nzima akisikiliza maombi yenu na kuyapeleka kwa Yesu. Hii ni sifa ya Mungu peke yake. No wonder mnapenda kumuita mama wa Mungu wakati mnajua fika maria hakumzaa Mungu bali alitumika tu kutengeneza mwili.
 
Madam pole naona nimekugusa pabaya. Mimi mtu akisema hiyo ni imani yake huwa namuheshimu sana maana imani ni suala binafsi na la kikatiba.

Uko tayari nikupe challenge? Mosi, mimi suala la kuomba maria awaombee watu silichukulii kama suala la imani bali ni jambo la ufahamu. Ni simple, je hilo ni agizo la biblia? Kama sio agizo wala fundisho la kibiblia basi mimi naliweka kando.

Lakini pili, kuna jambo la hatari sana mnalifanya pale mnapoomba Maria awaombee kwasababu mnamfanya yeye kuwa omnipresent. Kwamba yupo kila mahali dunia nzima akisikiliza maombi yenu na kuyapeleka kwa Yesu. Hii ni sifa ya Mungu peke yake. No wonder mnapenda kumuita mama wa Mungu wakati mnajua fika maria hakumzaa Mungu bali alitumika tu kutengeneza mwili.
Mimi sipendi kubishana kuhusu imani ndugu yangu...ndo maana nasema utuache tuu...umeshasema alitumika kuutengeneza mwili kama bado hauoni umuhimu wake tuache sisi tunaoona umuhimu wake tumwombe atusaidie kutufikishia maombi yetu...

Am out..
 
Moja kati ya mambo ambayo yapo wazi kabisa katika biblia ni maelekezo ya namna maombi yanatakiwa kufanywa. Agizo la maombi lipo very open.

Yesu Kristo alisema mara nyingi sana kwenye injili ya Yohana kwamba tuombe kwa jina lake. Mtume Paulo ameandika tufanye yote katika jina la Yesu Kristo.

Sasa profesa ambaye ameandika paper kibao na amefanya literature review za kutosha ameshindwa kusoma biblia kufahamu tunapaswa kuomba kwa jina gani?

Hakuna sehemu hata moja mitume waliomba kwa jina la Maria. Yule Maria mama wa Yesu alikaa pamoja na mitume na walijazwa Roho Mtakatifu pamoja na wakanena kwa lugha.

Maria alimzaa Yesu lakini hakumzaa Mungu. Kuna tofauti kati ya Yesu na Kristo. Maria sio mama wa Mungu bali ni mama yake Yesu. Yesu ni mwanadamu na Kristo ni Mwana wa Mungu.

Hivyo Yesu Kristo ni Mungu na mwanadamu kwa wakati mmoja. Asomaye na afahamu.
Kuna mapadre wamesoma kuzidi hata profesor...

Sent from my Infinix X655 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom