Nimeshangaa kumuona Profesa mmoja maarufu wa pale UDSM akisali sala ya Bikira Maria

Mimi nimeshangaa na hapo sijavunja sheria wala kumlazimisha yeyote aamini ninachoamini.

Vingine ni vichekesho vya kawaida kama hicho cha nchi kuwekwa chini ya ulinzi wa Maria.
Ndo ulete huku?? Emu acha hizo wewe
 
Nani amefundisha kuomba kwa Bikira Maria? Tunaomba atuombee kama ninavyoweza kuomba wewe uniombee. Nikiomba wewe uniombee maana yake umechukua nafasi ya Yesu?

Utasema Bikira Maria amekufa hajui lolote, hapo maana yake tuhame mada ili ujue watakatifu hawafi, tena wako karibu na Mungu kuliko hata sisi tulio duniani.

Sisi Kanisa la duniani na Kanisa la washindi mbinguni ni Kanisa moja, tutashirikiana daima. Hapo umeona akisali na pia kuomba msaada wa maombezi kwa mama yetu lakini mimi majuzi nilikuwa kwenye maombi na intercessor niliyesali nae ni Mt. Rita.

Kama una swali uliza, sio ubishi bali majadiliano.

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
 
Nilitegemea labda utaleta maandiko ya kibiblia lakini naona umeishia kuweka msimamo wa kidini.

Mimi nilichofanya ni kushangaa tu kwasababu nimeona ni jambo la ajabu na halipo kwenye maandiko.

Naheshimu imani yako, fainali siku ya mauti.
Kwa hiyo tuseme wote wanaomheshimu na kumuomba Maria wote wanaenda moyoni hio siku ya kiyama?
 
Nimetunga na ninaimba wimbo wa MAMA MARIA MAMA WA YESU UTUOMBEE.

Huku duniani tupo tu ila hatuyajui mapenzi ya Mingu yako kwenye nini
Leo tunasherekea Bikira Maria mama wa Mungu. Watu wanafikiri tukisema habari za Bikira Maria tunamuinua yeye kumbe Yesu ndiye anayehubiriwa! Mfano kama unaamini Yesu ni Mungu na alivaa mwili kupitia Bikira Maria huoni kuwa huyo mama ni mama wa Mungu? Unafikiri kama si kuwa mama wa Mungu angekuwa kama watakatifu wengine tu.

Kama ni kuokoka tunaweza kusema Bikira Maria ndiye binadamu wa kwanza kumpokea Yesu maana kwa utii wake neno wa Mungu akafanyika ndani yake baada ya kufunikwa na Roho Mtakatifu!

Watu wanapaswa kujua kwanini Wakatoliki huomba intercession ya watakatifu kabla ya kumshambulia maombezi kwa Bikira Maria. Ukielewa mahusiano yetu na watakatifu wa mbinguni then ukajua nafasi ya Bikira Maria hutochanganyikiwa tena.

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
 
Unaposoma kitabu tunategemea unapata maarifa na baadaye kutumia maarifa hayo ili kukurahisishia maisha yako. Hatutegemei ufuate yale tu uliyoyoyasoma bila kuwa na ongezeko lolote ulilolipata (maarifa) kutokana na kusoma kitabu hicho. Vinginevyo utakuwa hujaelewa ulichokisoma; utakuwa umekariri.

Tumwomba au kusali kwa kulitaja jina la Yesu Kristo, lakini pia tunaongezea maombi hayo kwa kumuomba Bikira Maria atuombee kwa mwanae. Ni sawa tu wewe unaweza kumuomba kitu baba yako, halafu ukamuomba mama yako amsihi baba yako akupe hicho unachohitaji!

Tusikariri mambo, tulipewa akili ili kuweza kujiongeza. Sio kwakuwa Biblia ilisema hivi, basi tuishie pale pale tu, hapana, tunyambulishe mambo!
 
Sala ya Bikira Maria yote imetoka kwenye Biblia ...kama hujui uliza uelimishwe ndugu
 
Huyo mjinga hata hiyo bible anayozungumzia ni wakatoliki wameitunza na kuibadili lugha hata akaweza kusoma

Sent from my RMX2189 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…