Execute
JF-Expert Member
- Sep 21, 2022
- 3,000
- 7,336
Moja kati ya mambo ambayo yapo wazi kabisa katika biblia ni maelekezo ya namna maombi yanatakiwa kufanywa. Agizo la maombi lipo very open.
Yesu Kristo alisema mara nyingi sana kwenye injili ya Yohana kwamba tuombe kwa jina lake. Mtume Paulo ameandika tufanye yote katika jina la Yesu Kristo.
Sasa profesa ambaye ameandika paper kibao na amefanya literature review za kutosha ameshindwa kusoma biblia kufahamu tunapaswa kuomba kwa jina gani?
Hakuna sehemu hata moja mitume waliomba kwa jina la Maria. Yule Maria mama wa Yesu alikaa pamoja na mitume na walijazwa Roho Mtakatifu pamoja na wakanena kwa lugha.
Maria alimzaa Yesu lakini hakumzaa Mungu. Kuna tofauti kati ya Yesu na Kristo. Maria sio mama wa Mungu bali ni mama yake Yesu. Yesu ni mwanadamu na Kristo ni Mwana wa Mungu.
Hivyo Yesu Kristo ni Mungu na mwanadamu kwa wakati mmoja. Asomaye na afahamu.