Inategemea na umri wako maana Nyerere amefariki miaka 23 iliyopita. Kama ulikuwa na akili timamu wakati akipigania uhuru miaka hiyo ya 1950s na ulishuhudia, basi sio mapokeo. Lakini kama umesoma katika historia kuwa alikuwa akipigania uhuru miaka hiyo ya 1950s, basi hayo kwako ni mapokeo. Sasa baada ya maelezo hayo ujipime, kama harakati za kupigania uhuru za Nyerere kwako ni mapokeo au ulishuhudia ukiwa na akili za mtu mzima miaka hiyo
NB: Mimi miaka hiyo nilikuwa sijazaliwa, kwangu harakati za uhuru nikiziandika nitakuwa ninaandika mapokeo