Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ndugu jaribu kuumiza kichwa kidogo, sio kila mtu ana muda wa kupoteza huko MahakamaniSIoni kama ni kweli ni vile kijana hana uungwana, huyu hakutakiwa kuklsa kabisa maana ilifikia kuitwa 'Naibu Rais' , sidhani kama wanaotaka kumshtaki kama ndivyo anaogopa hawajui yuko wapi
Ndo sisi hao binadamu. Kama sio wale.Na hakuna hata 1 aliyefika. Wakina Babu Tale wakawa hadi wabunge
Hswatomshtaki unataka waumbuke ya sabaya yajirudie.SIoni kama ni kweli ni vile kijana hana uungwana, huyu hakutakiwa kuklsa kabisa maana ilifikia kuitwa 'Naibu Rais' , sidhani kama wanaotaka kumshtaki kama ndivyo anaogopa hawajui yuko wapi
NdugaiNkamia, mbunge kessy, heri james,pinda, lipumba, slaa nao wamemkacha swahiba
Yawezekana wanamuigopa boss mpyaSawa sawa ila mapema sana
Sidhani kama ana roho hiyo ila ni unafki wao na 'mentality' za kichawa, anakuwa anawaza nikienda nitaonekana vipi wakati watu wengine. Mbona Waziri Wizaea nyeti kaenda lakini kuna kina Bashiru na Hapi wako mtaani tu wanapost tu picha na mashamba ambayo unaweza kuta walipata kwa mgongo wa marehemuYawezekana wanamuigopa boss mpya
Ni kweli kabisaChama cha CCM kimemtupa mwenyekiti wao wa Taifa JPM ambaye pia alikuwa rais wa serikali ya CCM
Hii inaleta picha kuwa hawakuwa wanaamini alichokuwa anafanya mwendazake bali walikuwa wengi wao labda ni waoga kumwambia kuwa JPM hawakubaliani na ajenda zake wala vitendo vyake au wanachama hao waliokuwa na vyeo ni wachumia tumbo.
Inabidi sasa Mwenyekiti wa taifa CCM na rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan awe makini sana na wanaCCM wenye vyeo ktk chama na serikali.
Nadhani yote sawa, serikali imeshiriki kupitia Mkuu wa mkoa.Bado kuna kitu sijaelewa.
Hicho kilichofanyika Chato ni Ibada ya kumbukumbu (kifamilia), Misa ya kumuombea (kwa imani ya kikatoliki) au kumbukumbu ya kitaifa (kiserikali)?
Kweli siasa haina adui wala rafiki wa kudumu!Bila shaka ni watu ambao kwa namna moja au nyingine aliwabeba na kuwapa nafasi ya kuongoza, kujifunza na kupanda kisiasa
Aliziba masikio kelele za watu wengi dhidi ya baadhi yao na hata kukataa ushauri wa watu wa karibu na wataalamu juu ya kuwaweka pembeni, alifikia hatu kusema 'yeye ndio Rais na hapangiwi' ili tu kuendelea kuwabeba
Wengine bila yeye msingeweza kuwa mlipo sasa au kupata nafasi ambazo mlipata na mnaendelea kupata, baadhi walioneka kama 'outsiders' katika chama na serikali na hata wengine kupewa uraia ili tu mpate nafasi ya kumsaidia katika majukumu kama Mawaziri na wengine kutolewa 'Majalalani'
Wapi waliomea kipindi chake cha uongozi lakini cha kushangaza mmeshindwa kwenda kujumuika na familia na wenyeji katika sala na maombi kwa ajili yake.
Wabunge wengi ambao mlishika nafasi za 4 au chini au kuwa wageni kabisa katika chama lakini mkapewa nafasi kiasi hata kuwaacha watoto wake ili kuwapa ninyi. Wakazuia wapinzani mkashinda kiulaini Ubunge.
Nimemuona waziri wa ulinzi na kujenga Taifa Mh Innocent Bashungwa tu ambaye mbali ya kuwa ndio kwanza jana wametoka ziara ya kiserikali huko Afrika Kusini lakini ameweza kuwahi na kushiriki ibada.
Mlikuwa wapi wakina Makonda, Hapi, Mabula, Bashiru, Biteko, Doroth G, Kabudi, Babu Tale, Mwana FA, Shigongo na wengine wengi ambao bila maamuzi na mapenzi yakw binafsi msingekuwepo mlipo au kufikia ngazi mlizofika sasa