Nimeshangazwa na kauli ya Rais kudharau msimamo wa Waziri wa Kilimo juu ya kuzuia uagizaji wa sukari nje

Nani kakwabia kuwa TZ Kuna utamaduni wa kujiudhuru!sisi tuaangalia tumbo yetu bwn hata ingekuwa matusi makubwa hakuna kuhacha V8 namasurufu kibao
 
Profesa Mkenda Yuko sahihi 100%! Sukari iagizwe pale panapokuwa na nakisi Kati ya demand na local capacity of production, sio kuagiza tu kama mazoea kwani Hilo linauwa wazalishaji wa ndani!

SSH anong'onezwe, hapo kabugi!
Thats my point!
 
Kwa hiyo hapa tatizo ni Mkenda kuambiwa Hana SENCE? Ukweli Kati ya mawaziri si Mkenda peke yake ambaye Hana SENCE, wako wengi tu akiwemo wa Fedha, wa Biashara, wa Maliasili, wa Madini na kubwa Lao Afya.
Una mtazamo gani kuhusu waziri wa nishati?
 
Waziri kavunja protocol hata kama yuko sawa, kama hakubaliani ajiuzuru lakini sio kwenda kinyume na boss wako aliyekuteua tena hadharani, hizi kazi za kuteuliwa kisiasa huwezi kumkosoa au kwenda kinyume na boss wako, unatakiwa kushauri tuu tena kwa siri na kama hukubaliani ruksa kuachia ngazi
 
  1. Raisi naona anaingizwa chaka sana, sijui kama ana mfumo wa check and balance story anazoletewa
  2. Pamoja na mahaba ya raisi mwenziwe huwezi kumtusi publicly waziri mkuu na waziri wa kilimo, maana hizo stateteme zimetolewa na hao wawili
  3. Mama hana theory za uchumi, huwezi ku favour wanyabiashara jirani na kuwaua wako na kufanya nchi yako dustbin kwa bidhaaa jirani at the expenses of domestic trader.
  4. Museveni kwanini asiuze sukari yake kwa nchi zingine?
  5. Mama asijiangalia, kujipima, kujitathimini, kujiuliza what is the TRUTH ataendeshwa kama chizi mpaka ashangae at the expenses of the poor Tanzania
 
Hii nchi sijui kama ina sera...kila Rais na mitazamo yake almost kwenye kila kitu
 
Nmeona uzi hapa jana mtu anashauri Samia aruhusu cement toka Kenya, na usishangae na yeye akafanya hivyo.
Bukoba mfuko wa sementi ya ni TZS 24,000, inahitajika sana, inatafutwa sana, haipatikani!.
Sementi ikiingizwa kutoka Kenya mfuko ni TZS 12,000!.
Kama tuna upungufu, why not?.

P
 
Binafsi nimesikitika sana na kauli iliyotolewa. Inawezekana haikuwa nia yake ila alijisahau. Kati ya Mawaziri mahiri na wazalendo ni Mhe. Professa Adolf Mkenda. Nashauri atamke kuwa alipitiwa.
Kumbe ni Prof...aisee ,tumeumbwa tofauti ..Mimi huwa skubali kudhalilishwa kizembezembe!
 

Labda tutazinduka mapema na kuhakikisha mambo hayaharibiki. Kuielewa Tanzania na Watanzania wanataka nini, imekuwa kitu kigumu sana.
Mfano, Kilombero Sugar iko kwenye project ya kuongezea uzalishaji karibu maradufu. Statement za kisiasa ziendane na uhalisia huo wa hawa waliowekeza hapa nchini.
Bakheresa pale Bagamoyo na Mtwara wale wanaotaka kuanzisha kiwanda nao wanajisikiaje?
Naamini ipo nia njema ya kuliwezesha Taifa liwe kweli Taifa linalojitegemea. Kama ndivyo, tuunganishe nguvu kwa pamoja mambo yawezekane
 
Bukoba mfuko wa sementi ya ni TZS 24,000, inahitajika sana, inatafutwa sana, haipatikani!.
Sementi ikiingizwa kutoka Kenya mfuko ni TZS 12,000!.
Kama tuna upungufu, why not?.

P
Jibu ni kwamba kunawatu wanapenda Kila mtu Aishi kwa shida shida na vitu vizuri vibaki huko ulaya ila watanzania wao maisha yao yawe ya shida tu mpaka ndoto zao ziwe za kutisha tu na hata ikiwezekana wote waishi nyumba za nyasi na waishi na wanyama chumba kimoja, maji wanywe na wanyama na hata watembee uchi wote bila nguo Wala viatu ndo wanachopenda hao watu.
 

Tabia za kibandamaiti πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Ccm hupenda kuwaibia watanzania kupitia vibali vya sukari, mgao wa umeme na na kupandisha bidhaa muhimu bei.

Miaka nenda rudi sukari imekua ndio source ya wanaCcm mafisadi kuhakikisha makampuni yao yanaagiza sukari toka nje ili wapate faida kubwa huku viwanda vya ndani vikishindwa kupanuka ili kukidhi mahitaji.

Mwaka 2025 ndio wakati muafaka kuwaondoa CCM chama kinachonuka ufisadi kila kona.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…