Nimeshangazwa na kauli ya Waziri mwenye dhamana ya mitandao ya kijamii kuwa kura zipo mitaani sio mitandaoni

Umeshaambiwa ni watanzania asilimia 16% tu. Muwege mnakuwa na akili ya kuelewa basi. Hivi nyie ndo kingwangala alikuwa anawazungumzia kumbe
Nadhani anamaanisha hiyo asilimia 16 ya wanaotumia mitandao baadhi yao wanakaa vijijini na anataka kusema kudhani ni wa mjini tu unakuwa 'umepotea boya' (lugha ya wavuvi wanapopoteza direction wakiwa ziwani au baharini baada ya boya waliloweka kama alama ya kutambua nyavu zao ziko sehemu gani kutoonekana).
 
Wameishiwa hoja wanabaki kuongea vitu vya hovyo! Bure kabisa!
 
Umeshaambiwa ni watanzania asilimia 16% tu. Muwege mnakuwa na akili ya kuelewa basi. Hivi nyie ndo kingwangala alikuwa anawazungumzia kumbe
Asilimia 16? Leo hii karibu kila kaya ina smartphone. Alafu ndio iwe 16%?
 
Na raia walipo mitandaoni ndo waliopo uraiani kwa kauli ya nape humu mitandaoni yeye anaona kuna robbot
Asilimia 16? Leo hii karibu kila kaya ina smartphone. Alafu ndio iwe 16%?
We unamjibu huyu ye Kila kitu awamu hii ni kizuri hata wakimpa mimba mke wake bado atapongeza
 
Yeye kafanya utafiti na wewe fanya utafiti ili uje na takwimu zako. Research Ina chapter 5 tu.
 
huyu dogo pamoja na makamba, hawakustahili kupewa cheo chochote. sasa ndio naanza kumwelewa bashite kwanini alimfanyia yale kipindi kile. jeuri sana na anapenda kuchukiza.
 
Waziri anaponda mitandao wakati na yeye ni Member wa majukwaa kadhaa!
 
Sasa kwa nini huwa wanazima mtandao??
 
Yeye kafanya utafiti na wewe fanya utafiti ili uje na takwimu zako. Research Ina chapter 5 tu.
1. Hujaelewa nilikuwa namwongelea nani, maana niliyekuwa namjibu siyo huyo ambaye wewe ni msemaji wake.
2. Kwa vile umenipeleka huko ambako sikuwa, ngoja tu niende huko anyhow. Hakuna utafiti wowote ambao umetajwa na msemaji. Katika maelezo yake ametaja tu hizo asilimia 16 za mtandaoni na asilimia 40 diaspora na hakuonyesha hizo asilimia zimetoka wapi (hajataja chanzo cha takwimu zake).
4. Hajaeleza pia amezitapaje - ni kwa bara tu au hata Zanzibar? Ni watumiaji wa mijini tu au hata wa vijijini? Hajaeleza ni kwa mikoa mingapi!
5. Kutaja tu idadi ya watumiaji wa mitandao siyo sifa ya kufanya utafiti.
6. Je, huo utafiti unaoutaja unaitwaje na ulifanyika lini - ni wa mwaka juzi, jana au mwaka huu?
 
Kumbuka yule ni waziri hivyo anawataamu wa kumpa tamwimu kila anapozitaka
 
Kumbuka yule ni waziri hivyo anawataamu wa kumpa tamwimu kila anapozitaka
Tunaongelea utafiti uliofanyika, hatuongelei waziri wala wataalamu alio nao. By the way, kuna takwimu zimetolewa na NBS (ambao ni authority wa takwimu Tanzania) na wanaonyesha kuongezeka kwa idadi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii. Au NBS haina watalaamu wa takwimu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…