Nilichogundua baada ya kuangalia hii clip ni kwamba body language ya samia haiendani na wimbo anaouimba nape.
Maana yake ni nini..
1. Ameshatambua wanamdanganya sana na wanampaka mafuta kwa mgongo wa chupa.
2. Amegundua wapo kimaslahi zaidi na wanalinda matumbo yao.
3. Anajua huyo nape hamfai ila hakuna namna ya kumtoa..watamuendeshea fitina ambazo hataweza kupambana nazo..maana hilo ni zao la kinana na kikwete.
4. Huyu mama ni muumini wa mitandao toka siku alipotawazwa na anaiamini mitandao kuliko hao watu..kuambiwa apuuze mitandao inamchanganya sana maana anajua mitandao inafika duniani kwa haraka kuliko hao watu wa tandahimba..kuna wakati alipangua watu kwa kusoma mitandaoni tu.
5. Anaona kiza zaidi mbele kwenye safari yake ya kiuongozi kwa kushirikiana na hawa watu ambao mwanzoni alidhani watamfaa. Ni kama mwisho wa siku ama aamue kutogombea au apokee urais wa dhulma kwa maslahi ya kikundi kidogo cha watu fulani.
Kazi ipo..
Sent from my SM-A225F using
JamiiForums mobile app