Nimeshangazwa sana; Watu wanaosema kuna Rais na serikali Haramu wakisema Hakuna mtoto Haramu

Nimeshangazwa sana; Watu wanaosema kuna Rais na serikali Haramu wakisema Hakuna mtoto Haramu

Robert Heriel Mtibeli

Platinum Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
40,153
Reaction score
93,069
NIMESHANGAZWA SANA; WATU WANAOSEMA KUNA RAIS NA SERIKALI HARAMU WAKISEMA HAKUNA MTOTO HARAMU.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Nilileta mada hapa iliyozua mjadala mkubwa kuhusu mtoto haramu. Nilieleza kinaga ubaga kwamba Uharamu yaani jambo lisilo halali, kitendo kisicho halali, au matokeo yanayotokana na kitendo kisicho halali. Jinsi linavyoweza athiri kizazi.

Kilichonivutia kwenye mada ile niliyoianzisha yalizuka makundi makuu yafuatayo yale yaliyonipinga:
1. Kundi lenye huruma ya watoto.
Kundi hili halikuwa na hoja zaidi ya kusema mtoto hana hatia. Kumuita haramu ni kumzalilisha, kumfanyia ukatili na kumfanyia bullying.
Kundi hili linashindwa kuwa mtoto ni matokeo tuu. Na kuwa haramu ni matokeo. Kuwa haramu sio kosa. Isipokuwa ni status inayotokana na tendo lisilo halali. Sio kosa mtoto kuwa haramu. Ila atawajibika na kwa kosa kosa lililofanywa na watangulizi wake.
Ni kama mtoto mwenye kwashakoo au ulemavu uliosababishwa na wazazi wake.
Status ya mtoto itakuwa ni mlemavu. Na ingawaje hana makosa lakini yeye ndiye atateseka na ulemavu huo.

2. Kundi waliosema ni mitazamo na mambo ya kiutamaduni.
Wapo waliosema ni mtazamo potofu.
Wapo waliosema ni mambo ya kigeni ya waarabu na dini za kuletwa.
Hoja ya hawa ni kwamba mtoto hawezi kuwa haramu lakini bado hawakatai kwamba ni matokeo ya kitendo haramu. Hii inawaweka kwenye ukosefu wa uadilifu na ukweli wote.

Kama mtoto sio haramu basi hata kitendo kilichomleta sio haramu. Hii ina mantiki. Kwamba mwanamke na mwanaume kufanya ngono ni halali na hawatakiwi kuongozwa na sheria wala kanuni yoyote. Kumaanisha kama hakuna sheria yoyote kwenye kufanya ngono na mahusiano basi matokeo yoyote ya tendo la ngono hayapaswi kuhukumiwa katika mzani wa uhalali au uharamu.

Nikirudi kwenye siasa Siasani.

Kilichonishangaza kuliko ni waliopinga Mada yangu ni vile walivyo katika majukwaa mengine.

Wengi wa waliopinga mada hiyo mara nyingi nawaona huku kwenye siasa wakijiita, na pengine kujionyesha kama wapigania HAKI hasa HAKI ZA KISIASA.

Sikutegemea mtu kujitambulisha kama mtetezi na mpiganaji wa HAKI. ALafu asijue concept ndogo ya uharamu wa mtoto. Ni jambo linaloshangaza kidogo.

Humu kila mara tunasikia Uchaguzi haramu. Rais haramu. Wabunge haramu.
Wanaosema hivyo wanakuwa na hoja ya msingi kwa kuangalia HAKI. Pengine ni kile wakionacho HAKI kama vile wasemavyo yaani kwa mtazamo na maano yao. Lakini kiuhalisia inaweza kuwa tofauti.

Unapozungumzia suala la HAKI huwezi kulitenganisha ni human psychology ambapo hapo ndipo kuna tabia na akili za binadamu. Hizo ndio zinaamua kipi ni haki na kipi sio haki.

Kimantiki na kifalsafa. Iko hivi;
Kitendo haramu huzalisha matokeo haramu.
Hatuzungumzii matumizi ya matokeo kwa sababu kila kitu kinamatumizi iwe ni mazuri au mabaya.

Rais au serikali nzuri inaweza kupatikana kwa uchaguzi haramu. Hilo linawezekana kabisa.
Na Rais au serikali mbaya inaweza kupatikana kwa uchaguzi halali kabisa.

So mantiki ya uharamu wa tendo unaopelekea matokeo haramu haiamui faida au hasara za hayo matokeo.

Unaweza ukapata pesa kwa njia halali lakini ukazitumia kwa mambo haramu.
Na unaweza kupata kwa njia haramu lakini ukatimia kwa njia na mambo halali.
Hivyo hatuzungumzii matumizi wa matokeo ya uharamu.

Hoja ni kuwa, Tendo Haramu hupelekea matokeo haramu.

Unaposema hakuna mtoto haramu alafu hapohapo ukutwe unasema kuna Serikali au Rais Haramu unakuwa kama mtu aliyechanganyikiwa, au mwenye upeo mdogo, au usiyejua haki kwa kina.
Haki hainaga huyu ni mtoto au yule ni mtu mzima. Hiyo sio haki. Haki haingalii hayo.

Haki inachoangalia nani anastahili nini bila kujali umri, jinsia, maumbile, rangi cheo n.k.

Unaposema mtoto hana makosa. Upo sahihi lakini anawajibika kwa makosa yasiyo yake na hiyo ni HAKI.

Kama mtoto akipata faida kwa uadilifu na mafanikio ya wazazi wake inakuwa ni haki. Licha ya kuwa mtoto huyo sio mwema. Kwa nini watu waone mtoto huyohuyo akipata hasara kwa uovu na kushindwa kwa wazazi wake kama sio HAKI.
Unagundua kuwa watu wa aina hiyo ni wanafiki. Hawaijui HAKI ila wanapenda kuiimba.

Kwenye HAKI za Asili ambazo ndio msingi wa kuendeshwa kwa huu ulimwengu. Ni kuwa tendo haramu huleta matokeo haramu. Na tendo halali hupelekea matokeo halali.

Matokeo sio kosa. Ni status.
Mahakamani hautahukumiwa kwa matokeo. Utahukumiwa kwa kitendo na dhamiri.

Lakini matokeo yatabeba wajibu hata kama matokeo hayo sio kosa.

Nitakupa mfano, Dereva kafanya makosa yaani tendo haramu akakugonga na gari. Au wale waliompiga Tundu Lisu risasi.
Lile ni tendo haramu ambalo limezaa matokeo haramu ya ukilema wa Lisu.

Sio kwamba Lisu au aliyegongwa na gari anamakosa ila atawajibika kwa matokeo hayo.
Dunia haitaangalia kwa jicho la huruma. Dunia itaangalia vile jambo lilivyo.
Wapo watamuita Chiba, wapo watakaomdhihaki na kumtania majina ya ajabu. Yeye mwenyewe kutembea itamuwia vigumu. Lakin hana kosa wala hatia yoyote.

Katika Haramu.
Wapo wahanga wa haramu na wapo wanufaika wa haramu.

Jambo muhimu kuliko yote.
Haijalishi haramu inafaida au hasara. Kwa mtenda, mtendewa na matokeo (wanaojikuta wahanga wa matendo hayo).
Ni vizuri kuacha vitendo haramu.

Vitendo vya haramu ni vile ambavyo havifuati maadili ya asili na maadili ya mapokeo(mila na desturi).

Kingine, mtu kama umeamua kuisema haki. Usiseme nusu nusu. Sema haki yote bila kufumbafumba.

Kwenye haki hakuna cha mtoto wala mkubwa.
Hakuna cha maskini wala tajiri.
Hakuna cha mzungu wala muafrika.
Hakuna cha mtawala wala mtawaliwa.

Unaposema kitu fulani ni haramu lazima ujue sio kitu hicho pekee. Vipo hata ambavyo ni very sensitive na vinagusa watu wasio na hatia. Usiume ume maneno.

Kwenye HAKI hakuna kitu kwamba atajisikia vibaya, atahuzunika. Hiyo kitu haipo. Mtu hupewa na kuwekwa pale anapostahili bila kujali yeye anataka kitu gani.

Nimemaliza.

TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam
 
Unachangsny
NIMESHANGAZWA SANA; WATU WANAOSEMA KUNA RAIS NA SERIKALI HARAMU WAKISEMA HAKUNA MTOTO HARAMU.


TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam

Unachanganya mambo Taikon,
Umeshawahi ona mahali mtoto amekosa haki yake kisheria kisa ni haram? Sheria inachotaka ni uhakika kwamba ni mtoto wa mhusika, end of story.

Shida umechanganya mila, dini, siasa, tamaduni, desturi na mazoea.
 
Na kwa kuongezea tu, unapoleta hoja ya kiongozi wa nchi, utaratibu wake uko wazi, kuna sheria kikatiba ya namna mambo yanavyotakiwa kwenda ili huyo mkuu apatikane.

Unafananisha mazingira ambayo kimsingi utaratibu unaomtambua huyo mkuu uko wazi mambo yanavyotakiwa kwenda na umekiukwa watu wasitoe duku duku lao kwamba hayupo kisheria?

Tukirudi kwenye hoja ya mtoto haramu, hilo jambo lina mapokeo tofauti tofauti kwa jamii tofauti vilevile kutokana na mapokeo ya kiimani, kimila, kidini n.k

Naomba nikuulize, ni ipi tafsiri au maana ya ndoa kwa uelewa wako?
 
Tukirudi kwenye hoja ya mtoto haramu, hilo jambo lina mapokeo tofauti tofauti kwa jamii tofauti vilevile kutokana na mapokeo ya kiimani, kimila, kidini n.k
Ndugu Mtibeli, Hoja yake ni nzuri ila mifano yake ni mibovu.

Jamii za watu kama Wahadzabe wanaoishi porini au indigenous societies wana mifumo yao mingine kabisa.
 
Kijana tulia
Unamaanisha hao watu walioua vijana October 29 ili waingie ikulu ni sawa na kitendo cha kulala na mwanamke kisha kupata mtoto??
Uko wapi nitume gari kutoka milembe?

Kwanza waafrika hatuna haramu
Haramu ililetwa na waarabu kisha wabantu wakaja na msemo
"Kitanda hakizai haramu"
Wazee walioleta huu msemo hawakua wajinga kama wewe na vijana kama nyie mnawakosea sana huko walipo

1000295775.jpg
 
😀 Kuleta mada ya pili kama muendelezo wa mada ya jana ni uthibitisho kuwa mada yako ilipwaya, so you are here trying to convince yourself kuwa hukutoa boko. Like tulishamaliza umepata after thought ukaona uendelee ulikoishia.

Kauli ya uchaguzi haramu =Rais haramu + Ngono haramu = Mtoto haramu mnaijenga katika msingi mbovu. (Wazee wa fallacy mtanisaidia hii ni aina gani ya fallacy)


Iangalie kwa namna hii: Watu wazima akiwemo Rais mwenyewe wamekaa wakaharibu mchakato wa uchaguzi, wakafanya rafu, wakaua watu wakampa Kiti Rais, tukimuita Rais haramu ni sawasawa na Watu wawili waliojifungia ndani wakapeana mimba, wakazaa mtoto (Ambaye hakuwa anajua, hahusiki, wala hatambui) Akizaliwa aitwe mtoto haramu?

Inconsistency kwenye hoja hapo ni ipi au unatumia neno consistency bila kujua linahusu nini na halipaswi kuhusu nini..!



Jifunzeni kwa wapigania haki, angalieni mipaka yao katika kusema ukweli na kuonesha haki, kuna mambo huwa wanayaacha, hawashughuliki nayo… Kwanini? Kuna mpaka wa mambo binafsi, kuna taratibu za jamii, kuna sheria za nchi na kuna sheria za kimataifa (Dunia) Huwezi kumkuta Msomi mpigania haki anapambana na mambo binafsi.

Ninyi wengine ni bullies mliojivika joho la kusema ukweli /haki.


NB: Sheria ya Tz haitambui an illegitimate child. (Haitambui uwepo wa mtoto haramu) Haitambui kuwa kuna mtoto haramu. Soma uone mifano ya kesi za aina hiyo na jinsi zilivyotupwa. Kwahiyo inabidi utuambie hiyo haki ya kumuita mtoto haramu unaipigania kwa ukijiegamiza wapi!
 
NIMESHANGAZWA SANA; WATU WANAOSEMA KUNA RAIS NA SERIKALI HARAMU WAKISEMA HAKUNA MTOTO HARAMU.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.


Kwenye HAKI hakuna kitu kwamba atajisikia vibaya, atahuzunika. Hiyo kitu haipo. Mtu hupewa na kuwekwa pale anapostahili bila kujali yeye anataka kitu gani.

Nimemaliza.

TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam
Haramu kwa mujibu wa? Hapo ndipo unapopishana na baadhi ya watu tuliokupinga. Haramu kwa mujibu wa katiba ya nchi? Biblia? Makubaliano yako na mkeo? Quran? Katiba ya kikundi cha kufa na kuzikana? Kibiolojia mtoto ana afya wewe unasema ni haramu, kwa mujibu wa nini?
 
Ndoa zenyewe za kiarabu na kizungu zimeletwa miaka 1800s kabla ya hapo basi waafrika wote walikua haramu basi, na vizazi vyao vyote ikiwemo baba na babu wa mtoa mada, kwa hoja yake ya vitendo haramu kuleta matokeo haramu!
 
Mkuu hao watu wapo hata kwenye jamii, kuna vitu vya kutumia common sense kuvielewa ni ubatili kama
Mifumo ya utawala, sheria na dini
Binadamu hatukuumbwa kuishi hivyo ila "DIVIDE AND RULE"
Watu wenye akili wote wameenda juu ya mfumo au wanaishi kwa kufuata vile ambavyo ni lazima ili kuendana na mazingira ambayo tumeyakuta

kuna sehemu nimeandika jana humu kwamba hakuna matendo mema kama kufanya mambo yanayoleta uhai duniani kama kutunza mazingira na vyanzo vya maji
Hakuna mbingu/pepo zaidi ya kuwa na moyo safi kama mtoto, ila watu wanashinda makanisani na kusali mara tano huku wamejaa hasira/chuki/vinyongo kwenye mioyo yao
Nonsense
Ndugu Mtibeli, Hoja yake ni nzuri ila mifano yake ni mibovu.

Jamii za watu kama Wahadzabe wanaoishi porini au indigenous societies wana mifumo yao mingine kabisa.
 
Labda ajibu hapa ili tuendelee
Haramu kwa mujibu wa? Hapo ndipo unapopishana na baadhi ya watu tuliokupinga. Haramu kwa mujibu wa katiba ya nchi? Biblia? Makubaliano yako na mkeo? Quran? Katiba ya kikundi cha kufa na kuzikana? Kibiolojia mtoto ana afya wewe unasema ni haramu, kwa mujibu wa nini?
 
wafuasi wa ccm hata asome vipi hawezi ondoka upumbavu kichwani kwake

mbona mambo hayafanani kabisa, mfumo wa upatikanaji serikali una taratibu zake na zinatakiwa kufuatwa

ila huku kwingine inabaki mapokeo ya jamii na tamaduni zao

unafahamu kuna tamaduni mwanamke anakuwa na mke na anamiliki watoto (nyumba ndobhu) hili wazo lako kule halita eleweka

sema ukiwa ccm na umeme una flow kidogo sana kichwan
 
😀 Kuleta mada ya pili kama muendelezo wa mada ya jana ni uthibitisho kuwa mada yako ilipwaya, so you are here trying to convince yourself kuwa hukutoa boko. Like tulishamaliza umepata after thought ukaona uendelee ulikoishia.

Kauli ya uchaguzi haramu =Rais haramu + Ngono haramu = Mtoto haramu mnaijenga katika msingi mbovu. (Wazee wa fallacy mtanisaidia hii ni aina gani ya fallacy)
Kiranga
 
Ndoa zenyewe za kiarabu na kizungu zimeletwa miaka 1800s kabla ya hapo basi waafrika wote walikua haramu basi, na vizazi vyao vyote ikiwemo baba na babu wa mtoa mada, kwa hoja yake ya vitendo haramu kuleta matokeo haramu!
Mkuu suala la kuoana lipo Kwa miaka mingi hata kabla ya hizo dini.
 
Mkuu suala la kuoana lipo Kwa miaka mingi hata kabla ya hizo dini.
Kuna kuoana na kuna kwenda kusaini makaratasi huko kanisani na msikitini

Kuoana kiafrika hakuna idadi ya wanawake wala sheria uchwara zilizowekwa bali kuna mwanaume anayejenga himaya yake kadiri ya uwezo alio nao
Na huo ndio msingi wa maendeleo ya kiafrika mpaka hapa tulipo,
Kulikua na jamii yenye vijana strong wanaozalisha chakula na jamii iliishi kwa furaha, tiba za magonjwa zilikuwepo na elimu ya kujitegemea ilifundishwa
Kijana alikua akifariki jamii nzima inakaa kikao kwa nini kijana amefariki

Maisha yalikua mazuri sana ila modernisation ya wazungu ndio imetufikisha hapa sababu wametuzidi akili
Africa tulitakiwa tuachwe tuje kuwa modern kwa maarifa na ubunifu wetu wenyewe jambo ambalo lisingeepukika with time
 
Haramu maana yake sio halali. Mtoto haramu maana yake sio mtoto halali. Sasa mtoto sio halali kwa nani? Kwa jamhuri,mtoto yoyote ni halali na analindwa na sheria zote kama watoto wengine.
Kwa ukoo,sijawahi kuona ukoo umemfukuza mtoto eti kwa sababu kutokana na namna alivyozaliwa.

Kwa dini, sijawahi kusikia dini imemtenga mtoto kutokana na namna alivyozaliwa.

Sasa unaposema mtoto sio halali(haramu) ni haramu kwa nani?
 
Back
Top Bottom