NIMESHANGAZWA SANA; WATU WANAOSEMA KUNA RAIS NA SERIKALI HARAMU WAKISEMA HAKUNA MTOTO HARAMU.
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.
Nilileta mada hapa iliyozua mjadala mkubwa kuhusu mtoto haramu. Nilieleza kinaga ubaga kwamba Uharamu yaani jambo lisilo halali, kitendo kisicho halali, au matokeo yanayotokana na kitendo kisicho halali. Jinsi linavyoweza athiri kizazi.
Kilichonivutia kwenye mada ile niliyoianzisha yalizuka makundi makuu yafuatayo yale yaliyonipinga:
1. Kundi lenye huruma ya watoto.
Kundi hili halikuwa na hoja zaidi ya kusema mtoto hana hatia. Kumuita haramu ni kumzalilisha, kumfanyia ukatili na kumfanyia bullying.
Kundi hili linashindwa kuwa mtoto ni matokeo tuu. Na kuwa haramu ni matokeo. Kuwa haramu sio kosa. Isipokuwa ni status inayotokana na tendo lisilo halali. Sio kosa mtoto kuwa haramu. Ila atawajibika na kwa kosa kosa lililofanywa na watangulizi wake.
Ni kama mtoto mwenye kwashakoo au ulemavu uliosababishwa na wazazi wake.
Status ya mtoto itakuwa ni mlemavu. Na ingawaje hana makosa lakini yeye ndiye atateseka na ulemavu huo.
2. Kundi waliosema ni mitazamo na mambo ya kiutamaduni.
Wapo waliosema ni mtazamo potofu.
Wapo waliosema ni mambo ya kigeni ya waarabu na dini za kuletwa.
Hoja ya hawa ni kwamba mtoto hawezi kuwa haramu lakini bado hawakatai kwamba ni matokeo ya kitendo haramu. Hii inawaweka kwenye ukosefu wa uadilifu na ukweli wote.
Kama mtoto sio haramu basi hata kitendo kilichomleta sio haramu. Hii ina mantiki. Kwamba mwanamke na mwanaume kufanya ngono ni halali na hawatakiwi kuongozwa na sheria wala kanuni yoyote. Kumaanisha kama hakuna sheria yoyote kwenye kufanya ngono na mahusiano basi matokeo yoyote ya tendo la ngono hayapaswi kuhukumiwa katika mzani wa uhalali au uharamu.
Nikirudi kwenye siasa Siasani.
Kilichonishangaza kuliko ni waliopinga Mada yangu ni vile walivyo katika majukwaa mengine.
Wengi wa waliopinga mada hiyo mara nyingi nawaona huku kwenye siasa wakijiita, na pengine kujionyesha kama wapigania HAKI hasa HAKI ZA KISIASA.
Sikutegemea mtu kujitambulisha kama mtetezi na mpiganaji wa HAKI. ALafu asijue concept ndogo ya uharamu wa mtoto. Ni jambo linaloshangaza kidogo.
Humu kila mara tunasikia Uchaguzi haramu. Rais haramu. Wabunge haramu.
Wanaosema hivyo wanakuwa na hoja ya msingi kwa kuangalia HAKI. Pengine ni kile wakionacho HAKI kama vile wasemavyo yaani kwa mtazamo na maano yao. Lakini kiuhalisia inaweza kuwa tofauti.
Unapozungumzia suala la HAKI huwezi kulitenganisha ni human psychology ambapo hapo ndipo kuna tabia na akili za binadamu. Hizo ndio zinaamua kipi ni haki na kipi sio haki.
Kimantiki na kifalsafa. Iko hivi;
Kitendo haramu huzalisha matokeo haramu.
Hatuzungumzii matumizi ya matokeo kwa sababu kila kitu kinamatumizi iwe ni mazuri au mabaya.
Rais au serikali nzuri inaweza kupatikana kwa uchaguzi haramu. Hilo linawezekana kabisa.
Na Rais au serikali mbaya inaweza kupatikana kwa uchaguzi halali kabisa.
So mantiki ya uharamu wa tendo unaopelekea matokeo haramu haiamui faida au hasara za hayo matokeo.
Unaweza ukapata pesa kwa njia halali lakini ukazitumia kwa mambo haramu.
Na unaweza kupata kwa njia haramu lakini ukatimia kwa njia na mambo halali.
Hivyo hatuzungumzii matumizi wa matokeo ya uharamu.
Hoja ni kuwa, Tendo Haramu hupelekea matokeo haramu.
Unaposema hakuna mtoto haramu alafu hapohapo ukutwe unasema kuna Serikali au Rais Haramu unakuwa kama mtu aliyechanganyikiwa, au mwenye upeo mdogo, au usiyejua haki kwa kina.
Haki hainaga huyu ni mtoto au yule ni mtu mzima. Hiyo sio haki. Haki haingalii hayo.
Haki inachoangalia nani anastahili nini bila kujali umri, jinsia, maumbile, rangi cheo n.k.
Unaposema mtoto hana makosa. Upo sahihi lakini anawajibika kwa makosa yasiyo yake na hiyo ni HAKI.
Kama mtoto akipata faida kwa uadilifu na mafanikio ya wazazi wake inakuwa ni haki. Licha ya kuwa mtoto huyo sio mwema. Kwa nini watu waone mtoto huyohuyo akipata hasara kwa uovu na kushindwa kwa wazazi wake kama sio HAKI.
Unagundua kuwa watu wa aina hiyo ni wanafiki. Hawaijui HAKI ila wanapenda kuiimba.
Kwenye HAKI za Asili ambazo ndio msingi wa kuendeshwa kwa huu ulimwengu. Ni kuwa tendo haramu huleta matokeo haramu. Na tendo halali hupelekea matokeo halali.
Matokeo sio kosa. Ni status.
Mahakamani hautahukumiwa kwa matokeo. Utahukumiwa kwa kitendo na dhamiri.
Lakini matokeo yatabeba wajibu hata kama matokeo hayo sio kosa.
Nitakupa mfano, Dereva kafanya makosa yaani tendo haramu akakugonga na gari. Au wale waliompiga Tundu Lisu risasi.
Lile ni tendo haramu ambalo limezaa matokeo haramu ya ukilema wa Lisu.
Sio kwamba Lisu au aliyegongwa na gari anamakosa ila atawajibika kwa matokeo hayo.
Dunia haitaangalia kwa jicho la huruma. Dunia itaangalia vile jambo lilivyo.
Wapo watamuita Chiba, wapo watakaomdhihaki na kumtania majina ya ajabu. Yeye mwenyewe kutembea itamuwia vigumu. Lakin hana kosa wala hatia yoyote.
Katika Haramu.
Wapo wahanga wa haramu na wapo wanufaika wa haramu.
Jambo muhimu kuliko yote.
Haijalishi haramu inafaida au hasara. Kwa mtenda, mtendewa na matokeo (wanaojikuta wahanga wa matendo hayo).
Ni vizuri kuacha vitendo haramu.
Vitendo vya haramu ni vile ambavyo havifuati maadili ya asili na maadili ya mapokeo(mila na desturi).
Kingine, mtu kama umeamua kuisema haki. Usiseme nusu nusu. Sema haki yote bila kufumbafumba.
Kwenye haki hakuna cha mtoto wala mkubwa.
Hakuna cha maskini wala tajiri.
Hakuna cha mzungu wala muafrika.
Hakuna cha mtawala wala mtawaliwa.
Unaposema kitu fulani ni haramu lazima ujue sio kitu hicho pekee. Vipo hata ambavyo ni very sensitive na vinagusa watu wasio na hatia. Usiume ume maneno.
Kwenye HAKI hakuna kitu kwamba atajisikia vibaya, atahuzunika. Hiyo kitu haipo. Mtu hupewa na kuwekwa pale anapostahili bila kujali yeye anataka kitu gani.
Nimemaliza.
TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam