Nimeshangazwa sana; Watu wanaosema kuna Rais na serikali Haramu wakisema Hakuna mtoto Haramu

ok.πŸ’
 
Mtibeli unaenda mbali sana baba, usilinganishe uharamu wa kiongozi wa kisiasa namna alivyopatikana na mtoto kuzaliwa. Kuna jamii nyingi sana humu nchini hazina msamiati wala istilahi ya neno haramu kwa mtoto. Nenda tu hapo kanda ya kaskazini kuna jamii mtoto anazaliwa anahesabika ni wa boma fulani hata kama mama yake alichepuka akapata mimba nje au beberu la nje lilikukuja bomani na kula mzigo mimba ikapatikana. Wototo wote ni halali na ni wa mwenye boma. Kuna hawa single mothers hawana waume rasmi, wao kila anayeomba mzigo hupewa kulingana na vigezo vyao vya uchumi. Unazaa na singo maza hapa na pale. Sasa hao watoto watakuaje haramu? Mind kuwa wana wazazi wao baba na mama. Kwani kuzaa mpaka ufunge ndoa na kupewa cheti cha ndoa ndio uzae watoto halali? Uharamu ni mind set tu ya jamii fulani. Nimesema wengine hawali nyama nya nguruwe wakiamini ni haramu huku wengine wanakula kwa raha zao
 
Ndoa za kiafrika hazikuwa na kuita binadamu aliyezaliwa na mwanamke ni haramu namaanisha, uharamu uliletwa na ndoa za kizungu!
Kwa kipindi hicho ili mtoto awe halali kwako ilikuwa ni lazima umtolee mahari tofauti na hapo hata kumsogelea ulikuwa huruhusiwi.
 
Ama nene!!!

Nimemuuliza atupe mfano hai kwamba kuna mtu ameshawahi kosa haki yake kisa ni mtoto haram, na hiyo haram ni kwa muktadha upi?
 
Kamwe ziwezi kuita watoto wangu niliowazaa na wanawake tofautitofauti eti ni haramu huku niliozaa na wanawake ninaoishi nao ni halali. Watoto wote ni sawa na wana haki sawa kwa baba yao. Siruhusu mtu aite watoto au mpenzi/mke wa nje ni haramu, uharamu ni mind set tu
 
Dear hapa nakupinga hiyo ya kupigania haki ni UONGO, tena kwa hapa kwetu Bongo, km ndio hivyo Mbona mnapinga ushoga, ili hali kila mtu ana haki na uhuru wa kuchagua muenendo wake wa kingono.

Nijibu hapa. Nasubiri.
 
Mnaleta mambo ya dini kubagua watoto, hii haikubaliki. Watu wamekulana kwa raha zao mtoto akapatikani hiyo njema na inakukupasa kushukuru uzazi unaendelea. Mambo sijui mke wa ndoa, mara mke wa nje, mara mchepuko, kimada, nyumba ndogo, changudoa, kiruka njia, kahaba, wote hawa si wana mashene? Ikipigwa tu mimba itanasa na mtoto atazaliwa, wapo watoto waliozaliwa katika mazingira haya na wakawa watu maarufu katika jamii zao, mama zao walikuwa ni makahaba wa kutupwa. Kahaba naye ana mashine kama ya mke wa ndoa tu na zote ni tamu zafanana!
 
Mkuu hoja hapa sio kuwa na wanawake wengi bali hoja ni umewaowa Kwa utaratibu gani .
Hata Uislam unaruhusu kuoa wanawake wengi lakini Kuna utaratibu wa kuwaowa na sio unaowa hovyo hovyo tu.
Pia jamii zote duniani hata zisizo fuata hizo dini ulizo zisema zimejiwekea utaratibu na Sheria za kuoana na hawowani kama mbwa , inamaana ukizikiuka basi mahusiano yako yanakuwa haramu kutokana na utaratibu wa jamii husika au kabila husika ,dini au nchi husika.
 
Correct. Utaratibu wa kupatikana Rais ni wa kisheria. Utaratibu wa mtoto ni wa kibiolojia. Sasa process ya kibiolojia inawezaje kuwa halali kwa upande fulani na haramu kwa upande mwingine ?
 
Hakuna taratibu ya kiafrika inayotamka mtoto ni haramu
Sanasana kuna msemo wa kibantu usemao "kitanda hakizai haramu"
Na nina uhakika huu msemo uliletwa baada ya waarabu kuja kwa sababu neno "haramu" kwenye kamusi limekopwa kutoka kwenye lugha ya kiarabu
 
 
Basi nawewe ni mtoto haramu usituchoshe na ngonjera zako hapa
 
Mkuu mbona umekomalia waarabu kwanza ngoja nikuelimishe .
Hao waarabu unawasakama bure maana hata kwenye kitabu chao Qur'an hakuna kitu kinacho itwa mtoto haramu bali Kuna mtoto wa zinaa.
Ukijaribu kuangalia utaritu wa waislam kwenye jambo hili hawana tofauti sana na hao wazee wa zamani unao wasema.
Kwanza kwenye uislam hakuna mtoto haramu bali Kuna mtoto wa zinaa na katika hilo wazazi ndo huwa wanaadhibiwa Kwa zinaa walio ifanya mfano.
Kama ww ni muislam ukazini na mwanamke nje ya utaratibu wa dini ya kiislam basi ww huyo mtoto sio halali Yako na wala huna haki wala mamlaka juu ya huyo mtoto Kwa sababu huyo mtoto umemzaa Kwa mwanamke ambaye sio halali yako,mfano hauwezi kupita kwenye shamba la mtu ukatupa ganda alafu huo mti ukasitawi ukadai kuwa huo muembe ni wa kwako eti Kwa sababu ww ndo ulitupa mbegu ambayo ndo chanzo cha huo muembe.
Pia na Kwa hao wazee wa zamani hata mpaka Sasa Kwa baadhi ya makabira mfano wasukuma hauwezi kuwa na uhalali kwa watoto ambao umewazaa na mwanamke ambaye hujamtolea mahari.
 
Pia na Kwa hao wazee wa zamani hata mpaka Sasa Kwa baadhi ya makabira mfano wasukuma hauwezi kuwa na uhalali kwa watoto ambao umewazaa na mwanamke ambaye hujamtolea mahari.
Hapa tunaenda sawa, huyu mtoto anahesabika ni wa familia ya mwanamke au kama huyo mwanamke kaolewa mtoto atapewa jina la baba wa familia aliyemuoa huyo mwanamke ila kamwe hawezi kutengwa au kuitwa haramu.
 
Reactions: ITR
Haramu ni namba au jambo lolote lililokatazwa, lisiloruhusiwa, au kinyume cha sheria na maadili, ama katika mafundisho ya kidini (hasa Kiislamu) au katika sheria za nchi.
Kuhusu uwepo wa "watoto haramu" au "watu haramu," kibinadamu na kisheria hakuna binadamu aliye haramu, ila kuna vitendo au taratibu zinazoweza kuwa haramu.



1. Haramu ni nini?
Neno "haramu" asili yake ni Kiarabu na hutumika kumaanisha kitu kilichopigwa marufuku.
  • Katika Dini: Ni jambo ambalo ukilifanya unapata dhambi, na ukiliacha unapata thawabu (mfano: wizi, uongo, au kula vyakula vilivyokatazwa).
  • Katika Sheria za Nchi: Ni jambo lolote linalokiuka sheria za nchi (mfano: biashara ya magendo au madawa ya kulevya).

2. Je, kuna "watoto haramu"?
Kijamii na kimila, usemi "mtoto wa haramu" (illegitimate child) umekuwa ukitumika kumaanisha mtoto aliyezaliwa nje ya ndoa. Hata hivyo, mtazamo wa kisasa wa kibinadamu na kisheria unafafanua hivi:
  • Mtoto hana hatia: Kitendo kilichofanywa na wazazi (kuzini nje ya ndoa) ndicho kinachochukuliwa kuwa ni haramu au kosa, lakini mtoto mwenyewe si haramu. Kila mtoto anazaliwa akiwa safi na ana haki zote za kibinadamu.
  • Haki za Kisheria: Sheria nyingi za kimataifa na za nchi mbalimbali zinalinda haki za watoto wote bila kujali walizaliwa ndani au nje ya ndoa.

3. Je, kuna "watu haramu"?
Hakuna binadamu aliye haramu. Kila mtu ana utu na haki ya kuwepo duniani. Hata hivyo, neno hili wakati mwingine hutumika kimakosa katika mazingira yafuatayo:
  • Wahamiaji wasio na nyaraka: Katika masuala ya kisheria na kisiasa, watu wanaoingia au kuishi nchi nyingine bila kibali rasmi wakati mwingine huitwa "illegal immigrants." Lakini mashirika ya haki za binadamu yanasisitiza kuwa kitendo chao cha kuingia nchini ndicho kilicho kinyume cha sheria, lakini mtu mwenyewe si haramu.
  • Wanaofanya makosa: Mtu anaweza kufanya makosa makubwa au uhalifu (kama vile ujambazi), lakini sheria inamchukulia kama "mhalifu" na si "mtu haramu."
 
Hapa tunaenda sawa, huyu mtoto anahesabika ni wa familia ya mwanamke au kama huyo mwanamke kaolewa mtoto atapewa jina la baba wa familia aliyemuoa huyo mwanamke ila kamwe hawezi kutengwa au kuitwa haramu.
Mkuu mm sijaongelea mtoto haramu mm nilikuwa na pingana na jamaa mmoja hapo juu aliye sema eti utaratibu wa kuoana umeletwa na wazungu na waarabu ,kuoana upo Kwa maelfu ya miaka na miaka ila Kila jamii huwa inataratibu zake unazo takiwa kuzifuata kabla ya kuoa kutokana na jamii unayo toka au unayo toa mwanamke.
 
Hakuna jamii ambayo haina utaratbu wa ndoa uko sahih uharamu upo tukatae tukubali.
 
Dear hapa nakupinga hiyo ya kupigania haki ni UONGO, tena kwa hapa kwetu Bongo, km ndio hivyo Mbona mnapinga ushoga, ili hali kila mtu ana haki na uhuru wa kuchagua muenendo wake wa kingono.

Nijibu hapa. Nasubiri.
Lakini Coca unatuhukumu kwa mafungu.

πŸ˜€πŸ˜€
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…