Nimeshaoa, naombeni nifahamu mambo ninayotakiwa kufanya na kutofanya kwa mke

Nimeshaoa, naombeni nifahamu mambo ninayotakiwa kufanya na kutofanya kwa mke

Hukutak
Wakuu nilileta uzi hapa wa kuoa, basi sasa kitu ndani ya nyumba.

Sasa ningependa kupata Code kutoka kwa mliooa, vitu vya kufanya na visivyo vya kufanya (Do's and Don'ts) kwa mke. Code zinazotokana na experince ni nzuri zaidi

Hizi ni nzuri ziwe experience ambazo Wakuu wau wanachama mmejifunza kwenye ndoa sio tu ushauri.
Hukutakiwa kuoa muda wako ulikuwa hujafika
 
Wakuu nilileta uzi hapa wa kuoa, basi sasa kitu ndani ya nyumba.

Sasa ningependa kupata Code kutoka kwa mliooa, vitu vya kufanya na visivyo vya kufanya (Do's and Don'ts) kwa mke. Code zinazotokana na experince ni nzuri zaidi

Hizi ni nzuri ziwe experience ambazo Wakuu wau wanachama mmejifunza kwenye ndoa sio tu ushauri.
Are you serious? Yaani itakuwa unatania hapa! Itakuwaje unaoa ya kujua nini unatakiwa kufanya na kutofanya katika ndoa yako? Kwa hiyo ulioa kwa sababu gani hasa? Kwa nini ukaharakisha kuoa bila ya kujifunza unachotakiwa kufanya katika ndoa?
 
Andika urithi
Asijue kipato chako
Usilete ndugu kwako waishi
Asijue ratiba yako
Usiache kumpa zawad
Msifie kila siku
Mwpe hela
Mtoe out
Usile housegirl
Nunua magari mawili
Usimtafutie kazi
Mlipe mshahara
Kila siku acha hela mezani...
Hii asijuie kipato changu alivoking’ang’anizi huyu si atanitoa koromeo na anajua nafanya kazi
 
Are you serious? Yaani itakuwa unatania hapa! Itakuwaje unaoa ya kujua nini unatakiwa kufanya na kutofanya katika ndoa yako? Kwa hiyo ulioa kwa sababu gani hasa? Kwa nini ukaharakisha kuoa bila ya kujifunza unachotakiwa kufanya katika ndoa?
mkuu kama umesoma vizuri nimeandika based on Experience
 
Wakuu nilileta uzi hapa wa kuoa, basi sasa kitu ndani ya nyumba.

Sasa ningependa kupata Code kutoka kwa mliooa, vitu vya kufanya na visivyo vya kufanya (Do's and Don'ts) kwa mke. Code zinazotokana na experince ni nzuri zaidi

Hizi ni nzuri ziwe experience ambazo Wakuu wau wanachama mmejifunza kwenye ndoa sio tu ushauri.
Kuwa makini tu na yaliyotokea Igurusi usiku wa kuamkia leo

Hii husaidia sana kumaliza migogoro ndani ya Ndoa.........
Kwa hiyo Babu unatumia sana hiyo "mbwinu eeh".

On a serious note; s'times ni rahisi sana kumfanya mkeo afurahi. Yaani hata Ile umemnunulia ka-muhindi ka kuchoma; tunafurahi kwelikweli. Ile tu mtu amenifikiria, akaamua kuniletea zawadi jamani.
 
Hakikisha anadeki nyumba yote, anafua nguo zote mpaka na mazulia, afagie uwa na kukata nyasi, apike Milo yote mitatu, afute mabuibui na kusafisha vioo, alime mboga mboga, amuoshe mbwa na kumpikia mbwa, asisuke Bali uwe unamnyoa na wembe, asiende sokoni Bali uwe unamletea kila kitu.
Mwisho hakikisha ndani ya miaka 3 awe na watoto 3.
Hakikisha hajipaki mafuta zaidi ya mafuta ya kula.
Fanya hivyo mkuu utanishukuru baadae usimwonee mwanamke huruma kwenye majukumu yake yalio kwenye maandiko na kumtaftia msaidizi.
mmmh hapa kuna vingine vina utata!

baba mkwe kaniambia hatarajii mwanae achakae zaidi ya alivokua kwake
ni either apendeze au awe kama alivokua kwa wazazi wake
 
Kwa hiyo Babu unatumia sana hiyo "mbwinu eeh".

On a serious note; s'times ni rahisi sana kumfanya mkeo afurahi. Yaani hata Ile umemnunulia ka-muhindi ka kuchoma; tunafurahi kwelikweli. Ile tu mtu amenifikiria, akaamua kuniletea zawadi jamani.
Hii mbinu kusema kweli naitumia sana, maana tangu nimeanza kuitumia miaka 45 iliyopita, imefanya Bibi yenu aendelee kunivumilia

Kuna Siku nililala site kutokana na Ubovu wa barabara miaka ile ya 70's, bahati mbaya nilikosa njiwa wa kumtuma anipelekee salamu Kwa Bibi yenu.

Basi baada ya wiki 2 barabara kutengemaa, nikapita zangu mnadani na kwenye yale maduka ya Ushirika miaka ile nikanunua Jogoo Mkubwa na Khanga doti 2 nikampelekea Zawadi.

Baada ya kuona zawadi zake, hasira zake zote ziliisha 🤗
 
Wakuu nilileta uzi hapa wa kuoa, basi sasa kitu ndani ya nyumba.

Sasa ningependa kupata Code kutoka kwa mliooa, vitu vya kufanya na visivyo vya kufanya (Do's and Don'ts) kwa mke. Code zinazotokana na experince ni nzuri zaidi

Hizi ni nzuri ziwe experience ambazo Wakuu wau wanachama mmejifunza kwenye ndoa sio tu ushauri.
wale jamaa zako wa kataa ndoa sasa sio tena washauri wako, achana nao kabisaa labda ukutane nao tu kazini, ibadani au mazishini 🐒

Zingatia sana hilo,
mshauri, msaidizi na mshikaji wako namba moja katika shida na raha, huzuni, karaha, faraja na furaha sasa ni mkeo 🐒

usiwe mwepesi kutoa siri za ndani nje 🐒
Zile habari na stori za zamani na wale jamaa zako wa kataa ndoa kwamba ukitoka kunyandua, unaanza kuwahathia masela aah demu fulani anajidai sista duu lakini ndani hana maajabu wala nin ...

habari hizo hakuna tena kwenye ndoa beba msalaba wako mwenyewe na pekeyako tu 🐒
 
Mwambie mapema kila anapokopa akope kwa Jina lako maana mwenyewe jukumu la kulinda familia ni wewe, akikopa bank akope kwa Jina lako akikopa Vicoba akope kwa Jina lako akikopa kausha damu akope kwa Jina lako utakuja kulipa bila hivyo jiandae kugongewa mfululizo
 
Wakuu nilileta uzi hapa wa kuoa, basi sasa kitu ndani ya nyumba.

Sasa ningependa kupata Code kutoka kwa mliooa, vitu vya kufanya na visivyo vya kufanya (Do's and Don'ts) kwa mke. Code zinazotokana na experince ni nzuri zaidi

Hizi ni nzuri ziwe experience ambazo Wakuu wau wanachama mmejifunza kwenye ndoa sio tu ushauri.
1. Usiwe na muda maalumu wa kurudi home. Mfano leo saa 4 usiku, kesho saa 1 usiku, keshokutwa saa 6 usiku. Siku nyingine hutoki kabisa home.

2. Siku za mwanzo si za kukaa na ndugu ndani. Jengeni kwanza uwezo wa kujitegemea kwa 100%. Siyo siku ya kwanza tu una mtoto wa nani sijui unaishi naye. Kama kuna kumsaidia ndugu basi asaidiwe akiwa huko aliko. Kumbuka ndugu hawaambiani kuwa nimeshamuomba msaada fulani hivyo mwingne asubirie. Wanaweza wakaomba msaada ndug wengi kwa wakati mmoja.

3. Mkeo asijue kipata chako kwa 100%. Wanawake huwa wanatabia ya kujipangia matumizi wakishajua una shilingi ngapi.

4. Achana kabisa na mabo ya kutaka kumchunguza. Mjengee mazingira ya yeye kujichunga mwenyewe. Kumbuka, zi kila alipo utakuwepo.

5. Acha kabisa kuwaema wanaume wenzio kwake. Mfano fulani malaya, sijui yule mwizi..!! Kumbuka siku akikuona nao na huku umemwambia ubaya wao, uwezekano wa yeye kuona na wewe upo kama wao ni mkubwa sana.

6. Si kila unapoombwa msaada unatoa hapo hapo. Unless usipotoa msaada kuna kifo kitatokea. Hii hata kwa mkeo pia. Kuna wakati hata kama una hela, jifanye huna.
 
Back
Top Bottom