Nimeshawasilisha barua ya mashtaka dhidi ya Rais Samia kwenye mahakama ya The Hague ICC

matukio kama yalotokea tarehe 29 na 30 Octoba
Mkuu,
Siyo siku hizo mbili pekee.

Kwa mfano, kuna jamaa anakaa maeneo ya Bonyokwa ambako hakukuwa na vurugu wala maandamano, ila alinusurika kuliwa kichwa tarehe 1/November/2025.

Ilikuwa hivi, baadhi ya watu walihisi kuwa kufikia tarehe hiyo mambo yamepoa, wakawa wanaanza kwenda kwenye centre ya hapo kutafuta mahitaji. Mara gari ya policcm ikafika ghafla mida ya saa 6 mchana, risasi zikarushwa kwa watu, watu wakakimbilia vichochoroni chap, ila watu 8 waliuawa pale pale.

Nisikia hata Kinyerezi ilikuwa hivyo.
Labda pia kuna maeneo mengine ilikuwa hivyo
 
Ndiyo maana shughuli za kukusanya ushahidi kamili ni endelevu.
Shukrani mkuu kwa compliment.

Huwa situmii kiingereza sana lakini nikikasirishwa na jambo na nikipata mai ya kutosha, basi huamua kudondosha nondo kama hizi.

Yote hayo uliyo yaelezea, ni sehemu ya juhudi hizi za kukusanya ushahidi. Kwa hiyo tafadhali, kama kuna picha zozote zinazohusiana na tukio hilo, au mashuhuda waliolishuhudia tukio hilo ni muhimu kuwa nazo na kuziongeza kwenye barua ya mkuu 'Richard'.

Mimi naongeza ushahidi wa matumizi mabaya ya mahakama anaoufanya Samia Suluhu Hassan ili kuwanyanyasa wapinzani wake wa kisiasa. Kesi zote za mchongo zilizo anzishwa dhidi ya viongozi wa CHADEMA, kama hii ya Uhaini na juu ya kusitisha shughuli zote za chama, ni ushahidi unaopaswa kuwasilishwa.

Hata katika usikilizwaji wa kesi hizo, kuna mambo yamefanyika kusigina haki za watu juu ya uhuru kuhuzuria mahakamani. Kuna picha za viongozi wa CHADEMA waliokamatwa mahakamani Kisutu na kwenda kuvunjwa miguu na kuterekezwa porini. Kuna picha, wafuasi wa CHADEMA wakipigwa mbele ya mahakama kuu Magogoni. Zote hizi ni ushahidi unaotakiwa kuandamana na barua hiyo ya mkuu 'Richard' kuongeza uzito.

Hatuwezi pia kusahau yaliyo mkuta Marehemu Mzee Mohammed Kibao ; na Manusra Padre Kitima, huku polisi wakikejeli matukio hayo.
Mapadre kadhaa kutekwa, na kuanza kuonekana kwa mfarakanyo katika jamii kufuatana na tofauti za kiimani. Mambo ya namna hii yamekuwepo Zanzibar kwa muda, sasa yanaonekana kuwa ya kawaida hata huku Tanganyika?

Mkuu 'Richard', nami naomba nikupongeze kwa hatua yako hii mhimu sana.
Hata kama hiyo ICC hawatakuwa tayari kufanya kazi hiyo, lakini ni mhimu kuwa waTanzania wote hatukukaa kimya.
 
Jamani inatosha mjipange sasa, tuhuruminieni zikusanyeni tu na kuzipeleka kunako husika. Kwa wengine hizo images zinaanza kuwa very disturbing ukizikuta bila ya warning.
Hulazimishwi kuzifungua na kuziangalia. Sasa sielewi tatizo kwako ni nini.

Sisi sote hizi picha zinatuumiza sana; lakini ni muhimu kabisa zote zipatikane na zijumuishwe pamoja kama ushahidi wa yaliyo tokea.
Usizuie watu kuweka hizo picha kama wanazo, kwa sababu tu wewe hutaki kuziona.
Ni kama upo upande wa hao hao waovu ambao hawakutaka tukio zima lionekane!

Huwa mara kadhaa nashindwa kuelewa ni nini hasa msimamo wako sahihi katika maswala ya namna hii.

Sasa usisahau maoni yako juu ya tukio lililompata Tundu Lissu. Maoni hayo yamo humu JF.
Kama tukio hilo halikukupa hali unayojisikia kuwa nayo sasa; sielewi kwa nini hili liwe ni tofauti na lile.

Sijatukana popote, nimetoa tu maoni yangu juu ya hayo unayotoa wewe.
 
Tupo pamoja na wewe kiongozi.
Mungu akutangulie kwa elimu uliyonayo basi itumie kuwasemea watu wa mungu kupigania haki.

Silaa yako ni kalamu na akili yako. Mungu akulinde. Watu wameumia sana sana ndani ya mioyo yao
 
To: Office of the Prosecutor

International Criminal Court

The Hague.

Kingdom of Netherlands.

Subject: Submission of Evidence – Crimes Against Humanity by Samia Suluhu Hassan President of United Republic of Tanzania.
Mkuu 'Richard',

Natanguliza samahani yangu, kwako; hasa kuhusu jambo hili zito sana linalotuhusu waTanzania wote.

Nauliza tu, hii barua umeipeleka kwa njia gani huko ICC; kuhakikisha kwamba itafika na itapokelewa kwenye ofisi sahihi na wahusika wa ofisi hiyo.. Au umeituma kwa njia ya 'internet? Au kupitia Ubalozi wa Uholanzi hapa nchini?

Sihoji nia yako njema, la hasha. Natamani tu juhudi hizi zifanikiwe na kuzaa matunda mema kwetu sote; lakini ni muhimu pia kuwa na hakika kwamba tunayoyafanya, tunayafanya kwa usahihi.

Hii barua uliwakabidhi kwa mkono, au uliiwasilisha kwa wawakilishi wao hapa, kama wanayo ofisi hapa?
 
CC wamenithibitishia kuwa tiyari wana barua kadhaa kutoka kwa watanzania akiwemo mzee Malisa ambae ndiye alielianzisha ambazo zalingana na barua yangu na kwamba wapo wakisubiri barua zaidi na ushahidi wa kutosha.
Samahani.
Nilisahau mistari hii miwili nilipo andika bandiko langu hapo juu.

Unawasiliana nao kwa simu au mitandao ya kijamii?
 
Mkuu una kingereza kizuri Richard
EEeeenHeEEeeEEh!

Bila kupunguza chochote katika juhudi anazofanya mkuu 'Richard', ni vizuri pia kujuwa kuwa ChartGPT ni rafiki mzuri sana kwenye maswala ya namna hiyo.
 
So far hakuna vitendo vya kuifanya ICC iingilie kati.

Yaliyopo ni matokeo ya vyombo vya ulinzi kupambana na vitendo vya uvunjifu wa amani.

Jeshi la polisi lina majukumu ya kulinda raia na mali zake.

Pale inapotokea kuna watu wanataka kuondoa amani kwa raia wengine kufanya shughuli zao za kila siku, wanapaswa kuingilia na kurejesha utulivu.

Hao vijana hawajawahi kupeleka madai yao yeyote popote na kutosikilizwa.

Hivyo wanachokifanya ni uhuni tu na wanapaswa kuadhibiwa.

Huwezi amka tu kwako ukaenda barabarani, ukaweka mawe , ukachoma miundo mbinu, hatujui ni kwanini unafanya hivyo, halafu uachwe tu, hiyo sio sawa. Na sidhani kama kuna serikali yeyote itaacha hilo litokee.
 
EEeeenHeEEeeEEh!

Bila kupunguza chochote katika juhudi anazofanya mkuu 'Richard', ni vizuri pia kujuwa kuwa ChartGPT ni rafiki mzuri sana kwenye maswala ya namna hiyo.
πŸ™‚

Kuna mtu nilimjibu huko juu kwamba wakati nasoma miaka hiyo ChartGPT haikuwepo hivyo kiingereza kilikuwa ni lazima katika kuandika khasa dissertations. Tulikuwa twaandika sana essays hivyo zilinijenga katika kuandika.

Pili, mimi nimesoma seminary hivyo kiingereza kilikuwa ni lugha ya mawasiliano mahali pale na tulizoea sana kutokana na kufanya mijadala.

Moja ya mambo muhimu tulojifunza pale ni nidhamu na kuheshimu watu hata kama mtu huyo hawi rafiki mzuri.

Kwenye maisha halisi mie ni mtu naheshimwa sana mahali nilipo.
 
Kwamba haujaona watu wanakimbia wanafyatuliwa risasi za mgongo?

Unajua maana ya mtu kukimbia na kukupa mgongo? Maana yake ni kuwa ameretreat! Huko CCP- Moshi mnawafundisha nini polisi wetu kuhusu mtu aliyeretreat?

Haujaona clips za watu wenye mitutu wakiwa mitaani wakifyatua risasi vichochoroni, vichochoro vilivyowazi havina watu (Video zimerekodiwa kutoka juu na zinaonesha mitaa iko wazi) Walikusudia hizo risasi zimpate nani?

Hii kauli ya kuchekewa/kuachwa tu mmeipatia wapi kwasababu ni kauli ya kipuuzi kupata kutumiwa katika muktadha huu, Kuna mwenzio nimemuuliza mbadala wa kutokuachwa ni kupigwa risasi ya moto? Jeshi lote la polisi lilikaa likaona mbadala wa kutokuachwa wale β€œwahalifu” ni kupigwa risasi?? Jibu hili swali uoneshe umma akili zako zinapokaa.

Kama ninyi ndio watu mnaomzunguka Rais au wenye nafasi za uongozi mbalimbali, haishangazi kuona tuna serikali ya aina hii.

You people are very selfish, ignorant and barbaric.
 
Nimetumia njia ya kupeleka barua kwenye dawati la mapokezi na pia pana Link.

Anuani halisi kwa maana ya jengo la ICC ni kama ifuatavyo:

Oude Waalsdorperweg 10
2597 AK, The Hague
The Netherlands
Tel. + 31 (0)70 515 8515
Fax +31 (0)70 515 8555

Kwenye hiyo ya link yaitwa OPT Link bonyeza hapa: https://otplink.icc-cpi.int/

Hatua hii (kuingiza kwenye link) itakuja pale tu ushahidi wa kutosha na vielelezo vyote utakapokamilika ndipo Tanzania itawekwa rasmi humo kwenye orodha kwamba ipo kwenye ile "Preliminary Examination Process", kwani hadi sasa bado haijawekwa rasmi.

Anuani ya sehemu hiyo ambayo ushahidi waweza kuupeleka hata weye ni kama ifuatavyo:

Information and Evidence Unit
Office of the Prosecutor
Post Office Box 19519
2500 CM The Hague
The Netherlands
 
Tupo pamoja na wewe kiongozi.
Mungu akutangulie kwa elimu uliyonayo basi itumie kuwasemea watu wa mungu kupigania haki.

Silaa yako ni kalamu na akili yako. Mungu akulinde. Watu wameumia sana sana ndani ya mioyo yao
Amina Amina ndugu, tupo pamoja.
 
ICC haina uwezo wa kuingilia kati hayo si majukumu yake.

Chini ya mkataba wa Rome sehemu ya 13 yaipa uwezo nchi yoyote ile kuiamuru ICC ifanye uchunguzi wa awali (preliminary examination) ambao kama ilithibitisha kuwepo kwa ushahidi (ambao mwakazana sana kuuharibu) basi itakuja hatua ya pili ya kufanya uchunguzi kamili yaani Investigation.

Pia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa waweza kuamuru ofisi ya mwendesha mashtaka kufanya uchunguzi ndani ya nchi mwanachama dhidi ya vitendo vya mauaji na uharamia mwingine unofanywa na vikosi cya serikali.

Na njia ya tatu mwendesha mashtaka mwenyewe wa ana uwezo wa kuamua kufanya uchunguzi yeye mwenyewe.
 
Huu uzi mzito sana wa wakongwe nimeona wamejiunga 2006, kumbe 2006 jf ilikuepo
 
Hongera.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…