DOKEZO Nimeshinda Sh 27M kwenye kubet, Kampuni inataka kunipa Sh 3M, Gaming Board hainisaidii

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Kampuni au sport book? Maana kuna tofauti kati ya kampuni na kitabu husika. Kama kulikuwa na changamoto ya mtandao sheria yao inasemaje ? Wanarudisha dau au wanalipa fidia au wana cancel ushindi ? Nimuhimu kupitia pia
 
Tafuta mwanasheria akusaidie usipambane peke yako
 
Sasa mbona malalamiko ya konakona nyingi ni mengi sana kwa wakamaria,hakuna tofauti na upande wa bima za vyombo vya moto.

Wabongo wanawaza leo tu siyo hiyo kesho ndiyo chimbuko la huu uhuni.
 
sasa suala zito kama hili mtu unakuja anonymous kweli? follow up questions utajibuje huko ulipo mtoa mada.

kwanza pole sana ,

pili kama mkoa ulipo ukisikia ziara yeyote kama zile za waziri mkuu usisite kujaribu bahati yako. --- yani namaanisha gaming board ikishindwa kukusaidia na wao unawaunga kama sehemu ya watuhumiwa kwa kushindwa kutekeleza wajibu wao

tatu, kabla ya kuendelea mbele fika hapo gaming board au hata wizara ya michezo waombe mkataba wa huduma kwa wateja wa hio gaming board uusome wote kabla ya kuanza tena harakati

nakutakia kila la kheri
 
Hizo fixed match unajua vipi? Na kwanini waweke fixed match watu wabeti kama wao wanazijua?
Je kama ni janja yao kwamba Kila tukiliwa hela kubwa tuseme match ilikua fixed. Uthibitisho wa match kuwa fixed ni ngumu na haupo, pili huyu aliyebet hausikii na kufix watch yeye amebashiri matokeo atahusika tu endapo ni mchezaji au ana mahusiano ya karibu na hao waliofix match
 
Bwana mdogo mechi fixing zinatambuliwa na mfumo kutokana na indicator flan haijalishi unajua au hujui mechi kama imewekwa na bookmaker itafungwa odds na kama ulikuwa ushaweka itaondolewa na dau lako utarejeshewa. Na kila kampuni ya kubeti kwenye sheria lazima waandike hiki kipengele
 
Match fixing ili itambuliwe lazima kuwe na uchunguzi toka mamlaka husika, wala sio indicator unazosema wewe.
Match inaweza ikaondolewa na ukarudishiwa pesa kama kampuni itakuwa imefanya makosa kwenye odds.
Fuatilia mkasa wa pacueta hawakukurupuka tu pia watu kubetia option mmoja wengi haimanishii hio match ipo fixed.
Hawa Piga bet ni wezi na matapeli kuna kesi nyingi sana hata zakuweka pesa tu ni tatizo hii ni kampuni ya kiswahili
 
Your wrong brother. Mimi sijasema watu kubetia mechi moja wengi,, bali nimesema mfumo wao una uwezo wakutambua match fixing ,, na wala sio mamlaka mamlaka nikwaajili ya kufanya uchunguzi kuhitimisha tu na kutoa adhabu kwa wahusika
 
Lakini nimuhimu kusoma vigezo na masharti
 

Attachments

  • Screenshot_20260913-165214.png
    347.3 KB · Views: 10
Lakini nimuhimu kusoma vigezo na masharti
Hio vigezo Bado vinaonyesha jamaa hana makosa , walitakiwa wathibitishe kwamba match Iko fixed, solid ground evidence.
Match imechezwa italia Palermo Mimi nipo mtwara ndanda nibeti correct score 2:2 na imetoa .
Nahusika vipi na kufix match as long as results zingesoma void , ngoma imesoma winner .
Pili jamaa hajapewa sababu ya kwanini hajalipwa na inaonekana haihusiki na match fixing
 
Inawezekana kampuni haijapata faida, kwa hiyo wanaona wakilipa hizo fedha kwao ni hasara.
Tafuta wakili wawili au watatu, wakusimamie kwenye hiyo kesi; vinginevyo, ukiwa unafuatilia mwenyewe, unaweza kuatarisha maisha yako, kwa sababu wao wataangalia watumie njia zipi hizo kelele zisiwepo.​
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…