Nimeshindwa kusema uongo kwa kisingizio cha uzalendo

Nimeshindwa kusema uongo kwa kisingizio cha uzalendo

Wandugu; kuna inquiry kutoka nje (mimi ni mwanachama kwenye forum fulani inayojihusisha na investments kwenye agribusiness na SMEs). Kuna potential investor ameniuliza maoni yangu - akinukuu alichosema Dangote miaka miwili iliyopita na kuhusu maneno yasemwayo na watawala wetu - kuhusu hali ya uwekezaji hapa nchini kwa sasa.

Anataka kuwekeza kwenye food processing. Nimeshindwa kumpa maneno matamu ili aje awekeze (kumbuka kuna uwezekano wa mimi binafsi kufaidika na yeye kuwekeza hapa). Nimempa facts zifuatazo:

1. Huwezi ku-predict sasa hivi kuwa serikali itafanya nini katika mazingira yeyote
2. TRA wanaweza kukudai kiwango chochote cha kodi watakayojisikia (na ili ukate rufaa ni lazima ulipie theluthi moja ya hicho walichokuambia kuwa wanakudai; na hata ukishinda rufaa hawarudishi ulicholipa).

Nimemshauri asubiri angalau miaka 5 ijayo kunako majaaliwa tuone hali itakuwaje.
Mataga mnaruhusiwa kunitukana muwezavyo; LAKINI huo NDIO Ukweli halisi.

Nimeipenda hii ya theluthi moja.

Kinachoshangaza ni TRA kukomaa na watu wa kawaida kuwalazimisha kulipa 1/3, Ingependeza kama wangedai hiyo 1/3 ya kwa BARRICK kwenye yale maksio ya kodi.

Kwa imani tutafika tu.
 
King James Bible
And seek the peace of the city whither I have caused you to be carried away captives, and pray unto the LORD for it: for in the peace thereof shall ye have peace.

Christian Standard Bible
Pursue the well-being of the city I have deported you to. Pray to the LORD on its behalf, for when it thrives, you will thrive."

Contemporary English Version
Pray for peace in Babylonia and work hard to make it prosperous. The more successful that nation is, the better off you will be.
Jer 29:7
Nimependa neno "work hard"... kuna mambo mengine yanaweza yasiwe smooth hao wanaokwamisha au kuchelewesha mwisho wa mwezi wana mshahara, na at 60 years wana uhakika na kiinua mgongo.

So far, mimi na wewe ambao kweli tuna nia ya kutoka, ugumu na vikwazo vya sheria iko haja kutafuta suluhisho jambo lifanyike ndani nawe ukiwa mfaidika wa mchakato.

Ni wakati huuhuu kuna makaburu wanaitwa "Silverlands" wanauza vifaranga na vyakula vya kuku, kwa sasa msimu huu wa JPM; they are the leading chicken feed manufacturer in Tz.

Sasa mwenzetu, sijui ni angle ipo umekwama na sidhani you should put tools down. Sio sawa.

Sijamwambia asije, remember? Nilichofanya ni kumwambia risks zilizopo kwenye maeneo niliyoyataja. Ni ukweli kuwa yapo, na kwangu mimi sioni kuwa ni sahihi kumficha. Ni bora kumwambia ukweli ili aamue atakachoamua.
Kwangu mimk ni heri kukosa pesa kuliko credibility.
 
Kwamba si kweli kuwa Dangote alisema alichosema mwanzo (na kumbuka si mimi niliemnukuu Dangote bali ni huyo potential investor - na alinukuu matamko ya watawala pia, remember?) au si kweli kuwa ili ukate rufaa ya kodi ni LAZIMA ulipe theluthi ya ulichodaiwa?

PS: Najua kuwa sheria inasema unaweza kumuomba Kamishna Mkuu akusamehe kulipa hiyo one third; ila sijawahi kukutana na mtu aliekubaliwa so far.
Ukifuata sheria, taratibu na kanuni za kikodi, huko wala hufiki.
Mfano mdogo ni kijikampuni changu, kimekuwa assessed kodi ya TZA, 120 m pa. Kila miezi 3, ni 30m, kila mwezi ni 10m.

Baada ya Magufuli kuingia, mambo yamebadilika, hakuna biashara tena, tenda zote za serikali nimezuiwa na Saba Saba na Nane Nane nimeondolewa. Last Dec, nimeletewa tax bill ya TZS 360m za miaka 3 ya Magufuli, wakidai naendelea na biashara bila kutoa risiti!.

Nimewahakikishia, hakuna biashara kabisa, wakasisitiza hata kama hujafanya bishara yoyote, jaza tuu tax returns kuonyesha hujafanya biashara.

Ndani ya hiyo Tax bill pia wamejumlisha corporate tax ya 30% kwenye gross income, wakati corporate tax inakuwa calculated from net profits tena nionyeshe faida, hivyo ukiondoa expenses zote, kiukweli kabisa there is nothing!.

Kama ningekuwa nimefuata utaratibu toka mwanzo huku wala tusinge fika.
Wawekezaji wengi wana inflate the value of their investment costs hivyo ukijumlisha na returns of investment, mahesabu yanaonyesha hakuna faida yoyote!- kitu ambacho TRA hawakubali, ila ukiweka hesabu vizuri, TRA hawana tatizo kabisa na wewe.
P
 
Najua kuwa kuna wengine mmeamua kubuni "ukweli" wenu wenyewe na mnauamini. Bahati mbaya kwenu; investors' confidence haitokani na imagination but hard facts. Na baadhi yake ndizo hizo nilizozianisha. Sasa wewe na wenzio njooni na ushahidi kuthibitisha kuwa nilichokiandika si kweli.

Mtoa hoja mwenyewe hujielewi. Umeleta riwaya dumavu isiyo na mashiko. Ukweli unaambatana na takwimu na ushahidi kutoka vyanzo aminika( Credible sources). Mtapata taabu sana.
 
Mfiaukweli,
Ni kweli kabisa,kwa sasa kuwekeza kwenye biashara kubwa za uzalishaji ni kuji risk sana kwani serikali ni unpredictable kuna mambo mpya kila siku.Wakiona hawakupati utafunguliwa kesi za ajabu ajabu .Wao badala ya kujikita kwenye elimu ya mfanyabiashara wanaangalia wapi pa kukupatia ili wakupige kodi na fine
 
Sijamwambia asije, remember? Nilichofanya ni kumwambia risks zilizopo kwenye maeneo niliyoyataja. Ni ukweli kuwa yapo, na kwangu mimi sioni kuwa ni sahihi kumficha. Ni bora kumwambia ukweli ili aamue atakachoamua.
Kwangu mimk ni heri kukosa pesa kuliko credibility.
Kwenye risks analysis umefanya sawa. lla kwa mtu yeyote anasoma recommendation hawa anachukua kama conclusive information/counsel.

Sijui swot analysis yako ikoje na wala sihitaji kuifahamu. Ila ndiyo kama nilivyokueleza, kwa mfano hai, kuna kaburu katoka South anashrikiana na Waingereza kunzisha mradi wa kuku. Washajua population growth haina uwiano na uzalishaji wa kuku iwe wa kienyeji, layers au bowlers.Jamaa wanatuuzia vifaranga, wanauza animali feeds, net profit flows back to parent company.

Tungekuwa na sera na mikakati nyumbulifu, Benki ya kilimo, TRA, Wizara ya Biashara na Wizara ya ajira walitakiwa kukaa na wewe ili kuona longterm benefits za kwanini uwekezaji huo uje hapa.

Tanzania, Tanzania nakupenda kwa moyo wote
 
Huo mradi ulianza lini? Hapa Arusha kuna kampuni imewekeza USD 5m kwenye uzalishaji wa mbegu,na ujenzi unakaribia kwisha. Ila commitment ya mradi ni ya 2014. Siamini kuwa wangekuwa wanafanya feasibility study ya huo mradi leo wangefanya maamuzi hayo waliyoyafanya 2014.
 
Mtoa hoja mwenyewe hujielewi. Umeleta riwaya dumavu isiyo na mashiko. Ukweli unaambatana na takwimu na ushahidi kutoka vyanzo aminika( Credible sources). Mtapata taabu sana.

Endelea kuimba mapambio dada. Hapa tunajadili mambo yaliyo juu ya uwezo wako wa kuelewa.
 
Wandugu; kuna inquiry kutoka nje (mimi ni mwanachama kwenye forum fulani inayojihusisha na investments kwenye agribusiness na SMEs). Kuna potential investor ameniuliza maoni yangu - akinukuu alichosema Dangote miaka miwili iliyopita na kuhusu maneno yasemwayo na watawala wetu - kuhusu hali ya uwekezaji hapa nchini kwa sasa.

Anataka kuwekeza kwenye food processing. Nimeshindwa kumpa maneno matamu ili aje awekeze (kumbuka kuna uwezekano wa mimi binafsi kufaidika na yeye kuwekeza hapa). Nimempa facts zifuatazo:

1. Huwezi ku-predict sasa hivi kuwa serikali itafanya nini katika mazingira yeyote
2. TRA wanaweza kukudai kiwango chochote cha kodi watakayojisikia (na ili ukate rufaa ni lazima ulipie theluthi moja ya hicho walichokuambia kuwa wanakudai; na hata ukishinda rufaa hawarudishi ulicholipa).

Nimemshauri asubiri angalau miaka 5 ijayo kunako majaaliwa tuone hali itakuwaje.
Mataga mnaruhusiwa kunitukana muwezavyo; LAKINI huo NDIO Ukweli halisi.
Ongeza:
3) Mkuu wa wilaya au wa Mkoa anaweza kukusweka NDANI muda wowote atakapojisikia, kwa sababu yoyote ile.
 
Watu mumekosa uzalendo hadi mnawadanganya investors wasije kuwekeza, uzuri investors wanazidi kuja na huwa hawategemei taarifa za mtu mmoja, atakuuliza wewe na aende kuthibitisha kwa mwingine, hivyo ukikaa unsheherekea kwamba umeikomoa Tanzania, unashangaa huyo huyo muwekezaji ametangaza kutinga nchini.
Hapana hajasherehekea, ndio kwanza amesikitika ila hakuwa na namna.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom