Nimeshindwa kusema uongo kwa kisingizio cha uzalendo


Nimeipenda hii ya theluthi moja.

Kinachoshangaza ni TRA kukomaa na watu wa kawaida kuwalazimisha kulipa 1/3, Ingependeza kama wangedai hiyo 1/3 ya kwa BARRICK kwenye yale maksio ya kodi.

Kwa imani tutafika tu.
 

Sijamwambia asije, remember? Nilichofanya ni kumwambia risks zilizopo kwenye maeneo niliyoyataja. Ni ukweli kuwa yapo, na kwangu mimi sioni kuwa ni sahihi kumficha. Ni bora kumwambia ukweli ili aamue atakachoamua.
Kwangu mimk ni heri kukosa pesa kuliko credibility.
 
Kwenye huo mchoro kuna features nyingi za ajabu ajabu, mojawapo ni yule sijui farasi anamlawiti twiga.... ni nini hiki lakini..?
Huu mchoro unamaanisha kuwa TZ sasa hivi ni kama jehenamu!
 
Ukifuata sheria, taratibu na kanuni za kikodi, huko wala hufiki.
Mfano mdogo ni kijikampuni changu, kimekuwa assessed kodi ya TZA, 120 m pa. Kila miezi 3, ni 30m, kila mwezi ni 10m.

Baada ya Magufuli kuingia, mambo yamebadilika, hakuna biashara tena, tenda zote za serikali nimezuiwa na Saba Saba na Nane Nane nimeondolewa. Last Dec, nimeletewa tax bill ya TZS 360m za miaka 3 ya Magufuli, wakidai naendelea na biashara bila kutoa risiti!.

Nimewahakikishia, hakuna biashara kabisa, wakasisitiza hata kama hujafanya bishara yoyote, jaza tuu tax returns kuonyesha hujafanya biashara.

Ndani ya hiyo Tax bill pia wamejumlisha corporate tax ya 30% kwenye gross income, wakati corporate tax inakuwa calculated from net profits tena nionyeshe faida, hivyo ukiondoa expenses zote, kiukweli kabisa there is nothing!.

Kama ningekuwa nimefuata utaratibu toka mwanzo huku wala tusinge fika.
Wawekezaji wengi wana inflate the value of their investment costs hivyo ukijumlisha na returns of investment, mahesabu yanaonyesha hakuna faida yoyote!- kitu ambacho TRA hawakubali, ila ukiweka hesabu vizuri, TRA hawana tatizo kabisa na wewe.
P
 

Mtoa hoja mwenyewe hujielewi. Umeleta riwaya dumavu isiyo na mashiko. Ukweli unaambatana na takwimu na ushahidi kutoka vyanzo aminika( Credible sources). Mtapata taabu sana.
 
Mfiaukweli,
Ni kweli kabisa,kwa sasa kuwekeza kwenye biashara kubwa za uzalishaji ni kuji risk sana kwani serikali ni unpredictable kuna mambo mpya kila siku.Wakiona hawakupati utafunguliwa kesi za ajabu ajabu .Wao badala ya kujikita kwenye elimu ya mfanyabiashara wanaangalia wapi pa kukupatia ili wakupige kodi na fine
 
Kwenye risks analysis umefanya sawa. lla kwa mtu yeyote anasoma recommendation hawa anachukua kama conclusive information/counsel.

Sijui swot analysis yako ikoje na wala sihitaji kuifahamu. Ila ndiyo kama nilivyokueleza, kwa mfano hai, kuna kaburu katoka South anashrikiana na Waingereza kunzisha mradi wa kuku. Washajua population growth haina uwiano na uzalishaji wa kuku iwe wa kienyeji, layers au bowlers.Jamaa wanatuuzia vifaranga, wanauza animali feeds, net profit flows back to parent company.

Tungekuwa na sera na mikakati nyumbulifu, Benki ya kilimo, TRA, Wizara ya Biashara na Wizara ya ajira walitakiwa kukaa na wewe ili kuona longterm benefits za kwanini uwekezaji huo uje hapa.

Tanzania, Tanzania nakupenda kwa moyo wote
 

Huo mradi ulianza lini? Hapa Arusha kuna kampuni imewekeza USD 5m kwenye uzalishaji wa mbegu,na ujenzi unakaribia kwisha. Ila commitment ya mradi ni ya 2014. Siamini kuwa wangekuwa wanafanya feasibility study ya huo mradi leo wangefanya maamuzi hayo waliyoyafanya 2014.
 
Mtoa hoja mwenyewe hujielewi. Umeleta riwaya dumavu isiyo na mashiko. Ukweli unaambatana na takwimu na ushahidi kutoka vyanzo aminika( Credible sources). Mtapata taabu sana.

Endelea kuimba mapambio dada. Hapa tunajadili mambo yaliyo juu ya uwezo wako wa kuelewa.
 
Ongeza:
3) Mkuu wa wilaya au wa Mkoa anaweza kukusweka NDANI muda wowote atakapojisikia, kwa sababu yoyote ile.
 
Hapana hajasherehekea, ndio kwanza amesikitika ila hakuwa na namna.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…