Nimeshindwa kuvumilia, naomba msaada wenu jinsi ya kuachana na mzazi mwenzangu

Nimeshindwa kuvumilia, naomba msaada wenu jinsi ya kuachana na mzazi mwenzangu

Unataka ukimbie majukumu. Baba sio jina la ubatizo baba ni majukumu.
Mkiwakimbia wakifanikiwa mnaanza oo huyu ni mtoto wangu hanitunzi we ulimtunza. Upendo unajengwa hauoti tu kama magugu

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app

Kama umemuelewa "Anatafuta njia ya kutekeleza majukumu yake bila kuonana na huyo mwanamke"

Mtoto ake anamtaka ila mke hamtaki.

ANZIA HAPO...

#YNWA
 
Habarini za asubuhi waungwana.

Kwanza kabisa nichukue nafasi hii kuwapa HESHIMA ya pekee wale wote mlioko kwenye ndoa.

Turudi kwenye mada,
Nimebahatika kupata mtoto na sasa ana miezi miwili, lakini vitimbi ninavyokutana navyo kwakweli nimeshindwa kuvumilia.

Ombi langu kwenu ni hili, nahitaji kuachana kabisa na huyu mzazi mwenzangu, KABISA, isiwepo hata chembe ya mawasiliano.

Je, inawezekana kwa umri wa huyu mtoto? Kama inawezekana naomba ufafanuzi wa hatua za kuchukua ili mtoto awe katika mazingira salama. Pia Kama haiwezekani (DAAH) japo itaniumiza nishaurini cha kufanya sababu nipo mwisho.

NB:
Huyu mtu hatuishi pamoja, anaishi na mtoto na mimi naishi kivyangu ila nahusika kwa kila kitu kuhusu yeye na mtoto.

Ahsanteni.
Umedandia boti ya vibwengo
 
Kifupi sisi sio wanandoa mkuu. Ni kwamba nimempa mimba na tukakubaliana nitamtunza mpaka mtoto akifika umri wa kwenda shule namchukua mtoto maisha mengine yanaendelea.

Mahusiano Mimi na yeye yamekoma tangu akiwa na mimba ya miezi minne baada ya kuona mambo yanakuwa mengi Mimi nikabaki kumhudumia tu
Nina amini dini uliyonayo inafudisha kuwa zinaa ni dhambi,na hakuna dhambi isiyo na concequences,hayo unayoyapata ni madhara ya hiyo zinaa,yani umetembea tu na mwanamke kwa nia ya kufanya starehe na siyo kwamba ulikuwa unampenda,mwisho wa siku mimba imeingia unaanza kupiga kelele,sina kingine cha kukushauri,kifupi unalolipitia unalistahili...
 
Aisee nimekubali, unaweza kujitunza, ukawa smart katika Kila ufanyalo ila ukaja kujaa sehemu ya kifala sana.
Yes mkuu hapo umejaa kwa hio huo mzigo ni wako ushajitwisha anza na moja mlianzia wapi ili ujue njia ya kurudia

Kingine mwambie mambo ya shiriki aache au apunguze kabisa, hana dini? Au ana abudu uchawi tu? Haamini uwepo wa Mungu?

Kwa kua ushamgundua kua yeye ni chizi fresh nenda nae polepole usibadirike haraka fanya maamuzi polepole maana machizi fresh ukiwabadirikia haraka hua wanashtuka sana maana wao hua wana picha zao za mtiririko wa matukio yako, yaan yeye anajua nikifanya hivi kinachofuata ni hiki

Ushaelewa?
 
Kifupi sisi sio wanandoa mkuu. Ni kwamba nimempa mimba na tukakubaliana nitamtunza mpaka mtoto akifika umri wa kwenda shule namchukua mtoto maisha mengine yanaendelea.

Mahusiano Mimi na yeye yamekoma tangu akiwa na mimba ya miezi minne baada ya kuona mambo yanakuwa mengi Mimi nikabaki kumhudumia tu
Sasa ttz liko wapi kikubwa hauishi nae nyumba moja endelea na mambo yako uwe unamtumia matumizi tu au shd kipi?
 
Huyu mdada kipindu amebeba mimba, alisitisha huduma zote alizokuwa akijihudumia na kusema nimhudumie Mimi coz nimempa mimba, nikakubali. Akahama alikuwa amepanga(vyumba viwili na sebure) akahamia nyumba mzima, Kodi kwangu, nikakubali. Akalazimisha nitoke kazini nikaishi nae au nihakikishe Kila baada ya wiki naenda kumuona kitu ambacho hakiwezekani Kwa mazingira ya kazi yangu. Hapo ndipo mtiti uliopoanza.

Akaanza kwenda Kwa waganga usiku na mchana. Huko akaambiwa Mimi Nina mke na watoto wawili ndio maana siendi kwake muda mwingi nipo Kwa hiyo mke wangu(kifupi Mimi sijawahi kuona na hiyo mtoto wake ndio mtoto wangu wa kwanza).

Ikafika kipindi akahamia kabisa Kwa huyo sijui ndo ostadh sijui vitu gani Kila siku ni kupigwa Dua ili nirudishe mapenzi kwake niachane na huyo anaedai ni mke wangu. Kwangu nikawa nachukulia Kama ujinga flan tu. Mambo ni mengi mkuu.
Ohoooooo!! Hapo umezaa nae tu anataka kukupelekesha hivo!!!!
Umejaribu kukaa nae chini mkayajadili ???
 
Ohoooooo!! Hapo umezaa nae tu anataka kukupelekesha hivo!!!!
Umejaribu kukaa nae chini mkayajadili ???
Nishakaa nae chini zaidi ya Mara tatu mkuu. Ni kwamba ana jeuri kubwa sana na hakutegemea Kama naweza kutengana nae. Alifanya yote hayo kunikomoa mpaka kuacha kujihudumia kuanzia Pichu mpaka Kila kitu ilihali anafanya kazi.
 
Sasa ttz liko wapi kikubwa hauishi nae nyumba moja endelea na mambo yako uwe unamtumia matumizi tu au shd kipi?
Nimefanya hivi tangu mimba ikiwa na miezi minne mpaka Sasa. Ila Sasa naona kabisa mtoto wangu atakuwa katika malezi mabovu mikononi mwa huyu mama.
 
Yes mkuu hapo umejaa kwa hio huo mzigo ni wako ushajitwisha anza na moja mlianzia wapi ili ujue njia ya kurudia

Kingine mwambie mambo ya shiriki aache au apunguze kabisa, hana dini? Au ana abudu uchawi tu? Haamini uwepo wa Mungu?

Kwa kua ushamgundua kua yeye ni chizi fresh nenda nae polepole usibadirike haraka fanya maamuzi polepole maana machizi fresh ukiwabadirikia haraka hua wanashtuka sana maana wao hua wana picha zao za mtiririko wa matukio yako, yaan yeye anajua nikifanya hivi kinachofuata ni hiki

Ushaelewa?
Nashukuru sana mkuu. Ubarikiwe sana.
 
Nishakaa nae chini zaidi ya Mara tatu mkuu. Ni kwamba ana jeuri kubwa sana na hakutegemea Kama naweza kutengana nae. Alifanya yote hayo kunikomoa mpaka kuacha kujihudumia kuanzia Pichu mpaka Kila kitu ilihali anafanya kazi.
Sasa huyo ameshaona amekupanda kichwani Ndiomana!
Kama hataki kubadilika yanini kuendelea kuishi na mtu asiekupa amani?? Mtu asiyeona wala kujali msaada anaopewa ilhali ana kazi yake??

Yaeza kuwa kuna pahala unamlegezea sana anza kumkazia akili itamkaa sawa na anaeza kujirudi au kubadilika!!
 
Huyo anakufanyia vituko kwa kuwa yuko frustrated tu. Anataka umuoe. Kwanini umemzalisha halafu unataka kumuacha? Kuna dots zinamiss kwenye hii story yako.
 
Jaribu kuongea naye kwa kina maana kifuatacho ni ongezeko la Single Mother.
 
Habarini za asubuhi waungwana.

Kwanza kabisa nichukue nafasi hii kuwapa HESHIMA ya pekee wale wote mlioko kwenye ndoa.

Turudi kwenye mada,
Nimebahatika kupata mtoto na sasa ana miezi miwili, lakini vitimbi ninavyokutana navyo kwakweli nimeshindwa kuvumilia.

Ombi langu kwenu ni hili, nahitaji kuachana kabisa na huyu mzazi mwenzangu, KABISA, isiwepo hata chembe ya mawasiliano.

Je, inawezekana kwa umri wa huyu mtoto? Kama inawezekana naomba ufafanuzi wa hatua za kuchukua ili mtoto awe katika mazingira salama. Pia Kama haiwezekani (DAAH) japo itaniumiza nishaurini cha kufanya sababu nipo mwisho.

NB:
Huyu mtu hatuishi pamoja, anaishi na mtoto na mimi naishi kivyangu ila nahusika kwa kila kitu kuhusu yeye na mtoto.

Ahsanteni.
yaani wewe unatakiwa uhasiwe....sex is responsibility. Ulidhani ni starehe tu?
 
Back
Top Bottom