Nimeshindwa kwenda kumzika Mama haya maisha hayako fair naombeni msaada😭

Pole sana natumai utapata msaada pia ingependeza ufanye update umepata kiasi gani....

Back to the story ingawa haina uhusiano na mtoa mada ila nimeweka tujifunze jambo.

Nina mshikaji wangu tulisoma naye O level kuna siku akanipigia simu amefiwa na mzee wake na amefariki pale muhimbili. So wanajiandaa na kujichanga wapate hela ya jeneza na kusafirisha kwenda mtwara. Uzuri siku hiyo nilikua free so nikamwambia mi nipo msasani hapa nakuja kukupa tough muhimbili hapo unajua mambo ya msiba kusaidiana.... Haijapita dakika 10 akanipigia simu wametoka pale wanarudi home. Nikamwambia sio shida nakuja home. Akaniambia msiba hautafika home so nisiende. Hapo anasisitiza nimtumie hela ndio hitaji la muhimu.
Basi nikamwambia haina noma nitakutumia ngoja miamala isome. Sasa nikasema hebu ngoja niende muhimbili nikawasubirie maeneo ya mochwari pale. Kufika nikakaa kama saa hv nikamwambia nipo hapa daah jamaa alishtuka kinyama. Akasema asee sijakuupdate tushasafiri now tunaitafuta Mtwara....
Kwa kifupi sikutuma hela na kumbe aliwala kamba watu kibao akusanye hela.....

Mwaka juzi akafiwa kweli na mama yake aisee ilikua shughuli marafiki kumchangia mpaka mtu alienda kuhakikisha msiba kweli ndio watu wakaanza kutoa michango...

Bongo nyoso kweli.
 
Niliwahi kutapeliwa na rafiki wa kaka yangu kuwa anawenda msibani Dar tukitokea Tanga, nikamlipia nauli na kumpa pesa ya mlo njiani kumbe anakwenda kwa mwanamke Sinza
Watu wameshapigwa tayari jamaa ameshachangiwa ametokomea mitini amewaachia thread yake tuangaike nayo.
Wahuni wapo wengi wapo radhi waue mzazi ili wapate mchango
 
ata huyu jamaa muongo hajafiwa wala nini ata thread zake za nyuma nyingi anaomba omba msaada..leo baadhi ya member wamemchangia ameingia zake mitini.
Hawezi kukwambia kiasi alichopata
 
Unaishije kwani? Wenzio wanajiunga vikundi vya ujirani mwema ili kuepuka aibu kama hizo...acha ukaidi ishi vizuri na majirani..badilik
 
Ni kweli wengi wetu ni tia maji ila humu scammers wengi sana, sio kwamba hatutaki kusaidia ila trust me humu kuna mambo sana...utapeli nje nje!
 
Mungu atusaidie, ni kweli hii ni sadaka ila huwezi kutoa tu bila evidence yoyote kwamba mtu kafiwa kweli. Kama ni huruma naamini una ndugu kibao wenye uhitaji, anza nao...binafsi ikiwa verified nitatoa sadaka, la sivyo humu hapafai.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…