Dennis nakuelewa sana, humu wajuaji ni wengi sana na ukifatilia ni sura zile zile wakiwa kwenye nyuzi zingine wanajikweeeza wakibanwa sehemu wanakimbilia ujuaji na ubishi, mie naamini kama mtu hataki kumsaidia mtu akae kimya tu awapishe wengine wanaojiweza, binafsi nimejiwekea siwezi kutoa pesa kwa mtu wa mtandaoni nisiyemuona ila siwezi kuwabana wengine,
Watu wana shida jamani, ukitembea tembea hii Tanzania utaona watu wana maisha magumu na wengine hawajui hata kama wana maisha magumu, usimuite mtu tapeli ambaye hajakutapeli au kumdhalilisha na kumtweza utu wake kisa shida zake.