Nimeshuhudia mtu akiwanga, hili limenitisha

Nmekuelewa vyema kabisa mkuu ahsante kwa ushauri mzuri.
 
Unaishi wapi na maeneo gani? Ninachojua, Dar sehemu za uswazi na hata wakati mwingine sehemu zenye watu wa heshima, hizi ni drill za kawaida sana wakati wa usiku. Mimi niliwahi kuishi uswazi na mambo kama haya wala hayashangazi. Hao ni wahanga wa waganga wa kienyeji wakitekeleza maagizo na hawana madhara yoyote. Ishi bila wasiwasi.
 
Ushauri bei ya tochi zile za mwanga mkali IPO chini sana, tena ni za kucharge. Siku nyingine mmulije usoni na full light 🚨, atapagawa na kuzilahi, Kisha Nenda mpelekee moto.
Ngoja niitafute hiyo tochi
 
Wahanga wa waganga wa kienyeji si ndio hao hao wachawi? Au kuna tofauti
 
Tukio umeanza kuliona saa 4:24. Huu muda ulimaanisha saa nne usiku au saa kumi usiku/alfajiri?.
Kama ni saa kumi na dakika 24 alfajiri na wewe umeandika na kupost saa kumi na dakika 25, naweza kuamiani sasa ulimwengu wa kiroho upo fasta sana kuliko huu wa mwili
 
Wahanga wa waganga wa kienyeji si ndio hao hao wachawi? Au kuna tofauti
Hao ni mafala tu wanaliwa fedha. Unakuta mtu ameambiwa fanya abc ili utajirike etc. Mimi nilishawahi kuona mpaka dada mrembo kabisa anaoga njia panda uchi wa usiku wa manane. Bibi mmoja niliona anasugulia makalio yake kwenye mti akiwa uchi. Haya yasikutishe hata kidogo.
 
Saa 10 alfajiri, nmekuja kuandika humu saa 11 .
 
Sawa mkuu siogopi kitu
 
Potezea hiyo mambo isikufanye mtumwa.
 

Your browser is not able to display this video.

Mchawi akamatwa live na kamera ya CCTV.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…