Nimeshuhudia mtu akiwanga, hili limenitisha

Nimeshuhudia mtu akiwanga, hili limenitisha

Herini ya sikukuu ya Noeli, kwangu naona ilishakuwa mbaya kwa mfululizo wa yanayoendelea na hili lililonifanya niandike hapa muda huu.

Kwanza nianze kwa kusema sina utulivu kabisa usingizi umekata na hauwezi kuja kwahiyo kama ntakosea kwenye kuandika mnivumilie.

Ipo hivi nilikuwa ndotoni ghafla nikashtuka muda ilikuwa saa 04:24 , nilivyoshtuka naona reflections za mwanga wa moto, nikajua labda ni mwanga wa taa za gari lakini moyo ukasita kuliamini hilo kwa kuwa mwanga wa gari huwa ni mkali zaidi,

Nikiwa bado kitandani nashangaa zile reflections ghafla zikaanza kumove na kupotea, nikasogeza kapazia kidogo nione nje kinachoendelea. Nimeona moshi unafoka na nikapigia mstari majibu yangu kuwa ule ni moto.

Moyo ukapiga paa!! Nikazungusha macho upande wa pili wa dirisha nikaangalia kwa kunata bila kupepesa macho kama sekunde 40 na kushuhudia mtu kwa mbali kama kapigwa na butwaa akitazama uelekeo wangu kama vile ameniona (ni kama mita 10-15 kutoka nyumba ilipo) ila sikumtambua ni nani kutokana na giza.

Baada ya kuona vile nikarudishia pazia nimefanya maombi na ninaamini nipo salama ila hili limenishtua kwa kiasi fulani.

Wakuu nifanye nini zaidi?

Kuna madhara yeyote kushuhudia hilo?
Mshana Jr muongozo wako ni muhimu mkuu nna taharuki kwa lililotokea.
Wanaweza kukutafuta wajue umewezaje kuwaona, hivyo kuwa mwangalifu na kujishika na Yesu haswa.
 
ID yako nilidhani location California au chicago

kumbe upo hapa kwetu ......hahahah pole mkuu I wish nione hicho kitu maana mpaka sasa

sina hofu na kifo maana kifo kipo sehemu yoyote ile
Location ni bongo land mkuu jina la Id halina uhusiano wowote ule.

Utakiona tu one day
 
Yaani unamuogopa binadamu anaechoma moto sehemu
Kama unamuamini bianadamu basi utahangaika sana kwenye maisha yako
Lakini kama imani yako iko kwa Mungu basi hutapatwa na kitu ila kwa uwezo wake

Hapo mimi ningemtokea na fimbo na kumcharaza kama akizingua
Usimuogope binadamu mwenzio
Sawa mkuu hofu sina nnaamini hakuna litakalofanyika kunidhuru.
 
Uko dar ni shda, mara ya kwanza nilishuhudia mtu akipasua nazi adharani huko, pia nilishuhudia kuku akinyofolewa shingo kwa mkono alafu damu inaelekezewa kichwani kwa binti mmoja, sijui ndio alikua anazindikwa!
Mambo ni hayo hayo ya kishirikina
 
Back
Top Bottom