Unaweza kufafanua na kuiweka vizuri hoja yako?
Sisi tuliona namna alivyotoka na orodha ya watu wanaojihusisha na hiyo "kada" na watu hao kuanza kushughulikiwa!
Sasa kusema tu alifanya kinyume na bila kufafanua wakati mamlaka za kisheria zilikuwepo na hazikumchukulia hatua, yahitaji maelezo ya ziada ama ya kina kuiweka sawa hoja yako hiyo.
Mimi nimekwisha kueleza kuwa, alifitinishwa na kuonekana ni adui wa nchi baada ya kutaja na kuwanyooshea vidole watu wasiogusika, wakatumia ukwasi wao kumpaka "upupu".
Na kwa kuwa waTz ni vibendera fuata upepo, kila mtu akageuka na kumsema vibaya Makonda, bila uthibitisho wa mabaya aliyoyatenda.
Maana mpaka leo ukimuuliza mtu, ni makosa gani dhahiri ya Makonda ayaweke wazi kwa vielelezo, kwamba ni aina gani ya "rafu" alizocheza katika mchakato huo ama katika uongozi wake wa uRc, huwa hakuna wa kujibu vya maana!
Ni kesi ngapi Makonda anafunguliwa kwa kishindo,halafu zinaisha kimya kimya kama upepo wa pancha?
Sisi tunaamini kwamba jamii iliyo'corrupt' huwa imelaaniwa, ni ngumu sana kama ngamia kupita katika tundu la sindano kuirudisha katika maadili, labda kizazi chote kiangamizwe kwa kiama kama cha Sodoma, kitakapozaliwa kizazi kingine kipya, labda chaweza kuwa na maadili pamwe hofu ya Mungu!