Nimesikia asilimia 40 ya watumishi wa umma hawafanyi kazi hii inasikitisha sana ni kwasababu ya mfumo mbovu wa kiutawala uliopo

Genius Man

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2024
Posts
1,012
Reaction score
2,317
Katika uhalisia mfumo wa kiutawala unachangia kusiwe na uwajibikaji kwa watumishi wa umma nina uwakika kuna zaidi ya aslimia 99% za watumishi wa umma kuwa hawafanyi kazi zinaweza kuzidi hizi aslimia 40% nilizo zisikia.

Kutokuwa huku na uwajibikaji kwa watumishi hao kunaweza kuchangiwa na utawala uliopo mbovu kwasababu utawala ndio wasimamizi wakuu wa watumishi hao.

katika uhalisia utawala uliopo ndio wasimamizi wakuu wa watumishi hawa wasio wazalendo kama watumishi hawafanyi kazi inamaana hata hawa wasimamizi kwenye utawala pia hawafanyi kazi hili ni pengo kubwa sana kwa watanzania maskini.
 
Simbachawene anakwepa ukweli huwez mtaka mtu awajibike kwa mishahara wanayowapa ya 10k kwa siku watumishi wamekuwa hawana tofaut na wabeba zege na mama ntilie mtaan nao wanawaza kuku na mbuz zao walizofuga nyumban kujiongezea kipato
Wema sepetu anahudhuria kikao kimoja cha ccm anatoka na zaid ya 2m mtumish anashinda mwez mzima anapata 400k
Serikali iboreshe viapro na maslahi za watumish wawe wanawaza kaz sio kuku na marejesho ya vikoba
 
sazani kama watumishi wa umma hawafanyi kazi kwasababu ya mishahara, ni kwasababu ya utawala mbovu kabla ya mtu kuajiriwa sikuna mkataba ?

pamoja na hayo nafikiri hawa hawafanyi kazi kwasababu ya usimamizi mbovu na utawala mbovu wanajua hata wasipo fanya chochote mshahara wao upo pale pale kimkataba. hivyo hoja ya udogo wa mshahara haina maana kwani hawakuona wakati wanaajiriwa kuwa mshahara mdogo.
 
Watumishi kwenye sekta nyingi za serikali hawafanyi kazi inavyotakiwa.Nenda ofisi mbalimbali,baadhi ya wafanyakazi wanasingizia NETWORK,wana msururu mkubwa wa kazi,ila hawazifanyi inavyotakiwa,badala yake baadhi yao wanatumia resources za serikali kwa manufaa yao.
 
Ndiyo maana wengi wanapenda kufanya kazi serikalini.
 
Watumishi kwenye sekta nyingi za serikali hawafanyi kazi inavyotakiwa.Nenda ofisi mbalimbali,baadhi ya wafanyakazi wanasingizia NETWORK,wana msururu mkubwa wa kazi,ila hawazifanyi inavyotakiwa,badala yake baadhi yao wanatumia resources za serikali kwa manufaa yao.
kama hawafanyi kazi inamaana hata serikali haifanyi kazi
 
sazani kama watumishi wa umma hawafanyi kazi kwasababu ya mishahara, ni kwasababu ya utawala mbovu kabla ya mtu kuajiriwa sikuna mkataba ?

pamoja na hayo nafikiri hawa hawafanyi kazi kwasababu ya usimamizi mbovu na utawala mbovu wanajua hata wasipo fanya chochote mshahara wao upo pale pale kimkataba. hivyo hoja ya udogo wa mshahara haina maana kwani hawakuona wakati wanaajiriwa kuwa mshahara mdogo.
Mzee mbona kama unachukulia poa uhalisia wa malipo ya watumishi?

Unapoanza kazi serikalini inakuwa hauna ujanja ila kukubali chochote unachopewa kama kuanzia then utajiongeza ukishaanza kazi huko mbeleni.
 
Mtu maisha yake anapambana ku-survive tu halafu unamwambia aache kazi sababu mahahara mdogo hivi una akili kweli.! Mbona unaandika kama vile haujui uhalisia wa maisha ya watanzania wanyonge. Hao viongozi waanze kuboresha masilahi ya watumishi na kupunguza hela wanzolipana kwa anasa.
 
Kijana hebu kuwa na heshima kwa mtu unaeongea nae hii mitandao isikufanye uone kila mtu unalingana nae sawa, wapi nimesema waache kazi ? mshahara mdogo ndio waangie kazini kukaa? alafu wewe ndio unaniita mimi sina akili kwa hoja zako hizi?
 
Mzee mbona kama unachukulia poa uhalisia wa malipo ya watumishi?

Unapoanza kazi serikalini inakuwa hauna ujanja ila kukubali chochote unachopewa kama kuanzia then utajiongeza ukishaanza kazi huko mbeleni.
Nazani pia kuna sababu nyengine mbalimbali za watumishi hao kutofanya kazi, lakini suala la mishahara nazani limechukua sehemu ndogo tu, kwa experience yangu watumishi wengi wa ngazi mbalimbali huwa wanamishahara mizuri kulingana na vitengo na nafasi wanazo zifanyia.

yote kwa yote tunarudi kwenye mfumo mbovu wa kiutawala uliopo ndio tatizo kuu la kuwepo kwa changamoto hizo unazodai za mishahara kwa baadhi ya watumishi.
 
Mi nadhani kazi wanafanya. Sema nyie mnataka wafanye kazi ya 3 M wakati mnawalipa 500K. Wanafanya ya 500k kulingana na mnavyowalipa

Kama umebaini, watumishi wanaolipwa vizuri wanakua flexible zaidi na hata ukiwaoverwork hawana shida maana wanajua mwisho wa siku atapata safari atafidishia. You can never expect loyalty kwa mtu mwenye njaa, let’s be realistic.
 
Simbachawene anakwepa ukweli huwez mtaka mtu awajibike kwa mishahara wanayowapa ya 10k kwa siku watumishi wamekuwa hawana tofaut na wabeba zege na mama ntilie mtaan nao wanawaza kuku na mbuz zao walizofuga nyumban kujiongezea kipato
Wema sepetu anahudhuria kikao kimoja cha ccm anatoka na zaid ya 2m mtumish anashinda mwez mzima anapata 400k
Serikali iboreshe viapro na maslahi za watumish wawe wanawaza kaz sio kuku na marejesho ya vikoba
Na wao wanajilipa x 20
Nadhani mishahara ya viongozi ingepangwa na wananchi wenyewe badala ya watawala kujipangia
 
Katika uhalisia mfumo wa kiutawala unachangia kusiwe na uwajibikaji kwa watumishi wa umma nina uwakika kuna zaidi ya aslimia 99% za watumishi wa umma kuwa hawafanyi kazi zinaweza kuzidi hizi aslimia 40% nilizo zisikia.

Kutokuwa huku na uwajibikaji kwa watumishi hao kunaweza kuchangiwa na utawala uliopo mbovu kwasababu utawala ndio wasimamizi wakuu wa watumishi hao.

katika uhalisia utawala uliopo ndio wasimamizi wakuu wa watumishi hawa wasio wazalendo kama watumishi hawafanyi kazi inamaana hata hawa wasimamizi kwenye utawala pia hawafanyi kazi hili ni pengo kubwa sana kwa watanzania maskini.
Sasa wewe Kwa mwezi una mshahara wa 600K, wakati mbunge analipwa Kwa siku posho tu 600K hata ningekuwa Mimi huo moyo wa kazi unatoka wapi ??

Tunawathamini zaidi wanasiasa ndio maana mambo hayaendi.
 
sazani kama watumishi wa umma hawafanyi kazi kwasababu ya mishahara, ni kwasababu ya utawala mbovu kabla ya mtu kuajiriwa sikuna mkataba ?

pamoja na hayo nafikiri hawa hawafanyi kazi kwasababu ya usimamizi mbovu na utawala mbovu wanajua hata wasipo fanya chochote mshahara wao upo pale pale kimkataba. hivyo hoja ya udogo wa mshahara haina maana kwani hawakuona wakati wanaajiriwa kuwa mshahara mdogo.
we unasema tu.

Mtu akiwa nje (hajahajiriwa ) matarajio yake hubadilika kutokana na anachokutana nacho.

Kwa mfano: unakaa miaka 7 bila kupanda daraja au miaka 6 bila ongezeko la mshahara huo moyo hata kama mwanzo ulikuwa mzuri baadae unakufa.

Tena ukisikia mbunge anakunja 18M Kwa mwezi na 20M posho Kwa mwezi, halafu wewe 600K bila thumuni ya posho huo moyo hata uwe wa chuma unakufa.
 
Kijana hebu kuwa na heshima kwa mtu unaeongea nae hii mitandao isikufanye uone kila mtu unalingana nae sawa, wapi nimesema waache kazi ? mshahara mdogo ndio waangie kazini kukaa? alafu wewe ndio unaniita mimi sina akili kwa hoja zako hizi?
Kwa nini wengine wanalipwa 10M wengine 300K serikali moja, nchi moja ?

Kama wao ndio mahodari zaidi au walisoma vizuri ZAIDI wafanye wenyewe sisi acha tufuge nguruwe Huku tukiwa na posho ya 400 K Kwa mwezi..

hakuna ubaya....
 
Thread za watanzania ni vituko😀😀😀

Yaani mtu anaandika anadhani alafu anakomalia point zake kama vile anauwakika na kitu anachokizungumza,watanzania tujifunze kuacha porojo.

Hao wabunge wanamoral authority ipi ya kunyooshea wengine vidole wakati wao ni mzigo namba moja katika hii nchi.Nyie majitu myeusi mnashida gani lakini,mbona mnamacho lakini hamuoni???!!!?

Mnalalamika kwa vitu vya kudhani.Ni mtu gani anaakili timamu anatoa hoja na tuhuma nzito kwa vitu vya kufikirika.

Hii nchi kila mtu amechanganyikiwa,hii inapelekea watu kutafuta mchaka ya kutolea machungu yao ya maisha.Kwahiyo nyie mnaona hii failed system ipo kwa watumishi hamuona kama nchi yote ipo ICU😄😄😄
 
Kijana hebu kuwa na heshima kwa mtu unaeongea nae hii mitandao isikufanye uone kila mtu unalingana nae sawa, wapi nimesema waache kazi ? mshahara mdogo ndio waangie kazini kukaa? alafu wewe ndio unaniita mimi sina akili kwa hoja zako hizi?
Kazi watazikubali na kwa sababu kipato akiendani na mahitaji lazima wajitafutie side hustles hapo ndipo wengine hawakai au wanaondoka mapema ofisini na wengine wanakua wapiga dili hapo hapo ofisini.

Suluhisho ni kuboresha masilahi ya watumishi, kusawazisha masilahi ya wanasiasa angalao yaendane hali yetu na kutumia kodi kwa uwazi na ufanisi. Otherwise kila mtu atakula kwa urefu wa kamba yake
 
watu wanaacha kujadili sababu za msingi wanakazi ya kutupa lawama huku na kule kitu ambacho ni makelele yasiyo na tija.

Kila mwaka wataendelea kufanya study na majibu hayatabadilika kama staili ya kutatua tatizo itakuwa the same.
 
Katika uhalisia mfumo wa kiutawala unachangia kusiwe na uwajibikaji kwa watumishi wa umma nina uwakika kuna zaidi ya aslimia 99% za watumishi wa umma kuwa hawafanyi kazi zinaweza kuzidi hizi aslimia 40% nilizo zisikia.

Kutokuwa huku na uwajibikaji kwa watumishi hao kunaweza kuchangiwa na utawala uliopo mbovu kwasababu utawala ndio wasimamizi wakuu wa watumishi hao.

katika uhalisia utawala uliopo ndio wasimamizi wakuu wa watumishi hawa wasio wazalendo kama watumishi hawafanyi kazi inamaana hata hawa wasimamizi kwenye utawala pia hawafanyi kazi hili ni pengo kubwa sana kwa watanzania maskini.
Asilimia 80% awafanyi kazi
 
Back
Top Bottom