Nimesikitishwa, huzunishwa na kufadhaishwa na uongo wa Kamati ya PAC! Escrow sio fedha za umma!

Nimesikitishwa, huzunishwa na kufadhaishwa na uongo wa Kamati ya PAC! Escrow sio fedha za umma!

Mayala anaweza kulikana andiko, jamaa anatafutaga kiki ili aonekane akabidhiwe ukuu, lakini hana nyota sijui awamu hii ya ngosha mwenzake itakuwaje?! anaweza kufikiriwa labda.
 
Hata baada ya Mhe. Ngeleja kurejesha mgao wake wa escrow, kwa kuzilipa fedha hizo serikalini kuashiria amejiridhisha escrow ni fedha za umma, mimi bado nashikilia msimamo huu, kuwa fedha za escrow sio fedha za umma mpaka pale mahakama itakapota tamka otherwise.

Paskali
Pascal buana, unafukua makaburi. Pesa ni za umma au za wafanya biashara?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aje atoe ufafanuzi wa kutosha
Sent using Jamii Forums mobile app
Ufafanuzi gani wakati kule mwanzo tumesema kila kitu!.

Kwenye mabadiliko ya uongozi wa juu, kuna kitu kinaitwa kuheshimiana kati ya uongozi iliotangulia na uongozi uliopo, aliyesema Escrow sio fedha za umma ni JK, na huu ndio ukweli halisi hadi mwisho wa dunia. Baada ya kutokea mabadiliko, jamaa ndio hivyo tena, wamehifadhiwa, kuusema huu ukiukwaji wa haki za watu utakuja kuleta a very bad karmic blows as a hit back!.
Time will tell, mimi nitakuwa ninawakumbusha tuu kila mapigo yakishuka.

P.
 
Mheshimiwa alisema ataki kufukua makaburi kwasababu hawezi kuhimili harufu ya mizoga iliyozikwa humo, sasa wewe ndugu Pascal hili kaburi unalolifukua unaweza kulikabili?
 
Wanabodi,
Kwenye issue hii ya fedha za Escrow kama ni za umma au la, the authority ni ofisi ya GAG na Ripoti ya CAG ndio wakweli, Fedha za Escrow sio fedha za umma!.

Paskali
Naendelezea hapahapa~~chochote chenye public interest kina mawazo na maamuzi yanayotoka kwa watu kwa ajili ya watu,mwenyekiti wa ccm ndiye anejigeuza kuwa mwenyekiti wa Tanzania,yeye ndiye anayeamua nini kiwe for public interest na kipi kisiwe,alipomtimua mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali baada ya mkaguzi huyo kusimamia public interest wewe Pascal Mayalla hukumgombeza magufuli au kumkumbusha kuwa pesa iliyopotea ni ya umma,na mkaguzi ndiye jicho la umma,unamshangilia mwizi halafu unaongea habari za public interest,fool
Mkuu Capt Tamar ,
Asante,
Ubarikiwe
Japo sina uhakika, kwavile siwezi kusoma mabandiko ya watu wote humu, lakini humu JF, mimi ni miongoni mwa tuliomuongelea sana CAG, Ofisi ya CAG na Ripoti za CAG!.
Nakutakia Jumapili Njema
P
 
Pascally ndugu yangu huoni kama haya maneno yako ungeyasema kipindi mzee huyo JR anakamatwa hadi anapelekwa huko rupango yangekuwa na sauti?
P
 
Wanabodi,
Inawezekana PAP ni matapeli, na amenunua IPTL kitapeli, hivyo IPTL chini ya PAP ni kampuni ya kitapeli, Singasinga amefanya utapeli kuinunua IPTL kitapeli, toka kwa wamiliki halali, that is pure business hayatuhusu, bali malipo ya Tanesco kwenye account ya escrow ni kulipia capacity charges ya mitambo ya IPTL ambayo ni mitambo kweli sio mitambo hewa!, na pia Tanesco inalipia malipo ya huduma za umeme ambao sio umeme hewa, bali ni umeme kweli unaokuwa generated na mitambo ya IPTL, na imeelezwa kuwa Tanesco bado inadaiwa!. Kwa lugha rahisi, hata baada ya PAP kulipwa fedha zote zilizoko ndani ya escrow account, bado Tanesco inadaiwa!.

Paskali
Wanabodi,
Naomba kwa hapa tuwe wakweli, huyu Mzee JR akamatwe kwa kosa gani?. Aliyechota fedha za escrow ni kalasinga wa PAP, fedha za Escrow zimelipwa PAP, yeye amefanya biashara halali kabisa ya kuuza hisa zake halali ndani ya VIP kwa kumuuzia PAP, na amelipwa na PAP malipo halali kwa hisa zake, na baada ya kupokea malipo, amelipa kodi zote stahiki na halali za serikali, pesa zilizobaki ndizo amezifanyia wema kuzigawa kama sadaka au asante kwa wale aliowachagua, sasa kosa lake ni lipi?!, na waliopokea sadaka ya wema ule wana kosa gani?!. Hakuna kosa lolote kwa mtu yoyote kugawa fedha zake mwenyewe kwa yeyote, na hakuna kosa lolote kwa mtu kupokea fedha zozote halali toka kwa yeyote.
Paskali.
Hiki nilichokisema humu, kimekuja kutokea kwa Mzee JR kukamatwa na kushitakiwa. Kiukweli kabisa, huyu Mzee ameshitakiwa kwa kuonewa bure, hana kosa lolote, baada ya Habinder Sing Sethi kukiri na kuachiwa huru, kinachofuatia ni Mzee JR kufutiwa kesi na kuachiwa huru bila masharti yoyote.

Wito wangu kwa Mzee JR, maadam karma imeisha washughulikia baadhi ya watesi wake, hana sababu ya kudai fidia yoyote ya kutiwa ndani kwa zaidi ya miaka 4 bila kosa lolote, hakuna kiwango chochote cha fidia kinaweza kumfidia kwenye dunia hii, hivyo aiachie karma imalizane na watesi wake wengine waliobakia.

Welcome back uraiani Mzee wetu JR.
P
 
Back
Top Bottom