Ujinga wa watanzania wengi ndio unaosababisha wakenya wapate mwanya wa kuwatumia katika mambo mbali mbali yanayohusiana na vita vya kiuchumi, kama vile hili swala la bandari, ujenzi wa bomba kutoka Tanzania hadi Uganda, na lile lingine waliloshindwa la kule Loliondo.
Adui kabla ya kuku target ili akutumie huwa aangalia kwanza akili yako, mawazo yako, na uwezo wako wa kufikiri.
Akigundua uko weak katika mambo yote matatu, basi na yeye anapata mwanya wa kukutumia kwa njia anazozijua yeye kama wanavyotumiwa vijana wetu na wanasiasa wetu uchwara wa Tanzania.
Kamwe ujinga huo hawawezi kuwafanyia wanyarwanda, au waganda, maana wanajua fika kuwa jamaa wako vizuri vichwani mwao.