KERO Nimesoma Chuo cha Udereva Meru, kwanini sasa natakiwa kusoma tena nikiomba leseni?

KERO Nimesoma Chuo cha Udereva Meru, kwanini sasa natakiwa kusoma tena nikiomba leseni?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Chuo cha Meru Driving, Arusha, kinanirudisha kila ninapofuatilia suala hili.

Wanasema mimi ndiye mwenye makosa, wakati nilitakiwa kutumia cheti hicho muda wowote. Ninalazimishwa kutoa pesa kwa askari ili niweze kupewa leseni.

Naomba kuuliza, nilisoma, nikafanya mtihani na nikapewa cheti; kwa nini sasa siwezi kukitumia muda ninaotaka? Je, cheti nilichopewa ni feki?

Nimefuatilia suala la leseni na nikaambiwa ni lazima nisajiliwe kwenye mfumo mpya wa polisi. Pia nimeambiwa nitoe Tsh 50,000 ili nisome tena ndipo nisajiliwe kwenye mfumo huo, wakati mimi tayari nilishasoma, nikafanya mtihani na nikapewa cheti.

Naomba mamlaka husika zichunguze suala hili na kutoa ufafanuzi kuhusu uhalali wa cheti nilichopewa na sababu za kutakiwa kusoma tena na kulipia fedha hizo.
 
Back
Top Bottom