Nimesoma makala ya Paschal Mayalla "Huyu ndiye Mwalimu Nyerere ninayemfahamu" simwelewi kabisa: Critical analysis

Nimesoma makala ya Paschal Mayalla "Huyu ndiye Mwalimu Nyerere ninayemfahamu" simwelewi kabisa: Critical analysis

Pascal Mayalla siku zote huwa nasema humu miaka ya hivi karibuni amegeuka kuwa chawa sana na Kuna namna huwa anatafuta kauteuzi Fulani huko ground ili azeeke na Mimi ninachomuomba aendelee tu kupiga kelele za kumsifia mama maana mama yetu sio kiziwi Wala sio kipofu atamuona tu. Pia katika uandishi Mimi naona astaafu tu ameshazeeka asije kuharibu image nzuri aliyoitengeneza uzeeni
 
umesahau kumtukana gentleman ili upate baraka na sifa zaidi za ujasiri na heshima jukwaani 🐒
 
Pascal Mayalla siku zote huwa nasema humu miaka ya hivi karibuni amegeuka kuwa chawa sana na Kuna namna huwa anatafuta kauteuzi Fulani huko ground ili azeeke na Mimi ninachomuomba aendelee tu kupiga kelele za kumsifia mama maana mama yetu sio kiziwi Wala sio kipofu atamuona tu. Pia katika uandishi Mimi naona astaafu tu ameshazeeka asije kuharibu image nzuri aliyoitengeneza uzeeni
Ameteuliwa kuwa "DC" wa JF!
 
umesahau kutukana na kuporomosha matusi gentleman 🐒
Nimetukana mwisho kabisa hapo soma usiwe na haraka. Kumbe mkipigwa pin za hoja huwa hamfurukuti kabisa mnataka vihoja vyepesi vyepesi vya kumuulizia nchimbi ili mseme twende kwake tukamuangalie😀😀mbona hili la huu Uzi huliandikii zile makala zako ndeeeeeefu za siku zote gentleman🐒
 
ok.
asante 🐒
 
Nianze na jambo dogo kuhusu hii makala ya Mheshimiwa Paschal Mayalla. Kwanza niseme wazi, bila kumung'unya maneno. Unasoma karibu 50% ya mwanzo wa makala hiyo huku unajiuliza hii ni makala kuhusu Paschal Mayalla mwenyewe au Nyerere? Hilo tuliache.

Tuje umalizio wa makala yenyewe. Hapo ndipo Mkuu Mayalla amelikoroga kabisa. Anadiriki kumsema Samia ni mkali kama Nyerere; really Mayalla? Samia ni mkali katika mambo gani kama Nyerere? Kushughulika na wapinzani? Kuiteteta Katiba na utawala wa sheria? Kuchukia rushwa? Kutotumia nafasi yake kujitajirisha? Kuwa mdini katika teuzi? Kutumia madaraka yake kupendelea upande wa Zanzibar? Kudhoofisha muungano kwa kuwaruhusu Zanzibar wafanye mambo ambayo yako ndani ya muungano?

Hivi unawezaje hata kuwa na wazo la kulinganisha ukali wa Nyerere na Samia? Labda ni wakali kweli, lakini basi ulipaswa kusema ni wakali katika completely opposite directions - kwa mfano, kwamba Nyerere alichukia sana rushwa, na Samia anachukia sana anapoambiwa analea wala rushwa (mafisadi) nchini! Nyerere aliitetea katiba kwa nguvu zote na Samia anaibeza katiba kwa nguvu zake zote! Fikiria maneno ya Samia juu ya katiba - kijitabu tu; angethubutu kuyasema Nyerere akiwa hai? Siku hiyo ndio ingekuwa mwisho wa uraisi wake!

Kitendo cha Paschall kumweka Samia na Nyerere katika skeli ya ukali ni kuchafua kumbukumbu ya baba yako ambae alikuwa victim wa ukali wa Nyerere akiwa polisi!

Nyerere angeamua kutumia watoto wake kujitajirisha, basi leo hao kina Mako wangekuwa wanaishi kama masultan wakinukia utajiri! Nasi asiejua utajiri wa Dula umekuja baada ya mama yake kuwa raisi? Samia anakuwa raisi kwa miaka mitano, Dula anakuwa tajiri mmoja wapo mkubwa Tanzania. Nyerere anakuwa raisi kwa miaka 23, watoto wake bado wanaishi kwa mishahara na pension. Halafu unadiriki kumlinganisha Samia na Nyerere wakati wa kumbukumbu ya Nyerere? Kwa nini usitafute kebehi ya aina nyingine?

Haya, tuje kwenye tukio la Ockoba 29. Kwa masikitiko makubwa sana, Mayalla anadiriki kusema "Kilichotokea Oktoba 29, ni kikubwa kuliko kilichotokea mwaka 1976, hivyo hii ni fursa kwa Raisi Samia kumuenzi Mwalimu Nyerere kwa kumuishi". Haya ni matusi kwa Nyerere!!!!

Hivi Paschal, ina maana alietoa maelekezo ya Polisi kutumia risasi dhidi ya waandamaji ni nani, sio Samia? Alieona askari wa bara wanaweza wasitii amri ya kuua hivyo waletwe askari toka Zanzibar ni nani, sio Samia? Aliewasifia Polisi kufanya kazi nzuri kwa kuua waandamanaji ni nani, sio Samia? Aliekebehi waliofiwa kwa tukio la Oktoba 29 kwamba kwa nini wasiwazuie watoto wao kutoka ni nani, sio Samia? Sasa leo hii, Mayalla unadiriki kusema Samia atumie Oktoba 29 kumuishi Nyerere, hivi uko sawa kweli? Kwamba Raisi Samia afanyeje, amwambie DPP amfungulie mashitaka ili Samia apelekwe mahakamani kwa tukio la Oktoba 29?

Kwa kweli hapa Mayalla umenisikitisha sana. Umejiharibia sana heshima yako ya uandishi wa habari.

Refer: https://www.mwananchi.co.tz/mw/habari/siasa/huyu-ndiye-mwalimu-nyerere-ninayemfahamu-5631072
toka siku nyingi tunajua P ni mlambishwa Asali tu!
 
Miaka 50+ kwenye siasa na uchawa na bado hajawahi kulamba hata ugoro!, unategemea aandike Nini?. Mayalla angekuwa shoger huyo angekuwa kwenye level za kina Juma lokole.... Mayalla ni mmoja ya waandishi wa habari wajingawajinga na ambao anayependa kuteuliwa ila hana hiyo bahata.... Matokeo yake anawaza kutumia mataqo yake.
 
Nawaelewa chawa ambao tayari wana nafasi fulani na wanakuwa machawa kulinda nafasi zao. Pascall kuwa chawa kutamsaidia nini kama hayuko katika nafasi ya maslahi? Si bora tu awe mzalendo wa kweli?
Kwahiyo Maghufuli aliposema ana njaa wewe unadhani alimaanisha nini?
 
Fikiria maneno ya Samia juu ya katiba - kijitabu tu; angethubutu kuyasema Nyerere akiwa hai? Siku hiyo ndio ingekuwa mwisho wa uraisi wake!
Nahisi Nyerere angemtia fimbo za Matako, wewe hii kitu imetuchukua miaka wewe unasema nini mtunzi Shaban Robert wa Kusadikika ni Kijitabu tu?
 
Miaka 50+ kwenye siasa na uchawa na bado hajawahi kulamba hata ugoro!, unategemea aandike Nini?. Mayalla angekuwa shoger huyo angekuwa kwenye level za kina Juma lokole.... Mayalla ni mmoja ya waandishi wa habari wajingawajinga na ambao anayependa kuteuliwa ila hana hiyo bahata.... Matokeo yake anawaza kutumia mataqo yake.
Oya punguza
 
Nahisi Nyerere angemtia fimbo za Matako, wewe hii kitu imetuchukua miaka wewe unasema nini mtunzi Shaban Robert wa Kusadikika ni Kijitabu tu?
Kuna mbunge mjinga mwingine naye, Cherehani, kwa kutiwa moyo na kuli ya samia ya katiba ni kitabu, karopoka sana kuhusu katiba. Eti anauliza katiba itakuwekea chakula mezani> Eboo, hajui katiba mbovu inaweza kuleta vurugu nchini hata hicho chakula mezami kisiwepo? Kuna watu akili ni zero kabisa

View: https://www.youtube.com/shorts/FoPUixfm1rA
 
Nawaelewa chawa ambao tayari wana nafasi fulani na wanakuwa machawa kulinda nafasi zao. Pascall kuwa chawa kutamsaidia nini kama hayuko katika nafasi ya maslahi? Si bora tu awe mzalendo wa kweli?

Pascal Mayalla akiwa mzalendo wa kweli watamshughulikia. Anajua jinsi ya kusukuma kete zake. Na uzee wake huo aanze purukushani na system kisa uzalendo
 
Narudia tena, Mayalla umefedhehesha sana Watanzania wanaomfahamu Nyerere kwa makala yako hii. Obviously, pamoja na kuwa na namna ya ukaribu na Nyerere kuliko sisi wengine, humfahamu kabisa Nyerere
Nimesoma alichoandika Mayalla na unachosema ww ni tofauti. Hajasema Samia anafanana na Nyerere, ila anamtaka Samia aige alichofanya Nyerere.
 
Naheshimu maoni ya watu lakini sijawahi kumuelewa Mayalla,na nina wasiwasi na judgment ya mtu anayemuona Makonda anafaa kuwa raisi
 
Back
Top Bottom