Nimesoma makala ya Paschal Mayalla "Huyu ndiye Mwalimu Nyerere ninayemfahamu" simwelewi kabisa: Critical analysis

Nimesoma alichoandika Mayalla na unachosema ww ni tofauti. Hajasema Samia anafanana na Nyerere, ila anamtaka Samia aige alichofanya Nyerere.
Nadhani hujanielewa. Issue ni kwamba kuna incosistent kubwa sana katika alichoandika hakieleweki. Kwa mfano, unawezaje kusema Samia amwige Nyerere kuhusu issue ya Octoba 29 wakati ukijua Samia ndio chanzo cha mauaji ya Octoba 29?

Unasemaje Samia ni Mkali kama alivyokua Nyerere? Ukali wa Samia unaanzia wapi kuulinganisha? Ukali kwenye nini, watu wanaokukosoa?
 
Kweli hata mimi nimetoka kusoma sasa hivi nadhani hapa tunamuonea Mayalla
Nikuulize, kwa mfano Mayalla anasema "Pili, ni kupitia Katiba mpya, falsafa ya Nyerere ilikuwa ni serikali mbili, kuelekea serikali moja, hivyo Tanzania kuwa nchi moja, serikali moja na rais mmoja. Kwa mujibu wa mwelekeo wa siasa zetu, ndoto ya Mwalimu ya kuwa nchi moja na serikali moja, inaweza kutimia tu kipindi ambacho rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anatoka Zanzibar"

Yaani kwa jinsi Samia anavyotumia mfumo wa serikali mbili kuikamua Tanzania bara bado Mayalla anasema Samia akazie hapo hapo kwenye serikali mbili? Ni mtu asioona ndio bado hataona ujinga unaofanyika kwa sasa chini ya kisingizio cha serikali mbili. Tanzania bara ni lazima iwe na serikali yake, ili kuondoa chuki na ukandamizaji wa upnde wa bara unaofanyika, hasa tukiwa na raisi kutoka Zanzibar. Unafikiri kuna jambo lolote lile hadi sasa, ambalo Zanzibar hawafanyi kama nchi huru, ukiondoa suala la JWTZ? Kimebaki nini? Bado unang'ang'ania serikali mbili?

Hivi hujagundua katika sehemu nyeti zote za serikali kwa hivi sasa, Samia kawapa zishikwe na Wazanzibar? Sawa tuna Mkuu JWTZ wa bara, lakini Chief of Staff wa JWTZ (mnadhimu mkuu) ni wa wapi? Na nani ana nguvu jeshini saa hizi, waulize wanajeshi. Mkunda ana nguvu yeyote jeshini ya kufanya aheshimiwe na raisi kama ilivyokuwa kwa kina Kiaro nk wakati wa Mwinyi?

Na hujagundua kuwa zilke nafasi nyeti chache ambazo hajawapa Wazanzibar anadanganyia kuzitoa kwa watu wa bara lakini kwa uteuzi wa kidini? Hivi watu hamuoni hivi vitu? Sasa huyo ni wa namna ya Nyerere?
 
Pascal ni chawa ambaye anapambana walau aonekane. Jua limeshazama na anaona mambo hayajakaa sawa. Lazima apambane kama chawa mwandamizi ili walau wakuu wamuone. Tumsamehe bure. Anaendeshwa na tumbo kuliko kutumia akili
 
Nimesoma alichoandika Mayalla na unachosema ww ni tofauti. Hajasema Samia anafanana na Nyerere, ila anamtaka Samia aige alichofanya Nyerere.
Kweli hata mimi nimetoka kusoma sasa hivi nadhani hapa tunamuonea Mayalla

Nadhani hujanielewa. Issue ni kwamba kuna incosistent kubwa sana katika alichoandika hakieleweki. Kwa mfano, unawezaje kusema Samia amwige Nyerere kuhusu issue ya Octoba 29 wakati ukijua Samia ndio chanzo cha mauaji ya Octoba 29?

Unasemaje Samia ni Mkali kama alivyokua Nyerere? Ukali wa Samia unaanzia wapi kuulinganisha? Ukali kwenye nini, watu wanaokukosoa?
Nikuulize, kwa mfano Mayalla anasema "Pili, ni kupitia Katiba mpya, falsafa ya Nyerere ilikuwa ni serikali mbili, kuelekea serikali moja, hivyo Tanzania kuwa nchi moja, serikali moja na rais mmoja. Kwa mujibu wa mwelekeo wa siasa zetu, ndoto ya Mwalimu ya kuwa nchi moja na serikali moja, inaweza kutimia tu kipindi ambacho rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anatoka Zanzibar"

Yaani kwa jinsi Samia anavyotumia mfumo wa serikali mbili kuikamua Tanzania bara bado Mayalla anasema Samia akazie hapo hapo kwenye serikali mbili? Ni mtu asioona ndio bado hataona ujinga unaofanyika kwa sasa chini ya kisingizio cha serikali mbili. Tanzania bara ni lazima iwe na serikali yake, ili kuondoa chuki na ukandamizaji wa upnde wa bara unaofanyika, hasa tukiwa na raisi kutoka Zanzibar. Unafikiri kuna jambo lolote lile hadi sasa, ambalo Zanzibar hawafanyi kama nchi huru, ukiondoa suala la JWTZ? Kimebaki nini? Bado unang'ang'ania serikali mbili?

Hivi hujagundua katika sehemu nyeti zote za serikali kwa hivi sasa, Samia kawapa zishikwe na Wazanzibar? Sawa tuna Mkuu JWTZ wa bara, lakini Chief of Staff wa JWTZ (mnadhimu mkuu) ni wa wapi? Na nani ana nguvu jeshini saa hizi, waulize wanajeshi. Mkunda ana nguvu yeyote jeshini ya kufanya aheshimiwe na raisi kama ilivyokuwa kwa kina Kiaro nk wakati wa Mwinyi?

Na hujagundua kuwa zilke nafasi nyeti chache ambazo hajawapa Wazanzibar anadanganyia kuzitoa kwa watu wa bara lakini kwa uteuzi wa kidini? Hivi watu hamuoni hivi vitu? Sasa huyo ni wa namna ya Nyerere?

Mkuu mtoa mada, naomba nikupongeze kwa uchambuzi wako wa kina. Kiukweli, umenifumbua macho sana. Mwanzoni, nikiri wazi kuwa hata mimi nilikuwa 'fooled' kama alivyokuwa mdau Tindo. Nilisoma makala ya Paschal Mayalla kijuujuu na kuona kama ni ushauri wa kawaida tu wa kizalendo wa kumtaka Rais amuige Mwalimu Nyerere.

Lakini kwa kuangalia muktadha wa matukio ya Oktoba 29 na jinsi ulivyochambua kinyume hicho cha kimantiki, umenifanya nielewe vizuri kile kinachoitwa kiweledi 'Calculated Sycophancy' au 'Diplomasia ya Kalamu.'
Katika uandishi wa habari na uchambuzi wa kisiasa—hasa kwenye nchi zetu hizi ambazo uhuru wa habari una mipaka yake—waandishi wengi wakongwe kama Mayalla hutumia mbinu hii ya kimkakati. Huu ni uandishi wa 'kujipendekeza kimkakati' au 'kusifu kwa mtego.' Mwandishi anajua fika kuwa hawezi kunyoosha kidole moja kwa moja kwa Mkuu wa Nchi na kumlaumu kwa matukio ya Oktoba 29 bila makala yake kufungiwa au yeye mwenyewe kupata matatizo.

Hivyo, weledi wa Mayalla unakuja kwenye kutumia lugha ya picha na kurembesha. Anampaka kiongozi 'mafuta kwa mgongo wa chupa' kwa kumwita 'mkali' na kumfananisha na Nyerere, lakini kiuhalisia anamtega. Ni kama anajenga hoja kwamba: 'Kwa kuwa wewe ni mkali kama Nyerere, na kwa kuwa unataka nchi moja, basi thibitisha ukali huo kwa kuwawajibisha waliofanya madudu Oktoba 29.'
Hata hivyo, kama ulivyofafanua mkuu, mtego huo wa Mayalla unajigonga wenyewe na kupoteza uhalali mbele ya msomaji anayejua ukweli wa mambo. Huwezi kumtaka kiongozi awajibishe mfumo ambao yeye mwenyewe ndio msimamizi na mnufaika mkuu wa matokeo yake. Kutumia kisingizio cha 'ukali' au 'ndoto ya serikali moja' ili kusafisha au kutenganisha mamlaka na matukio ya ukandamizaji ni kujidanganya.

Shukrani kwa kuondoa upofu huu wa kalamu ambao mimi na Tindo tulikuwa tumeingia!
NB: Kwa diplomasia hii ya kisomi ya kujipendekeza kwa gia ya falsafa na historia badala ya kelele za kawaida, basi Paschal Mayalla anastahili kabisa kutunukiwa cheo cha "Luteni Jenerali wa Propaganda" kwenye lile Jeshi la Machawa linaloongozwa na Jenerali Lucas Habel Mwashambwa!
 
Mr. Mayalla ni badluck person..
Kuna namna alishindwa kua mla National cake.
Sasa ana force king.
Namfananishaga na Tom cat.
 
Nianze na jambo dogo kuhusu hii makala ya Mheshimiwa Paschal Mayalla. Kwanza niseme wazi, bila kumung'unya maneno. Unasoma karibu 50% ya mwanzo wa makala hiyo huku unajiuliza hii ni makala kuhusu Paschal Mayalla mwenyewe au Nyerere? Hilo tuliache.
Mkuu Synthesizer, kwanza asante sana kuisoma makala yangu na kuianzishia thread, nimeitembelea kule, imekula hits za kutosha. Sisi waandishi wa habari wa magazeti, ukiisha andika, ndio umemaliza, hujui kama kuna mtu amesoma au ni umejiandikia tuu, hivyo kitendo cha mtu mmoja kusoma na kuchambua, ni faraja kubwa kwangu, thanks kwa kunisoma, japo hukunielewa, hivyo nitakwenda na wewe mdogo mdogo hadi ama utaelewa, ama mzito kuelewa na mwisho wa siku, tutafikia mahali, ama tukubaliane, ama tusikubaliane hivyo kufikia kukubaliana kutokubaliana.

P.
 
Mkuu Paschal Mayalla,
Nimesoma majibu yako kwa mkuu wetu Synthesizer pale uliposema "twende mdogo mdogo" hadi muelewane. Kwanza nikupongeze kwa ukomavu wa kukubali mjadala bila povu, hiyo ndio sifa ya waandishi wakongwe. Lakini kwa niaba ya Synthesizer na sisi wasomaji wengine tuliomuelewa yeye na tukashindwa kukuelewa wewe, naomba nikuweke sawa kwenye maeneo machache kishabiki na kimantiki.
Mkuu wangu, unajitetea kuhusu ule muundo wa makala yako, lakini ukweli unabaki palepale: Makala ilitangazwa kuwa ni ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (Nyerere Day), lakini karibu asilimia 50 ya mwanzo ulikuwa unajieleza wewe binafsi, ulivyosoma, ulivyokuwa mwandishi, na ulivyokutana naye. Wasomaji tulibaki tunajiuliza kweli hii ni siku ya kumkumbuka Nyerere au ni siku ya Paschal Mayalla? Hilo sawa, Synthesizer alisema tuliache, nami naliacha. Tuje kwenye hoja zenyewe.
Kwenye hoja ya "ukali," hapo ndipo ulipoangusha kalamu yako mkuu Paschal. Unajaribu kulazimisha ulinganifu kati ya mifumo ya sasa na ya Mwalimu Nyerere. Ukali wa Nyerere ulikuwa na misingi na itikadi inayoeleweka—ulilenga kupiga vita rushwa kwa vitendo, kulinda rasilimali za wanyonge, na kubana viongozi wasijitajirishe kupitia madaraka yao (Azimio la Arusha).
Sasa hivi tunaposifu "ukali" wa utawala wa sasa, tunasifu ukali upi hasa wakati jamii inalalamika kuhusu matukio ya utekaji, kuminywa kwa sauti za wakosoaji, na rasilimali za nchi kugawiwa hovyo? Nyerere hakuwahi kuwa mkali ili kulinda kiti chake cha enzi au kuwatishia raia wake, alikuwa mkali kulinda utu wa Mtanzania. Hapo umemvisha Rais wa sasa koti la Nyerere linalompwaya mno.
Kwenye suala la Muungano, mkuu wangu hapo ndio kabisa umeamua kupiga ramli ya kisheria. Wewe ni msomi wa sheria, unajua kabisa kuwa uwepo wa Rais kutoka Zanzibar haujasogeza nchi hatua mbele kuelekea "serikali moja" kama unavyodai. Kinyume chake, kikatiba na kiuhalisia, Zanzibar inazidi kujipambanua kama nchi huru kamili yenye bendera yake, wimbo wake, na mamlaka kamili ya ndani, huku huku upande wetu wa Tanzania Bara ukiachwa njiapanda bila sauti wala mamlaka ya kulinda rasilimali zake. Sasa hiyo serikali moja unayoiona wewe ipo wapi?
Ukweli ni kwamba, Synthesizer alikuwa sahihi kabisa kukutolea ule uchambuzi, na sisi wasomaji tumeelewa mbinu yako. Makala yako imejaa uandishi wa kujilinda—kile kinachoitwa calculated sycophancy. Unajua fika mazingira ya sasa ya kisiasa yalivyo; unajua ukiandika ukweli mtupu bila kuupaka mafuta kwa mgongo wa chupa, kalamu yako inaweza kuingia matatani. Ukajidai kumsifu Rais na kumlinganisha na Nyerere ili tu kulinda usalama wako kwanza, kisha ukapitisha ujumbe wako kiulaini.
Wasomaji wa leo tunasoma hadi alama za uandishi mkuu wangu, hatuangalii maneno ya juu pekee. Swali la kumalizia kwa niaba ya Synthesizer na sisi wenzake tunaoanza hii safari ya kwenda na wewe mdogo mdogo: Hivi mkuu Paschal, unaiandikia Tanzania hii halisi tunayoishi na kuishuhudia kila siku, au unaiandikia Tanzania ya kufikirika iliyojaa sifa ili mradi tu usalama wa kalamu yako uwepo?
Kilinge kiko wazi mkuu, tunasubiri raundi inayofuata!

Mtani wako Kijana wa Ifoza
mvuvi kutoka Lumemo katika Kimero cha Mto Kilombero
 
Miaka 50+ kwenye siasa na uchawa na bado hajawahi kulamba hata ugoro!, unategemea aandike Nini?. Mayalla angekuwa shoger huyo angekuwa kwenye level za kina Juma lokole.... Mayalla ni mmoja ya waandishi wa habari wajingawajinga na ambao anayependa kuteuliwa ila hana hiyo bahata.... Matokeo yake anawaza kutumia mataqo yake.
Hapana. Usimtusi aisee.Mayalla ana mazuri yake pia ameifanyia nchi huko nyuma. Japo sasa hivi anakengeuka sana.
 
Nianze na jambo dogo kuhusu hii makala ya Mheshimiwa Paschal Mayalla. Kwanza niseme wazi, bila kumung'unya maneno. Unasoma karibu 50% ya mwanzo wa makala hiyo huku unajiuliza hii ni makala kuhusu Paschal Mayalla mwenyewe au Nyerere? Hilo tuliache.

Tuje umalizio wa makala yenyewe. Hapo ndipo Mkuu Mayalla amelikoroga kabisa. Anadiriki kumsema Samia ni mkali kama Nyerere; really Mayalla? Samia ni mkali katika mambo gani kama Nyerere? Kushughulika na wapinzani? Kuiteteta Katiba na utawala wa sheria? Kuchukia rushwa? Kutotumia nafasi yake kujitajirisha? Kuwa mdini katika teuzi? Kutumia madaraka yake kupendelea upande wa Zanzibar? Kudhoofisha muungano kwa kuwaruhusu Zanzibar wafanye mambo ambayo yako ndani ya muungano?

Hivi unawezaje hata kuwa na wazo la kulinganisha ukali wa Nyerere na Samia? Labda ni wakali kweli, lakini basi ulipaswa kusema ni wakali katika completely opposite directions - kwa mfano, kwamba Nyerere alichukia sana rushwa, na Samia anachukia sana anapoambiwa analea wala rushwa (mafisadi) nchini! Nyerere aliitetea katiba kwa nguvu zote na Samia anaibeza katiba kwa nguvu zake zote! Fikiria maneno ya Samia juu ya katiba - kijitabu tu; angethubutu kuyasema Nyerere akiwa hai? Siku hiyo ndio ingekuwa mwisho wa uraisi wake!

Kitendo cha Paschall kumweka Samia na Nyerere katika skeli ya ukali ni kuchafua kumbukumbu ya baba yako ambae alikuwa victim wa ukali wa Nyerere akiwa polisi!

Nyerere angeamua kutumia watoto wake kujitajirisha, basi leo hao kina Mako wangekuwa wanaishi kama masultan wakinukia utajiri! Nasi asiejua utajiri wa Dula umekuja baada ya mama yake kuwa raisi? Samia anakuwa raisi kwa miaka mitano, Dula anakuwa tajiri mmoja wapo mkubwa Tanzania. Nyerere anakuwa raisi kwa miaka 23, watoto wake bado wanaishi kwa mishahara na pension. Halafu unadiriki kumlinganisha Samia na Nyerere wakati wa kumbukumbu ya Nyerere? Kwa nini usitafute kebehi ya aina nyingine?

Haya, tuje kwenye tukio la Ockoba 29. Kwa masikitiko makubwa sana, Mayalla anadiriki kusema "Kilichotokea Oktoba 29, ni kikubwa kuliko kilichotokea mwaka 1976, hivyo hii ni fursa kwa Raisi Samia kumuenzi Mwalimu Nyerere kwa kumuishi". Haya ni matusi kwa Nyerere!!!!

Hivi Paschal, ina maana alietoa maelekezo ya Polisi kutumia risasi dhidi ya waandamaji ni nani, sio Samia? Alieona askari wa bara wanaweza wasitii amri ya kuua hivyo waletwe askari toka Zanzibar ni nani, sio Samia? Aliewasifia Polisi kufanya kazi nzuri kwa kuua waandamanaji ni nani, sio Samia? Aliekebehi waliofiwa kwa tukio la Oktoba 29 kwamba kwa nini wasiwazuie watoto wao kutoka ni nani, sio Samia? Sasa leo hii, Mayalla unadiriki kusema Samia atumie Oktoba 29 kumuishi Nyerere, hivi uko sawa kweli? Kwamba Raisi Samia afanyeje, amwambie DPP amfungulie mashitaka ili Samia apelekwe mahakamani kwa tukio la Oktoba 29?

Kwa kweli hapa Mayalla umenisikitisha sana. Umejiharibia sana heshima yako ya uandishi wa habari.

Hapo chini ni Makala Ya Pascal Mayalla

Jumatano ya leo Oktoba 14 ni siku ya bahati, imeangukia Nyerere Day, hivyo naomba tutafakari jinsi sisi Watanzania, viongozi wetu na Mtanzania mmoja mmoja tunavyomuenzi Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere. Je, tunamuenzi kweli kwa mawazo, maneno na matendo? Je, viongozi wetu wanamuishi?

Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere sio tu alikuwa ni mwasisi wa CCM, mpaka kifo chake aliiamini CCM, hivyo hata baada ya Tanzania kuingia kwenye mfumo wa vyama vingi vya siasa mwaka 1992, bado aliamini kuwa wapinzani wanaweza kuleta wabunge bora, na hili tumelishuhudia kwa baadhi ya wabunge wa upinzani, walikuwa ni wabunge bora kabisa, lakini kwenye urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mwalimu Nyerere aliamini: “Rais bora atatoka CCM pekee”.

Je, kwa hali ya siasa zetu za Gen Z, huu mtazamo wa Mwalimu Nyerere bado unaishi nchini mwetu au kuna siku upinzani unaweza kuja kushika nchi?

Nilivyomfahamu Nyerere

Nimezaliwa mwishoni mwa miaka ya 1960, hivyo tangu nimepata akili za kujitambua, nimesoma shule ya msingi na sekondari enzi za Rais Nyerere, na kumuona kwenye magazeti na kumsikiliza kwenye redio.

Nimeishuhudia kwa macho CCM ikizaliwa. Ile kauli ya kila lenye mwanzo...Mwaka 1977 wakati CCM inazaliwa, nilikuwa darasa la tatu. Ule msemo wa kila lenye mwanzo lina mwisho, sio msemo wa ukweli, ni uongo, sio kila lenye mwanzo lina mwisho, mfano hai ni CCM ina mwanzo tu.

Nilimuona Nyerere kwa mara ya kwanza mwaka 1978, baada ya kuja kuishi jijini Dar es Salaam kwenye familia ya baba yangu mdogo, Mzee Mathew Kasanga, eneo la Drive In, kanisa letu ni St. Peters, hivyo siku ya kwanza napelekwa kanisani, ndio mara ya kwanza kumuona Mwalimu Nyerere, alikuwa anasali pale.

Wakati wa kutoka nikaona watu wanatoka kanisani haraka na kupanga foleni pale nje kwenye ngazi kumsubiri Nyerere atoke. Alipotoka akawa anawasalimia watu kwa kuwashika mkono. Jumapili iliyofuata na mimi nikapanga foleni, nikasalimiwa kwa kushikwa mkono na Nyerere. Nilifurahi sana, nikataka nisinawe ili nisifute ule mkono wa Nyerere.

Baadaye, nikawa mtumishi wa kanisa, nikawa naomba kupangiwa misa ya kwanza, hivyo nikawa namhudumia Mwalimu Nyerere kwa kumshikia kisahani cha hostia, na ndipo pia nikayaona meno yake kwa karibu na kuijua maana ya jina la Mchonga.

Tangu hapo nikawa namfuatilia sana, ile hotuba yake ya kutangaza vita, nikaikariri baadhi ya maneno na kumuiga: “Uwezo wa kumpiga tunao, sababu ya kumpiga tunayo, nia ya kumpiga tunayo. Tutampiga Amin.”

Mwaka 1979 kwenye mapokezi ya mashujaa wetu pale Uwanja wa Taifa, nilikuwepo na kumshuhudia Mwalimu machozi yakimtoka kutokana na lile tukio.

Baada ya kumaliza shule ya msingi, familia ya Mzee Kasanga ikahamia Mikocheni, opposite na Msasani kwa Nyerere, mimi nikajiunga sekondari ya Tambaza, tulikuwa darasa moja na mmoja wa watoto wa Msasani kwa Nyerere, akiishi hapo Msasani, sasa kwa Nyerere, tukawa tunakwenda kucheza.

Baada ya Tambaza nikaenda Ilboru Arusha, nikapelekwa nyumbani kwa Makongoro Nyerere, enzi hizi Mako ni mjeshi. Nilipelekwa pale na Rastafarian mmoja, mdada wa Kijamaica aliyelowea Tanzania akiitwa Gipsy, tukatokea kupatana sana na Mako, maana ndege wafafanao huruka pamoja. Siku za weekend ni usawa wa Cave, kiukweli sijui alikuwa anarudi nyumbani saa ngapi.

Baada ya sekondari nikajiunga na Chuo cha Uandishi Habari (TSJ), ndipo Jumapili moja asubuhi, nikafuatwa jamaa fulani mweupe, ana bonge la afro na gari sports car nyekundu na kujitambulisha “mimi ni Madaraka Nyerere, mtoto wa Nyerere, unahitajika Msasani kwa Nyerere.”

Niliitikia wito na kutakiwa kuwa MC kwenye harusi ya Binti wa Nyerere. Hapo ndiyo mara yangu ya kwanza kuwa karibu na Nyerere.

Baada ya kuhitimu TSJ, niliajiriwa Redio Tanzania Dar es Salaam (RTD), kufuatia kazi ya uandishi nikawa napangiwa matukio ya Nyerere, na baada ya kung’atuka, safari yake ya mwisho kabla hajaanza kuumwa, ilikuwa ni Bern nchini Uswisi, nilisafiri naye na kumfanyia mahojiano.

Baada ya kurejea nchini, ndipo alianza kuugua, mimi ni miongoni mwa waandishi wa habari tulioandamana na Rais Mkapa kumtembelea Mwalimu katika Hospitali ya St. Thomas, Uingereza na baada ya kufariki, mimi ni mmoja wa tuliomsindikiza mpaka kwenye makao yake ya milele, Mwitongo, Butiama.

Kwa upande wa viongozi wetu, aliyemuenzi Nyerere kwa vitendo ni Rais wa awamu ya tano, John Magufuli kwa kuichukia rushwa, serikali kuhamia Dodoma na kufua umeme wa Bwawa la Stigler Gorge, sasa ukijulikana kama JNHPP.

Rais Samia ana fursa adimu na adhimu mbili za kumuenzi Mwalimu Nyerere. Kwanza, ni kwa kuwa mkali kama Nyerere kwa kilichotokea Oktoba 29, 2025 kwa kuwachukulia hatua kali, kama Nyerere alizochukua mwaka 1976 baada ya kutokea vifo vya mahabusu wanne mikononi mwa polisi.

Aliifumua kuanzia juu kwa makamu wa pili wa rais, Rashidi Kawawa kuondolewa, mawaziri wa mambo ya ndani, Ali Hassan Mwinyi na Waziri wa Usalama, Peter Siovelwa walilazimishwa kujiuzulu. IGP Samue Pundugu na Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa (DGIS), Emelio Mzena, walistaafishwa kwa manufaa ya umma, wakuu wa mikoa ya Mwanza na Shinyanga, Peter Kisumo na Marko Mabawa walitenguliwa, kisha RPC,RSO, OCD na DSOs wa Mwanza na Shinyanga walipandishwa kizimbani kwa kesi ya mauaji Mwanza na Shinyanga.

Kilichotokea Oktoba 29, ni kikubwa kuliko kilichotokea mwaka 1976, hivyo hii ni fursa kwa Rais Samia kumuenzi Mwalimu Nyerere kwa kumuishi.

Pili, ni kupitia Katiba mpya, falsafa ya Nyerere ilikuwa ni serikali mbili, kuelekea serikali moja, hivyo Tanzania kuwa nchi moja, serikali moja na rais mmoja. Kwa mujibu wa mwelekeo wa siasa zetu, ndoto ya Mwalimu ya kuwa nchi moja na serikali moja, inaweza kutimia tu kipindi ambacho rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anatoka Zanzibar.

Pumzika Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, mwendo uliumaliza, imani uliilinda.

Tutaendelea kukukumbuka daima dumu.
Pascal Mayalla is either a willing spinner or a "useful idiot" to Samia and CCM.

I told him this.

Either way, it looks terrible.
 
Bro Pascal Mayalla a debate challenge..
 
Makala ndeeefu.... kumjibu Mayalla anayetafuta jinsi ya kutia mkono kinywani kwenye awamu hii. Kumfananisha Samia na Nyerere ni kumkufuru hayati. Kukufuru ni uhaini pia.
 
Pascal Mayalla is either a willing spinner or a "useful idiot" to Samia and CCM.

I told him this.

Either way, it looks terrible.
Mkuu Kiranga , to be honest, sasa nimefurahishwa na hii "useful idiot" ya kwenye post hii, kwasababu its not definite, ile either or ndio the little civility I was asking for. Tnank you for this!.

Mimi ni muumini wa ile concept ya "Me and I ", me ni jinsi mtu anavyoonekana alivyo, na anavyochukuliwa na the society, jinsi anavyoonekana, and I, ni the real you vs the purported you.

Hivyo mimi ninavyojijua mimi, I'm neither a willing spinner or a "useful idiot"

a willing spinner ni machawa na uchawa, mimi sio chawa, sifanyi spinning humu, ila kosa langu kubwa humu, ni kuwa mkweli, kuwaeleza watu ukweli mchungu bila kumumunya wala kutafuna maneno. mfano mzuri ni urais wa Samia post 29th October, nimeeleza humu, baada ya uchaguzi batilifu, uliendeshwa na INEC batilifu, na kikafanyika kilichofanyika ikiwemo kuzipiga kura za wale majinga wote ambao walijiandikisha kupiga kura lakini siku ya kupiga kura, hawakujitokeza, hivyo to make room kura zao kupigiwa, na yakatangazwa matokeo batilifu, nikaeleza watu humu, Tangazo hilo la INEC kumtangaza mshindi ndio the final and conclusive kuhusu uchaguzi wetu!, no ene can do anything unless YEYE aamue vinginevyo!. Na nikaeleza kitendo cha kuapishwa ni kuhalalisha kila kilichofanyika kwa kanuni ya "the end justifies the means", hivyo Rais Samia ni rais halili kikatiba na kisheria ila sio rais wa haki, kwasababu haki na sheria ni vitu viwili tofauti. Hivyo kitendo na kutoa facts kama hii, kunanifanya nihesabike as a "useful idiot", then be it!.

Kwa vile najua watu wenye uwezo to read in between the lines humu jukwaani wanahesabika, and I know, wewe you are one among them, hivyo nitakupitisha kwenye baadhi ya hoja zangu, kisha nikupe uhuru wa kuzi label kama a willing spinner or a "useful idiot", na ukikuta I'm not, nitakuomba umeze kauli zako kwa kunifahamu my I, besides Me.

Hii hoja ya bandiko hili, nimeijibu kwake https://www.jamiiforums.com/threads...u-simwelewi-kabisa-critical-analysis.2482371/, lakini naitafutia muda tumalizane.

P
 
You are a proper useful idiot then.
 
Back
Top Bottom