Katika hotuba moja ya mheshimiwa Rais Dr. Samia Suluhu Hassan alifunguka kutoka moyoni jinsi anavyokubali hoja kutoka upinzani.
Ni matumaini yetu makubwa mheshimiwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mwenyekiti wa CCM Taifa, mawasilisho haya ya CHADEMA mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge atayafanyia kazi kubadilisha miswada hii. Kwani wasilisho la CHADEMA linakwenda sawia na zile
4R , sheria za haki na katiba mpya inayokubalika kuwa ni ya usawa kwa wote bila kujali vyama.
Toka Maktaba :
17 Feb 2020
Samia Suluhu : "Napenda mawazo ya wapinzani, huwa wanajenga hoja vizuri, walini 'inspire' niingie siasa"
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amefunguka kuhusiana na historia ya maisha yake ambapo ameeleza siri ya mafanikio na chanzo kilichomvutia kuingia kwenye siasa. Samia Suluhu anaona hoja za upinzani ni moto, zimejaa mantiki kuliko za mawaziri wa serikali ya CCM , hivyo walinivutia / inspire, mimi ni activist ... kuingia siasani baada ya kuona majibu na hoja za upande wetu (CCM) hazina uhalisia na hazijibu maswali ya wananchi ....
View: https://m.youtube.com/watch?v=gb3MPZNXdt4