mrangi
JF-Expert Member
- Feb 19, 2014
- 88,759
- 123,368
Engineer huyo mwenye degree hata kushika drill au grinder hawezi kuitumiaWatu hawaoni hoja yako, wamekariri VETA.! Sasa kama Veta i mworabaini kuna sababu gani ya kuwa na Vyuo vya Kati na Vyuo vikuu? Yaani Engineer aende VETA kufundishwa na Fundi Mchundo!
Kazi ya Engineer si kuchomea (welding) au kufungua bolts and nuts, kazi ya Engineer ni nyingi ikiwemo ku design na kusimamia. Halafu hawataki kujibu hoja ya kwamba kwanini graduate wa SUA asipewe mkopo wa Trekta eti aende Veta! kuna ujuzi gani wa Kilimo VETA ambao SUA haupo!
Sina uhakika kama Waziri Mkuu alishauriwa vema kabla hajasema. VETA ilianzishwa kwasababu ya kupata Watalaam wa kada ya kati na ambao hawakuweza kupata nafasi za kuendelea na masomo.
Wahitimu wa ''University' wakifurika VETA, huyu wa Form 4 au 6 hatapata nafasi tena kwasababu wa Chuo kikuu atakuwa bora huko VETA! Je hapo watakuwa wame solve tatizo la ajira?
JokaKuu
Ova