Nimestushwa na Kauli ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Je ni kufilisika ki Maono kwa CCM?

Nimestushwa na Kauli ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Je ni kufilisika ki Maono kwa CCM?

Wanataka nesi nae aende kujifunza Rejeta inavofanya kazi, kumwaga injini oil
Aisee
Wee acha tu! maana inachekesha sana. Mbaya zaidi kauli ya PM ina wapiga debe! hawaoni wala kusikia

Kwamba, Nurse yupo VETA anajifunza kumwaga Oil
Journalist yupo VETA anajifunza kufungua rejeta za magari
Vertenary Officer na BVM yake kutoka SUA yupo VETA anapata ujuzi wa kushika grinder!
Mtaalamu wa Geology kutoka UDSM anapata ujuzi wa kufunga AC za Magari pale VETA
CPA naye yupo VETA anapata ujuzi wa kulisha ng'ombe kwa mashudu

Dah!
 
nadhani hizo ni hulka na tabia za wavivu tu kuchukizwa na kughadhabishwa, hasa baada ya kuelezwa ukweli mtupu tena wenye manufaa binafsi ambayo ni wazi yanaweza kuwaondoa graduates wengi katika unyonge wa kiuchumi walionao,
na kuondokana na uzururaji usio koma wa kusaka ajira mijini ambazo pia ni chache ukilinganisha na wingi wao.

Ni wazi,
watakaozingatia mawaidha hayo mujarabu sana ya waziri mkuu, watanufaika kibinafsi na familia zao huku wavivu na washupaza shingo kama PhD holder wa mchongo na mtoa hoja wakikodoa macho na kushangaa graduates walioenda veta wakitusua maisha.

Tz kua maskini au tajiri ni uamuzi binafsi wa mtu 🐒
Itoshe kusema huna akil unazani ikatokea wanaomaliza lasaba, form four, nawale wachuo wote waende veta mitaa c itajaa mafundi nakaz hazitawatosha
 
Hoja yako ni kwamba waende VETA. Sasa ujuzi gani wataupata huko VETA?

Kumbuka, hoja ni kauli ya Waziri Mkuu kwamba waende VETA na wewe ukasema yupo sahihi.
Ninakuuliza, Daktari na Nurse wanakwenda VETA kupata ujuzi gani?
Veta wakasomee welding au kupika keki kama ni daktari na hauajiriki kwa nini usitafute ujuzi wa kukuingizia kipato? Wapi uelewi?
Majaliwa yupo sahihi kabisa.
 
Toa Ushauri , tufunge vyuo?
Serikali itengeneze mazingira mazuri watu wajingize kwenye kilimo,ardhi ipo ya kutosha
Syo kila mtu atake kubanana mjini
Kwenye kilimo bado kuna fursa kubwa sana ,na dunia bado inahitaji chakula

Ova
 
Veta wakasomee welding au kupika keki kama ni daktari na hauajiriki kwa nini usitafute ujuzi wa kukuingizia kipato? Wapi uelewi?
Majaliwa yupo sahihi kabisa.
Hata kupaka rangi mtu kasomq civil engineer hawezi

Ova
 
Toa Ushauri , tufunge vyuo?
Ndomana nasema elimu yetu imekosewa mahali
Zamani tulikuwa na chuo cha sukari
Tulikuwa na chuo cha tanesco
Tulikuwa na chuo cha reli
Kuna chuo cha bandari
Huoni kama tulikuwa tunaenda vzr
Na walikuwa wanazalisha watu

Ova
 
Na amejaza vyeti ndani GPA Upper second. Si bora awe tu dalali au shoe shiner maana uinjinia umemshinda.
Waliyosoma veta hao hao ndy wana workshops za kutengeneza mageti, madirisha ya vyuma nk
Mafundi aluminium nk
Hao wenye degree wanashindwa kujiongeza wanasubiria ajira serikali

Ova
 
Wee acha tu! maana inachekesha sana. Mbaya zaidi kauli ya PM ina wapiga debe! hawaoni wala kusikia

Kwamba, Nurse yupo VETA anajifunza kumwaga Oil
Journalist yupo VETA anajifunza kufungua rejeta za magari
Vertenary Officer na BVM yake kutoka SUA yupo VETA anapata ujuzi wa kushika grinder!
Mtaalamu wa Geology kutoka UDSM anapata ujuzi wa kufunga AC za Magari pale VETA
CPA naye yupo VETA anapata ujuzi wa kulisha ng'ombe kwa mashudu

Dah!
Wakati nipo chuoni nilitumia laptop yangu na bundle la bure kujifunza online namna ya kutengeneza graphics. Baadae nikajifinza digital marketing. Nilianza kutengeneza pesa nikiwa mwaka wa pili, chuoni kunikuta na laki 5 mfukoni ilikuwa jambo la kawaida. Na nikiwa mwaka wa 3 ilitangazwa kazi na kampuni moja nikaomba wakaniita interview japo sikuwa na experience nikajieleza nikawaonesha kazi zangu jamaa wakanichukua nikiwa bado mwanafunzi nikawa nasoma huku nafanya kazi. Kwenye interview nilikutana na watu wameshamaliza chuo wapo mtaani wanasaka ajira na wamesomea marketing wengine communication ila nikachukuliwa mimi. Kwa sababu dunia ipo kwenye ujuzi haipo tena kwenye vyeti.
Veta ni traditional lakini kuna online platform kibao za kujifunza ujuzi.

Tuwaambie vijana ukweli serikali haiwezi kuajiri wala kutoa mikopo kwa graduates laki 8. Waende veta wakaapte ujuzi.
 
Waliyosoma veta hao hao ndy wana workshops za kutengeneza mageti, madirisha ya vyuma nk
Mafundi aluminium nk
Hao wenye degree wanashindwa kujiongeza wanasubiria ajira serikali

Ova
Wanasema serikali iwape mikopo. Kwanza ni risk kumpa mkopo mtu asiyejua hata mtaa unataka nini yeye akili yake ni kuwa boss. Alafu mikopo watapewa wakafanyie nini hata ujuzi hawana.
 
Kauli ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuhusu vijana wenye degree kwenda Veta ikiwa ni sehemu ya kukabiliana na changamoto ya Ajira ni kauli ya kukosa maono na ni red sign kuwa CCM ni MUFILISI......

Ni kitu cha ajabu sana kumsikia kiongozi wa Serikali kuwaambia vijana mjiajiri wakati yeye carear path yake yote imeanzia kwenye kuajiriwa from his age of 27 to the age of 60 or so....na wengine hadi kwenye miaka 80 wanapambana na ajira........ what a shame!

Nilitegemea top management ya nchi mkae chini na muje na evidence based decision on how to handle the matter na sio kutanua goli.

Kama kujiajiri ni rahisi mbona nyie mpo kwenye ajira kwenye 80 ?

Kwa mfano, huku majuu ajira sio big issue....haina maana kuwa watu ni SMART, ni serikali imeweka mazingira rafiki...,Nesi, Daktari , maabara na Famasia waliomaliza degree yao wanaweza kuandaa proposal yao na Serikali ikatoa 300M na watu wakafungua Hospital with minimum interest .

Engineers, Architect and all that, wanafungua kampuni they get gvt loan fund with minimal interest ... hizo kampuni za construction ndio hao wanajenga barabara, buildings na gvt inawapa tenders..... hao watu pia wanaajiri na wengine .... that is why majuu kuajiriwa na gvt sio kitu muhimu.

Kampuni ya Straberg iliyojenga zile mwendokasi za mwanzo ilianzishwa na degree holder 2 waliopata gvt loan. Hizi ndio Strategies viongozi mkae chini mje na solutions , vijana sio wajinga.....ni nyie hamna weledi na maono ya nini cha kufanya…..resources mnazouza zinamnufaisha MTZ?

Barabara za TZ unakutana na wachina, nyie mmeshindwa kuandaa vijana wenu kufanya hizo kazi ?

Kujenga barabara nazo we need Mchina...Karine ya 21 . what a shame ?hivyo vyuo vinakazi gani ?

Mchina anauza maji hadi KKO, yaani mtu katoka chini kuja kuuza maji TZ halafu mnajiita viongozi

mtu kasomeshwa na bodi ya mikopo kamaliza shule halafu unamwambia kajiajiri..... are we mad ? At the same token mtu wa 80 yupo kwa ajira ! Experience my foot ..... nini ambacho anakifanya kijana wa 35 hawezi kukifanya....?

Acheni hizo mambo na kulewa madaraka ....lets be real ....kujiajiri kuna hitaji START UP, nyie kama viongozi kaeni chini mje na mikakati ya kuwasaidia vijana na sio kuwaambia waende Veta , huo ni UCHAWI maana hata Veta Itajaa.

Kuna vile vimikopo vya 3M 🤣TAMISEMI.....huwa hata inawafikia walengwa... ? si wanakula kina Mchengerwa na kuongeza wake.....

Dr Megalodon Mushi, PhD candidate
WHO Regional Office
Rue 52, Ottawa
Canada
😅😅😅
 
Wakati nipo chuoni nilitumia laptop yangu na bundle la bure kujifunza online namna ya kutengeneza graphics. Baadae nikajifinza digital marketing. Nilianza kutengeneza pesa nikiwa mwaka wa pili, chuoni kunikuta na laki 5 mfukoni ilikuwa jambo la kawaida. Na nikiwa mwaka wa 3 ilitangazwa kazi na kampuni moja nikaomba wakaniita interview japo sikuwa na experience nikajieleza nikawaonesha kazi zangu jamaa wakanichukua nikiwa bado mwanafunzi nikawa nasoma huku nafanya kazi. Kwenye interview nilikutana na watu wameshamaliza chuo wapo mtaani wanasaka ajira na wamesomea marketing wengine communication ila nikachukuliwa mimi. Kwa sababu dunia ipo kwenye ujuzi haipo tena kwenye vyeti.
Veta ni traditional lakini kuna online platform kibao za kujifunza ujuzi.

Tuwaambie vijana ukweli serikali haiwezi kuajiri wala kutoa mikopo kwa graduates laki 8. Waende veta wakaapte ujuzi.
Well and congrats.
 
🤣 endelea kusema anaupiga mwingi

Give them sweets take them Gold

Utakuja kuelewa wakati ajira yako ya uchawa imeisha na una watoto wanadegree upo nao ndani

Uliowategemea wakupe connection hawapo Tena

Haya mamasamia mitano tena
Machawa wengi wamejificha humu. Wanategemea sana connection kuliko uwezo na ujizi
 
Mimi ninakubalina na PM
1. Dunia ya sasa inahitaji ujuzi (skills) na huo unaweza kuupata VETA ama katika Technical Colleges ila haimaanishi ukienda Veta baada ya kumaliza Degree ile Degree yako inakuwa haina kazi la hasha, VETA inakuongezea skills apart from your Prossionalism.

2. Hii ni kudhihirisha kwamba mtaala wa elimu yetu hauwasaidii vijana wengi na ndio maana wanashindwa kujiajiri. Kuna haja ya kufanya reform kwenye elimu yetu ili iweze kuwasaidia vijana wa kitanzania.

3. Umesema wachina wengi wanafanya kazi ambazo vijana wetu wangeweza kufanya, lakini ninaamini hao wachina wana degrees ama diploma kutoka katika vyuo vyao ila hawajasubiri kuajiriwa na ndio maana wanauza mahindi kkoo
 
Kauli ya PM ni yake binafsi kama Majaliwa sio kauli rasmi ya serikali. Mimi pia siungi mkono kauli yake.
Angeitoa kama kauli ya serikali angesemaje? Ni wakati gani kauli inayotolewa na waziri mkuu inakuwa ni yake binafsi na ni wakati gani inakuwa ya serikali? Tuna tatizo kubwa la kupeana nafasi za uongozi kama fadhila pasipokuzingatia uwezo na taaluma ya wahusika. Vyuo vyetu vinatoa taaluma ya utawala/uongozi wa umma (public administration) katika ngazi mbalimbali. Ni nadra kuwaona wahitimu wa fani hiyo katika nafasi za uongozi, badala yake wamejazana watoto wa wajomba na wanaoitwa chawa. Kwa nchi ilipofikia anahitajika Traore, hata kama itatugharimu kumpata
 
Back
Top Bottom