Nimetapeliwa zaidi ya Tsh. 45,000,000 kwa kuuziwa kiwanja feki

True jini anakupa utajiri nawe unampa jini kafara ya damu.
Damu ni chakula cha majini.
Waganga na wachawi ni matajiri Sana wa pesa lakini masharti yao hayawaruhusu kumiliki mali.Pesa zao wanazitumia kununua vifaa vyao vya Kazi
 
hujatapeliwa umebondwa na chuma kizito.
unakua ngangari kuitafuta hela ila kupoteza sasa mzembe.
hao wenzio mliotapeliwa wote walijiandaa kukupa uenyekiti wa kijiji sahii wanakuona boya mwenzao tu.
 
Hata mm hapa nais nimepigwa mnk nilinunua eneo la shamba huko mbeya bila kumshirikisha mke wa jamaa aliyeniuuzia Happ kwa kweli nimekozea nimewashirkisha wajomba zake na mwenyekit wa kijij tu bila kwenda offisini eeh mungu wangu nimemwaga pesa zangu buree duh

Ngao popote nakutafuta
 
Haya mambo yasikie tu.

Nina siku ya nne leo tangu nigundue kwamba nimepigwa, hata kula vizuri siwezi, nawaonea wivu wenzangu walionunua maeneo madogo kwa bei za 15m kushuka chini. Naona hasara yao ni ndogo kuliko yangu.
Bwana Mangushi,
Nakupa Pole sana,
Watu hao ni Walaghai eeee,
Wanaitwa Matapeli eeee,

Watu hao wameenea sana, kila pembe hapa mjini, kazi yao ni kuibia watu, jina lao matapeli.
 
Hapana mkuu usikate tamaa, hiyo werevu ndio huwa wanakugeuka ila kwa Mbeya kule ni mfumo dume zaidi hivyo mara nyingi mama anakua ameridhia. Ila kaa ukipiga maombi sana wasivurugane halafu waachane na mama apate wakili mwerevu utajua kwa kupata hela yako😂😂😂😂😂😂. Hii hufanyika zaidi katika mali za ndoa/zilizochumwa pamoja.

Ila kaa kwa machale hiyo ni voidable contract
 

Wakili wako anawajibu wakufuatilia taarifa zote kuhusu hiyo aridhi kabla ya mauziano,kwa hiyo lazima ajue background ya hiyo ardhi,mana hata sheria inambana mnunuzi kabla hujanunua aridhi hakikisha una taarifa sahihi vinginevyo utalia na kusaga meno huko mbele.
 

Wakivurugana lazima aite maji mma hapo Land Act na The Village land act pamoja na Law of marriage Act lazima imsulubishe[emoji23][emoji23][emoji23]
 
- mwenye masikio na asikie
-Wenyeviti wa serikali za mitaa hawaruhusiwi kujihusisha na Ardhi ya jumla (general Land) hata Waziri wa ardhi (Mhe.Lukuvi Kama alivyokuwa Waziri wa ardhi) alikuwa anawapiga marufuku
- Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa sio mtaalam wa Ardhi, Wakili atakuongoza kwenye kufanya utafiti wa Ardhi ili kujua mpango wa matumizi ardhi ya eneo husika kwa Mujibu wa Sheria ya Urban planning Act, ataenda Kwa msajili wa hati za Ardhi (kwa ardhi zilizopimwa na kusajiliwa) kuangalia hiyo ardhi mmiliki halali ni Nani?, Inamilikiwa kwa mfumo gani i.e ya wanandoa, au inamilikiwa na mtu zaidi ya mmoja, kuangalià Kama imekopewa kwenye benki fulani, kuangalia Kama zuio lolote limewekwa kwenye hiyo ardhi na Kama Kuna upangishaji wa muda wa muda mrefu kwa Mujibu wa Sheria ya Land registration act na Land Act, Wakili atakuongoza jinsi ya kuandika mikataba ambayo iko clear isiyo na utata ili kuepuka doctrine of contra proferetem,.
 
Mkuu CAT wametoa decision inayopiga marufuku Mahakimu kujihusisha na Mambo ya mikataba
 
Mkuu mm nikinunua kiwanja kwanza napoteza mda wiki nzima nishawasaidia marafiki kununua viwanja pia na nishawahi waokoa wengi tuu. Ww ukimalizana nao km viwanja visivyo nahati washakuonesha kiwanja kilipo nenda kwa mjumbe ulizia mmiliki nani, pia ulizia eneo lipo kwa ajili ya makazi ama laa, ukitoka hapo nenda kwa majirani hata watatu hakikisha maelezo yanafanana. Km kuna lolote utajua tuu.
 
Iko hivi, sheria haiwatambui, ila wao wakisimamia mauziano hayo ni sawa tu kama umemuita mtu yoyote yule kama shahidi tu, na sio kwa cheo chake!!yeye anachokusaidia ni kukuhakikishia kuwa anayeuza ndio mmiliki wa ardhi hiyo, japo naye anaweza kuwa hana uhakika nalo, kwenye mauziano unaweza kuwa na muuzaji , na mashahidi, na biashara ikafanyika, lakini kisheria kuna watu ambao ndio wamepewa jukumu hilo, hiyo document, ichukue ipeleke kwa wakili akuandalie , document, yenyewe ambayo hata huko mbele ukitokea mgogoro ni rahisi kuwa sehemu salama.Tatizo huwa tunakimbia gharama huko.
Inshu sio kujua background ya ardhi, kwani hao wenyeviti huwa wanakuwa na kumbukumbu tena baada ya kuchukua 10%yao?!labda mgogoro utokee baina ya pande mbili na wote muwe na hayo mavifungashio ya serikali za mitaa, , ndio wataangalia, labda muuzaji sahihi ni nani, nani alikuwa wa kwanza kunununua.
 
  • yeah nakubaliana na ww Mkuu
  • ndiyo maana mtu akiwa Wakili anakuwa na vyeo vitatu cha Kwanza Ni Wakili hiki Cheo ndiyo kinampa haki ya kuwakilisha Watu Mahakamani, Cheo cha pili ni Notary public Cheo hiki kimpa mamlaka ya kuthibitisha/kushuhudia mauziano, Cheo cha tatu ni Commissioner for Oaths cheo hiki kinampa haki ya kuandaa viapo, na kuthibitisha nyaraka nk
 
Mimi naweza kukuchezeshea hicho ulichotapeliwa na kikawa chako kweli.......
 
[emoji23][emoji23] oyaa unataka kuweka stock ya chakula nini
 
Juzi kati hapa nimeponea chupuchupu Mara 2 nikaona tu maneno siyaelewi Mara hivi Mara sijui biashara ifanyike chapchap mtu ana safari sijui nini nikaona huu utapeli live [emoji119][emoji119][emoji119] Dodoma kumekithiri utapeli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…