Nimetelekezwa na ujauzito, natafuta kazi

Atakuja mwingine naye akuzalishe... Mwanaume akikwambia nataka unizalie. Anakupima kama una akili timamu. Usikubali. Ukijipatisha mimba anajua huna akili anaku block.
 
Pole kwa yote yaliyokukuta! Ila nadhani watu mkiingia kwenye mahusiano mjue mnataka nini na kwa wakati gani kuepusha mambo kama haya!
 
Pesa ya kujifungulia inakadiliwa kuwa kiasi gani????

Nadhani ungeweka namna ya kuchangiwa so to help you cause duniani kuna watu na madudu in human form
 
Pesa ya kujifungulia inakadiliwa kuwa kiasi gani????

Nadhani ungeweka namna ya kuchangiwa so to help you cause duniani kuna watu na madudu in human form
Asante sana kwa kuguswa wangu Mungu akubariki. Ujue huku mtandaoni kumekuwa na matapeli sana. Mtu kukuchangia tu bila kukuona mhusika na uthibitisho wa kutosha n.k ni vigumu sana.

Me naomba kazi au kama kuna koneksheni ya kazi nifanye, niende uso kwa uso, nionane na wahusika laivu waone kweli huyu ni mjamzito, tuhojiene maswali watakayoniuliza kisha nianze kazi.

Ila kuchangiwa pesa hapana me nina imani kwa dini yangu sitaki kuweka mazingira ya kutengeneza utapeli hapa mtandaoni. Asante rafiki yangu...
 
[emoji1488][emoji1488][emoji1488][emoji1488]

Basi iwe Ameni hivyo hata sasa kwa Uweza wake MUNGU panapo siku ingine baada ya hii utatendewa sawasawa na hitaji la moyo wako tuseme

Amen
 
Duh asee pole sana Sista. Ajira peke yake haitoshi mana utafanya miezi miwili halafu utaenda jifungua na maternal leave itaanza, je kipindi hicho utamleaje huyo mtoto?
Naona solution ni kuwatafuta ndugu zake hiyo njemba iliyokukimbia im sure itakupa sapoti, hasa wazazi hawawezi telekeza damu yao.
 
Polee sanaaa Dada Muamini Mungu maana ndio muweza wa yote yeye aliyeruhusu kiumbe icho kuwepo hai mpka Leo hii maana take ana makusudi nacho ni lazima atatengeneza njia na hill nalo litapita na maisha yataendelea kikubwa omba toba na rehema kwa Mungu maana ni mwingi wa rehema na huruma
 
Asante kwa mawazo yako ila kwenye post yangu sijaandika kwamba nimeparamia mume wa mtu rafiki yangu. Jambo usilojua ni kama usiku wa giza me naomba endapo una koneksheni ya kazi nisaidie wangu na Mungu atakubariki. Yaliyotokea yameshatokea
 
Condoms 1000=3
 
Huyo fala, kakufanyia unyama Sana, siwezi kukulaumu ila ulivyokuwa na kazi ungeweka Ela ya kujifungulia, watu wanatafuta watoto ye anakimbia mimba, mbeleni atakutafuta tu.
 
Kutongozwa lazima, Ila akili kichwani, mbona hata si tunatongozwa pm Ila tunapangua tu, kikubwa kujiwekea mikakati, ujue Kama kakufata wewe pm kawafata wangapi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…